NI saa moja na nusu usiku!
Nyumbani kwa mzee Linus,
Nakasangwe, nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam, ndani
ya ua mkubwa wa nyumba
yake, mapambo
yamepambwa vya kutosha
na wageni waalikwa
wakianza kuingia.
Katika meza kubwa, pamoja
na watu wengine, mzee
Komba, jirani na rafiki yake
wa muda mrefu, amekaa.
Juddy mwenye umri wa
miaka 23, mtoto wa pili wa
mzee Linus alikuwa
anafanyiwa sherehe ya
kuagwa.
Kesho yake asubuhi,
alitarajiwa kupanda ndege
kuelekea Uingereza
masomoni baada ya kufanya
vizuri katika miaka yake
mitatu ya kusomea Uhandisi
katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
Familia ya Linus na Komba
ni marafiki wa muda mrefu,
urafiki wao una historia
ndefu. Walifahamiana
shuleni, walipokutana katika
michezo ya umisseta miaka
ya sabini, lakini walijikuta
wakiwa karibu zaidi
walipokutana Dar es Salaam
kikazi, mwanzoni mwa miaka
ya themanini.
Ingawa walifanya kazi ofisi
tofauti, lakini walifanikiwa
kupanga sehemu moja,
Kigogo. Baadaye, Linus
katika pitapita zake, akasikia
kuhusu kuuzwa kwa viwanja
eneo la Nakasangwe,
pembezoni mwa Kiwanda
cha saruji cha Wazo, Tegeta,
Dar. Viliuzwa kwa bei rahisi,
akamshawishi rafiki yake,
wakanunua jirani na mara
moja wakaanza kujenga!
Ingawa wote sasa ni
wastaafu, lakini wamejenga
makazi bora na familia zao
zinaendelea vizuri, wote
wakibarikiwa kuwa na watoto
wanne kila mmoja. Familia
zao ni zaidi ya marafiki,
shughuli ya kila mmoja wao,
ni shughuli ya wote. Ndiyo
maana leo mzee Komba ni
mgeni rasmi, mke wake,
ndiye anawaongoza akina
mama katika masuala ya
mapishi na vijana wa pande
zote mbili, ndiyo
wasimamizi wakuu wa
mambo ya muziki, burudani
na usafiri.
Shamrashamra ni nyingi
kweli katika mtaa huu,
muziki unasikika kwa sauti
ya chini lakini ya kupendeza,
majirani na wageni wengine
kutoka mbali wanaendelea
kumiminika katika nyumba
hii yenye eneo kubwa kwa
ndani.
Katika eneo la jukwaa,
lililotayarishwa rasmi kwa
ajili ya watu kucheza wakati
wa burudani ukifika,
mafundi walikuwa
wanamalizia kufunga
vyombo, huyu akijaribu kile
na huyu akijaribu kile.
Juddy, licha ya kwamba
ilikuwa ndiyo siku yake, naye
alikuwepo uani hapo
kuwapokea ndugu, jamaa na
marafiki waliojitokeza
kwenye shughuli hiyo.
Hadi ilipofika saa mbili na
nusu za usiku, ukumbi
ulionekana kujaa, kwani
maeneo machache tu ndiyo
yaliyoonekana kuhitaji watu.
Juddy alishaingia ndani
kubadili nguo na tayari
alisharejea akiwa amekaa
meza kuu.
Antony, kijana mwenye umri
wa miaka 14, mtoto wa tatu
wa mzee Komba, alionekana
akiingia ndani ya nyumba ya
mzee Linus akiwa amebeba
mfuko mweusi wa rambo,
ndani yake kukionekana
kuwa na kitu
kisichofahamika. Mama yake
Juddy, aliyekuwa akitokea
jikoni alimuona.
Nini hicho Tonny?
alimuuliza Antony, ambaye
alifahamika zaidi kifupi
kama Tonny, kijana wa jirani
yao.
Mama, wee subiri, kuna
sapraizi nataka kuifanya
hapa, alisema Tonny huku
akielekea chooni.
Mama yake Juddy akaguna
na kutikisa kichwa, kisha
akasema: Mambo ya watoto
bwana huyoo akaenda
zake uani kuungana na
wageni wengine!
Tonny akaingia chooni,
akaufungua mfuko wake wa
rambo. Akatoa sanamu ya
kishetani sehemu ya kichwa,
akaitazama, akatabasamu.
Akaijaribu kuivaa na kwenda
kujiangalia kwenye kioo. Yes,
alifanana na shetani kabisa!
Sasa subiri uone moto wake
hapo uani, alijisemea
kimoyomoyo, akafungua
mlango na kutoka nje ya
choo, akaanza kutembea
taratibu kuelekea uani !!!!
Nini kitatokea? Usikose
kufuatilia simulizi hii ya
kusisimua toleo lijalo!
Nyumbani kwa mzee Linus,
Nakasangwe, nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam, ndani
ya ua mkubwa wa nyumba
yake, mapambo
yamepambwa vya kutosha
na wageni waalikwa
wakianza kuingia.
Katika meza kubwa, pamoja
na watu wengine, mzee
Komba, jirani na rafiki yake
wa muda mrefu, amekaa.
Juddy mwenye umri wa
miaka 23, mtoto wa pili wa
mzee Linus alikuwa
anafanyiwa sherehe ya
kuagwa.
Kesho yake asubuhi,
alitarajiwa kupanda ndege
kuelekea Uingereza
masomoni baada ya kufanya
vizuri katika miaka yake
mitatu ya kusomea Uhandisi
katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
Familia ya Linus na Komba
ni marafiki wa muda mrefu,
urafiki wao una historia
ndefu. Walifahamiana
shuleni, walipokutana katika
michezo ya umisseta miaka
ya sabini, lakini walijikuta
wakiwa karibu zaidi
walipokutana Dar es Salaam
kikazi, mwanzoni mwa miaka
ya themanini.
Ingawa walifanya kazi ofisi
tofauti, lakini walifanikiwa
kupanga sehemu moja,
Kigogo. Baadaye, Linus
katika pitapita zake, akasikia
kuhusu kuuzwa kwa viwanja
eneo la Nakasangwe,
pembezoni mwa Kiwanda
cha saruji cha Wazo, Tegeta,
Dar. Viliuzwa kwa bei rahisi,
akamshawishi rafiki yake,
wakanunua jirani na mara
moja wakaanza kujenga!
Ingawa wote sasa ni
wastaafu, lakini wamejenga
makazi bora na familia zao
zinaendelea vizuri, wote
wakibarikiwa kuwa na watoto
wanne kila mmoja. Familia
zao ni zaidi ya marafiki,
shughuli ya kila mmoja wao,
ni shughuli ya wote. Ndiyo
maana leo mzee Komba ni
mgeni rasmi, mke wake,
ndiye anawaongoza akina
mama katika masuala ya
mapishi na vijana wa pande
zote mbili, ndiyo
wasimamizi wakuu wa
mambo ya muziki, burudani
na usafiri.
Shamrashamra ni nyingi
kweli katika mtaa huu,
muziki unasikika kwa sauti
ya chini lakini ya kupendeza,
majirani na wageni wengine
kutoka mbali wanaendelea
kumiminika katika nyumba
hii yenye eneo kubwa kwa
ndani.
Katika eneo la jukwaa,
lililotayarishwa rasmi kwa
ajili ya watu kucheza wakati
wa burudani ukifika,
mafundi walikuwa
wanamalizia kufunga
vyombo, huyu akijaribu kile
na huyu akijaribu kile.
Juddy, licha ya kwamba
ilikuwa ndiyo siku yake, naye
alikuwepo uani hapo
kuwapokea ndugu, jamaa na
marafiki waliojitokeza
kwenye shughuli hiyo.
Hadi ilipofika saa mbili na
nusu za usiku, ukumbi
ulionekana kujaa, kwani
maeneo machache tu ndiyo
yaliyoonekana kuhitaji watu.
Juddy alishaingia ndani
kubadili nguo na tayari
alisharejea akiwa amekaa
meza kuu.
Antony, kijana mwenye umri
wa miaka 14, mtoto wa tatu
wa mzee Komba, alionekana
akiingia ndani ya nyumba ya
mzee Linus akiwa amebeba
mfuko mweusi wa rambo,
ndani yake kukionekana
kuwa na kitu
kisichofahamika. Mama yake
Juddy, aliyekuwa akitokea
jikoni alimuona.
Nini hicho Tonny?
alimuuliza Antony, ambaye
alifahamika zaidi kifupi
kama Tonny, kijana wa jirani
yao.
Mama, wee subiri, kuna
sapraizi nataka kuifanya
hapa, alisema Tonny huku
akielekea chooni.
Mama yake Juddy akaguna
na kutikisa kichwa, kisha
akasema: Mambo ya watoto
bwana huyoo akaenda
zake uani kuungana na
wageni wengine!
Tonny akaingia chooni,
akaufungua mfuko wake wa
rambo. Akatoa sanamu ya
kishetani sehemu ya kichwa,
akaitazama, akatabasamu.
Akaijaribu kuivaa na kwenda
kujiangalia kwenye kioo. Yes,
alifanana na shetani kabisa!
Sasa subiri uone moto wake
hapo uani, alijisemea
kimoyomoyo, akafungua
mlango na kutoka nje ya
choo, akaanza kutembea
taratibu kuelekea uani !!!!
Nini kitatokea? Usikose
kufuatilia simulizi hii ya
kusisimua toleo lijalo!