Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Wengi huwa tunapenda kuanzisha familia ikiwa lengo kuu ni kupeana faraja tu, bila kufikiria ili familia iwe na amani na utulivu uchumi unatakiwa uwe umetulia.
Si vema kwa mtu mwenye familia kuwa na chanzo kimoja cha mapato, mfano mshahara; mshahara siku zote huwa hautoshi na huwa unapatikana mara moja kwa mwezi.
Na unapokuwa na familia kunaweza kutokea baadhi ya changamoto na kupelekea familia kuhangaika kutafuta suluhu ya kifedha kwa ndugu, jamaa, na marafiki; na wakati mwingine kutokufanikisha kabisa.
Kama umeamua kuanzisha familia, hakikisha umeanzisha vyanzo vingine vya mapato ambavyo vitakufanya uwe huru pamoja na kufurahia familia yako.
Sio unakuwa na chanzo kimoja cha mapato, ambapo bosi wako akikukoromea tu, na familia pia inaathirika kutokana na msongo wa mawazo utakao kuwa nao kutokana na kutokuwa na mbadala.
Ni vizuri kuwa na vibiashara vidogo vidogo kutokana na uwezo wako, mfano viduka vidogo vidogo, vigenge, vibustani, vishamba, mifugo n.k.
Na si lazima uanze na mtaji mkubwa, unaweza ukajiwekea malengo ya kuanzisha vigenge labda 10, vya laki tatu tatu n.k Kuwa na mifugo itakayo kuwezesha muda wowote kupata nyama n.k
Nimeona familia nyingi wanaoishi kwa chanzo kimoja hasa mshahara (ajira), huwa wana msongo wa mawazo sana, na wakati mwingine familia zao hazina amani; jumatatu mpaka jumamamosi wako bize kazini, na asipoenda familia inateketea kwa hiyo inabidi kujilazimisha hivyo hivyo.
Muhimu, tuwe na vyanzo mbalimbali vya mapato, ili kuboresha furaha, malezi na kuwa karibu na familia zetu