Familia na vyanzo mbalimbali vya mapato

Nakubaliana na hoja yako; ghafla umeugua na unatakiwa upelekwe India, na inatakiwa milioni 100, utafanyaje?
Utakufa !!! Kifo ni inevitable hata ukiwa popote pale unaweza ukatakiwa kupata moyo lakini hakuna donor (wakati kila siku watu wanakufa na tunazika organs za kutosha)...

Au unachangisha na kuuza asset zote ili uende India ukirudi au ukifa unaachia familia na ukoo madeni ya kufa mtu...; (Dunia ya Sasa ya Credit imewafanya watu wawe na madeni mpaka kwenye Kope - Unaweza kudhani wanamiliki vingi ila ukiweka na madeni huenda hawana hata elfu moja)...

Ndio maana nimekwambia Ingawa kuna utajiri wa material / luxury things umeongezeka ila watu wamekuwa watumwa wa maisha na kuishi kama mafukara wa kutupwa..., Maisha ya kukimbizana ili upate kitu ili uweze kuishi unasahau kwamba maisha ni sasa na sio hio siku ukipata au usipopata... Tunahitaji sera za kuzalisha middle incomes wa kutosha wenye ajira zenye ujira.....; Ualimu , Udaktari, Ukulima, Ufundi sio tu kitu cha kukupatia ajira bali inabidi iwe kitu ambacho mtu anapenda kufanya - Yaani kama vile msanii hata asipolipwa asingeacha kuimba ndivyo hivyo watu wanachofanya (mfano ualimu) kiweze kuwa-sustain - Unaongelea India kwanini hio India isiwe Muhimbili (what gives)?
 
Tatizo mfumo hauna muda na wewe, kinachotakiwa ni wewe kujipigania mwenyewe na familia yako.
 
Tatizo mfumo hauna muda na wewe, kinachotakiwa ni wewe kujipigania mwenyewe na familia yako.
Sidhani kama ulileta uzi kuongelea watu watatu au wanne; hata usingeongelea hayo duniani kuna percent chache wanakula na kusaza...; lakini hadi wewe kuleta uzi inamaanisha ni tatizo na ni tatizo linalowakumba wengi; solution yake itawachukua wachache ila wengi watabaki huko..., na omba isiwachukue wengi sababu ikiwachukua wengi ndicho hicho nakwambia....

Muda wa mwalimu kupita darasani na kuangalia huyu John kwanini maksi zake zimeshuka sana mwaka huu kuliko mwaka jana anapokea simu kuulize kama kifurushi chake cha mitumba alichotuma mikoani kimeshafika na kama kimefika kwanini hajalipwa ili aweze kurudisha pesa Saccos... (Lakini iwapo huyu mwalimu ujira wake ungemtosha kula kila siku, akizeeka pensheni yake ingemsukuma mpaka siku ya kufa, na watoto wake sababu wanakopeshwa na hawapewi grants wakishinda na wanatakiwa kwenye Vyuo / Veta ana uhakika watapata pesa za kupata ufunguo wa maisha (elimu) huenda huu uzi ungekuwa umeandika unauliza hivi Kati ya Serengeti na Mikumi ni wapi panavutia zaidi kwenda mida hii ya mwaka...
 
Nachukia sana ile misemo ya 'watoto ni baraka' na 'kila mtoto anakuja na sahani yake'

Inapotosha watu kuzaa hovyo bila mipango
Wanagharama; mpaka aje atoke kwako na kujitegemea labda afikishe miaka 30. Mfano, kwa siku kama anatumia 10,000 piga hesabu:-

1 mtoto x 10,000 x 365 siku x 30miaka= 109,500,000
Mtoto mmoja atakuwa ametumia nguvu zako zenye thamani ya 109, 500,000/= wakiwa 4, utazidisha mara nne.
Kwa mazingira hayo, kwa nini watu wasipate magonjwa ya akili?​
 
Hizo baraka sijui zinatokaga wapi kwa kweli
 
Na ukitaka kujua ugumu wa hili jambo pale mfanyakazi akifukuzwa kazi lazima NDOA ife na kuachana kabisa.
 
Nimekupata vizuri; ila unayetaka kumtupia lawama hana muda na wewe, ndio maana ata leo ukifariki, nafasi yako inazibwa haraka sana na mtu mwingine; na watakaoumia ni familia yako.​
 
Na ukitaka kujua ugumu wa hili jambo pale mfanyakazi akifukuzwa kazi lazima NDOA ife na kuachana kabisa.
Ni kweli, mfereji wa kuleta chakula umekufa , na uhusiano lazima ufe pia; muhimu kujikubali na kuchukua hatua mapema.
 
Mkuu umeongea madini matupu Sana, hongera Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…