Familia nchini Tanzania zanufaika na mradi wa maji uliojengwa na China

Familia nchini Tanzania zanufaika na mradi wa maji uliojengwa na China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
1743670175823.png


China ni nchi kubwa inayoendelea, na pia ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, ikiifuata Marekani. Kutokana na nafasi yake hiyo, China imekuwa mstari wa mbele katika kuzisaidia nchi nyingine zinazoendelea duniani kujipatia maendeleo kwa njia na mazingira ya nchi husika, huku ikishiriki katika ujenzi wa miradi ya miundombinu ya afya, uchumi na biashara, na sekta nyingine.

Wakati dunia inaadhimisha Siku ya Maji, ambayo huadhimishwa kila Machi 22, wakazi 450,000 katika sehemu ya kusini mwa jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania wamepata ahueni kubwa, kwani kwa mara ya kwanza, wanaweza kupata maji safi na salama.

Kabla ya mradi huo, wakazi walikuwa na muda mfupi wa kufanya shughuli za kujiingizia kipato, kwani muda wao mwingi ulikuwa unatumika kutafuta maji, tena ambayo wakati mwingine yalikuwa hayafai kutumiwa na binadamu.

Eva January Bugayane, mama wa watoto wawili na mkazi wa Bangulo kwa zaidi ya miongo miwili, anauelezea mradi huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dar es Salaam, kwamba umeleta ahueni kubwa kwake. Anasema alikuwa akiamka alfajiri kwenda kutafuta maji, na uhaba wa maji ulikuwa unaleta tishio kubwa kwa afya ya familia yake kwani walikuwa wanakosa maji ya kupikia, kufua nguo na hata kuoga. Lakini sasa, maji yanapatikana kwa wingi kwa ajili ya kila familia, na kuishukuru kampuni ya China kwa kukamilisha mradi huo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Goodluck Mwele, ambaye pia ni mwenyekiti wa kata ya Pugu Station, Bangulo, wilaya ya Ilala, anakumbuka uhaba mkubwa wa maji katika eneo hilo kabla ya mradi huo wa maji kutekelezwa. Anasema wakazi walilazimika kununua maji kwa bei kubwa, wakiyatafuta kutoka sehemu za mbali kama Ubungo, Kinyerezi na Pugu. Anaongeza kuwa, uhaba mkubwa wa maji ulisababisha milipuko ya mara kwa mara ya magonjwa yanayotokana na maji machafu kama vile kipindupindu na kuhara, lakini pia hali hiyo ilileta mvutano katika familia, kwa sababu wanawake waliondoka makwao alfajiri kwenda kutafuta maji na kurejea majumbani kwao nyakati za usiku.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, wakati mradi huo wa maji ulipotangazwa na serikali, wanachi hawakuwa na matumaini makubwa, lakini pale walipoona wafanyakazi wa kampuni ya PowerChina wakijiandaa kuanza ujenzi wa mradi huo, walianza kuwa na matumaini kwamba huenda serikali ilidhamiria kuwasaidia.

Yusufu Mtamile, ofisa rasilimali watu katika kapuni ya PowerChina, amefanya kazi katika kampuni hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja katika miradi mbalimbali, na anawasifu wafanyakazi wenzake Wachina kwa kuweka msingi wa kufanya kazi pamoja na nidhamu. Anaongeza kuwa, kufanya kazi katika kampuni ya PowerChina kumeboresha sana hali ya familia yake, kwani mshahara wake umewezesha kujenga nyumba, kuwasomesha watoto wake wanne, na pia kuweza kulipia gharama za matibabu pamoja na kulisha familia yake.

Yin Zifei, naibu mhandisi mkuu wa mradi huo, anaeleza kuwa unajumuisha ujenzi wa kituo cha pampu ya kuvutia maji, tanki la kuhifadhi maji, na uwekaji wa bomba la maji lenye urefu wa kilomita 10.8, na bwawa la maji lenye ukubwa wa mita za mraba 9,000.

Anasema mradi huo umeboresha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji salama, na mtandao huo mpya wa maji unajumuisha maeneo saba na vijiji vya mbali vilivyoko kusini mwa jiji la Dar es Salaam, na kutoka huduma ya maji kwa saa 24 bila matatizo. Pia anasema, licha ya miundombinu, mradi huo pia unalenga kujenga uwezo kwa watu wa huko, huku program za mafunzo yakitolewa kwa wahandisi wa huko katika kutengeneza mabomba, uendeshaji wa mitambo, na usimamizi wake.
 
Back
Top Bottom