Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
11 Ilipoishia wiki iliyopita..
Mzee Linus alikuwa
amejiinamia, kichwani
mwake akiwaza mambo
mengi, kifo kile cha kijana
wake kilimuumiza sana,
lakini alimshukuru Mungu
kwa kila jambo. Kama
aliyekumbuka kitu,
akamshika mkono mzee
Komba na kumnongoneza
jambo!
SASA ENDELEA
Kaka!
Niambie, Mzee Komba
alimuitikia rafiki yake,
kichwa chake kikiwa na
mawazo mengi.
Hivi nini kitatokea kwa
Bap? aliuliza tena
Kivipi? naye akajikuta
akiuliza.
Hii kwake itakuwa ni kesi ya
mauaji au kitu gani,?
Sidhani, ni traffic case,
alisema mzee Komba.
Ila itabidi lazima
tumwambie Bap, tabia yake
ya kuendesha gari kwa kasi
si nzuri, atamgonga mtu
sehemu wasiyomfahamu,
wanaweza kumfanyia kitu
kibaya sana, alisema mzee
Linus.
Kila siku ninamkataza,
lakini hasikii. Kuna wakati
niliamua hata kumzuia
kuendesha gari, lakini
nikashindwa, hebu
tumuache, tuamini kwamba
atabadilika mwenyewe, hasa
baada ya tukio hili.
Lakini hatujafuatilia Polisi,
nini kimemtokea?
Amewekwa mahabusu,
katika jambo kama hili,
hatuna sababu ya
kuhangaika hivi sasa, hebu
hili tulijadili kesho, mwache
alale leo,
Watu wakaendelea kujaa
pale nyumbani kwa mzee
Komba, msiba ulikuwa wa
ghafla sana. Mama yake
Tonny baada ya kuambiwa
aliyemgonga na kumuua
mwanawe ni Bap, akili yake
ikachanganyikiwa. Mambo
mengi yalipita kichwani
mwake, akajikuta akihusisha
tukio hilo na kile
kilichotokea mwaka mmoja
na nusu uliopita!
Atakuwa amefanya
makusudi? alijiuliza, lakini
sauti asiyoifahamu,
ikamtaarifu kuwa ni bahati
mbaya, naye kwa moyo
mkunjufu kabisa, akainua
mikono yake juu
akimshukuru Mungu na
kumuombea Baptist!
Baada ya kuwasiliana na
ndugu zake wa karibu
ambao walikuja msibani
pale siku ile ile, mzee
Komba akawatangazia
majirani na waombolezaji
wengine kuwa mazishi ya
mtoto wake yatafanyika siku
tatu baadaye, wakisubiri
watu wengine waliokuwa nje
ya Dar es Salaam wafike.
Hakutaka kwenda kumzika
mtoto wake nyumbani kwao
Mbinga, alitaka azikwe Dar
kwa kuwa ndipo yalipo
maisha yake!
Asfat aliwasili Dar es Salaam
saa tano na nusu asubuhi,
akakodi teksi iliyomtoa
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere na kumfikisha
Nakasagwe saa saba
mchana. Alipokelewa kwa
vilio kutoka kwa ndugu,
jamaa na marafiki. Baada ya
kuingiza begi lake chumbani
kwake, akaingia bafuni na
alipomaliza kuoga,
akamfuata mama yake na
kumuomba waongee kidogo.
Wakatoka nje kabisa ya
nyumba, ambako watu
walikuwa wametapakaa.
Wakatafuta eneo la peke
yao, wakakaa chini ya
matofali na kuanza
kuzungumza. Asfat akamtaka
mama yake amueleze ukweli
juu ya tukio lile, kwa sababu
alimwambia wazi kuwa yeye
binafsi, haamini kama ile
ilikuwa ni ajali kama ajali
zingine.
Mama akamtazama, macho
yake yakaanza kujaa
machozi, akajifuta kwa
khanga aliyokuwa
amejifunga na baadaye
akamwambia;
Hata mimi mwanzo
nilikuwa na mawazo kama
yako, sikuamini mara moja,
lakini kadiri nikirejea tukio
zima, sioni ni wapi Bap
alikusudia. Kama kuna mtu
wa kumlaumu, nilaumuni
mimi, nisingemfukuza,
asingetoka nje.
Kwa mara nyingine, Asfat
akakubali, lakini
hakuridhika!
Baada ya kumaliza
mazungumzo hayo, akarejea
chumbani kwake,
akaikumbuka albamu yake
ya picha, akaichukua na
kuanza kuziangalia picha
zake, zikiwemo za zamani
enzi za utoto hadi
ukubwani.
Akakutana na picha
aliyoipenda sana, alikuwa
amepiga na marehemu
Juddy, wakati flani wa
sikukuu ya Krismas, miaka
kadhaa iliyopita, aliipenda
picha hiyo kwa vile
ilimkumbusha mambo ya
siku hiyo, ambayo hawezi
kusahau.
Nini kitatokea? Usikose
kufuatilia simulizi hii ya
kusisimua katika toleo
lijalo.
Umerudia episode
Karudia mara mbili, ndo ujue kuna sehemu ana copy na kupest. Lakini mpenzi wangu ndo lazima uquote mpost mzima jamani? Haka kasimu nakokatumia kanawaka moto jamani.
Ha ha haaaaaaaa, ndo apate ajue na afaham eti.
Km vp tumpatie dozi ya aspirin
Njoo nikugaie umpelekee. kangekua kabinti ningekapelekea mwenyewe. Hebu nambie, hii valentine, haka kamwaga mkojo kako kalipita salama?
Karudia mara mbili, ndo ujue kuna sehemu ana copy na kupest. Lakini mpenzi wangu ndo lazima uquote mpost mzima jamani? Haka kasimu nakokatumia kanawaka moto jamani.
ndilo tatizo la wa tz mtu anangangania ni copy sawa kwani imekanushwa umeona haikufai waweza pita hivi..........siyo lazima usome