Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Utakufa !!! Kifo ni inevitable hata ukiwa popote pale unaweza ukatakiwa kupata moyo lakini hakuna donor (wakati kila siku watu wanakufa na tunazika organs za kutosha)...Nakubaliana na hoja yako; ghafla umeugua na unatakiwa upelekwe India, na inatakiwa milioni 100, utafanyaje?
Au unachangisha na kuuza asset zote ili uende India ukirudi au ukifa unaachia familia na ukoo madeni ya kufa mtu...; (Dunia ya Sasa ya Credit imewafanya watu wawe na madeni mpaka kwenye Kope - Unaweza kudhani wanamiliki vingi ila ukiweka na madeni huenda hawana hata elfu moja)...
Ndio maana nimekwambia Ingawa kuna utajiri wa material / luxury things umeongezeka ila watu wamekuwa watumwa wa maisha na kuishi kama mafukara wa kutupwa..., Maisha ya kukimbizana ili upate kitu ili uweze kuishi unasahau kwamba maisha ni sasa na sio hio siku ukipata au usipopata... Tunahitaji sera za kuzalisha middle incomes wa kutosha wenye ajira zenye ujira.....; Ualimu , Udaktari, Ukulima, Ufundi sio tu kitu cha kukupatia ajira bali inabidi iwe kitu ambacho mtu anapenda kufanya - Yaani kama vile msanii hata asipolipwa asingeacha kuimba ndivyo hivyo watu wanachofanya (mfano ualimu) kiweze kuwa-sustain - Unaongelea India kwanini hio India isiwe Muhimbili (what gives)?