Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ninafuata ushauri wa TanForm, alianza babu, baba mpaka mjukuu na kitukuu.Vitanda na magodoro katika familia nyingi za Kiafrika vimetumika kuzalishia watoto, wajukuu na hata vitukuu. Vitanda hivi vimeshuhudia mmiliki akiwa kijana au watu wakiwa wachumba, wakaoana, wakapata watoto ,wajukuu na kushuhudia wanavyozeeka hadi kufa. Pia mtu tangu aanze kazi hadi anastaafu amekuwa na Kitanda alichonunua kwa mshahara wake wa kwanza.
Bahati mbaya sana kitanda kilichotumika kukuzaa unakuta umerithishwa na wewe umekitumia kupata watoto wako. Nadhani ni kutokana na hali ya Maisha ILA MIMI NINGETAFUTA CHANGU KUPATA WATOTO NA SIO CHA WAZEE WANGU.
Anyway Nadhani sina issue nimejiandikia tu maana sina pa kwenda leo.
Kuna watu wakinunua Kitanda, godoro na kabati yaani ndio HADAIWI TENA MAISHANI , NI KAMA NYUMBA TU KWAKE.
Legendary ambaye hulalii kitanda cha urithi na ambaye umebadilisha kitanda cha kwanza na kununua godoro jipya JIPIGE KIFUANI MARA TATU UJIPONGEZE
Ni kweli ila kuna godoro lina mkojo likaanikwa weeee miaka hadi kijana naye kapata mtoto ambaye naye analikojolea. Cha kufurahisha huwa linatolewa kuanikwa sehemu ileile lilipokuwa likianikwa baba wa mtoto alipolikojolea akiwa mtoto.😂😂😂😂Mtoa mada as long as watu wanakoroma mengine hayo ni ya ziada
Tajiriiii arooooMi nishabadilisha mara mbili na mpango wa kubadilisha tena na godoro itakuwa mara ya tatu
Kama hali ya maisha hairuhusu sawa, lakini kama hali ni njema ifike sehemu kila uzao wako(mtoto) apatikane kwenye godoro lake. Na kama umeshamaliza kuzaa basi angalau badili godoro kila baada ya miaka mitano na kitanda baada ya miaka 10. Pia nguo za kuvaa isifike watu kukukariri kwa vazi lako ambalo hutaki kuliacha hadi lichanike kabisa.Godoro la tanfoam lile orijino linalodumu mpaka mjukuu analitumia kwann ulibadili
Tena ukitaka kiwe kipya unamuita fundi anakisugua kwa msasa laini kisha anapaka vanish, kinawaka ile mbaya 😄!.Ishu sio hali ya uchumi ni mazoea tu Sasa kitanda cha mninga kinachakaaje.hata miaka 1000 kinakaa.
Me nilibadili godoro tu lakini kitanda kile kile kilichobeba mabehewa ya treni nabadili tu godoro jipya kwa mtoto mpya akizaliwa.Tena ukitaka kiwe kipya unamuita fundi anakisugua kwa msasa laini kisha anapaka vanish, kinawaka ile mbaya 😄!.
Hapana sina utajiri wowote napendaTajiriiii aroooo