Familia tata

Familia tata

Luthar

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2011
Posts
519
Reaction score
105
NI saa moja na nusu usiku!
Nyumbani kwa mzee Linus,
Nakasangwe, nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam, ndani
ya ua mkubwa wa nyumba
yake, mapambo
yamepambwa vya kutosha
na wageni waalikwa
wakianza kuingia.
Katika meza kubwa, pamoja
na watu wengine, mzee
Komba, jirani na rafiki yake
wa muda mrefu, amekaa.
Juddy mwenye umri wa
miaka 23, mtoto wa pili wa
mzee Linus alikuwa
anafanyiwa sherehe ya
kuagwa.
Kesho yake asubuhi,
alitarajiwa kupanda ndege
kuelekea Uingereza
masomoni baada ya kufanya
vizuri katika miaka yake
mitatu ya kusomea Uhandisi
katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
Familia ya Linus na Komba
ni marafiki wa muda mrefu,
urafiki wao una historia
ndefu. Walifahamiana
shuleni, walipokutana katika
michezo ya umisseta miaka
ya sabini, lakini walijikuta
wakiwa karibu zaidi
walipokutana Dar es Salaam
kikazi, mwanzoni mwa miaka
ya themanini.
Ingawa walifanya kazi ofisi
tofauti, lakini walifanikiwa
kupanga sehemu moja,
Kigogo. Baadaye, Linus
katika pitapita zake, akasikia
kuhusu kuuzwa kwa viwanja
eneo la Nakasangwe,
pembezoni mwa Kiwanda
cha saruji cha Wazo, Tegeta,
Dar. Viliuzwa kwa bei rahisi,
akamshawishi rafiki yake,
wakanunua jirani na mara
moja wakaanza kujenga!
Ingawa wote sasa ni
wastaafu, lakini wamejenga
makazi bora na familia zao
zinaendelea vizuri, wote
wakibarikiwa kuwa na watoto
wanne kila mmoja. Familia
zao ni zaidi ya marafiki,
shughuli ya kila mmoja wao,
ni shughuli ya wote. Ndiyo
maana leo mzee Komba ni
mgeni rasmi, mke wake,
ndiye anawaongoza akina
mama katika masuala ya
mapishi na vijana wa pande
zote mbili, ndiyo
wasimamizi wakuu wa
mambo ya muziki, burudani
na usafiri.
Shamrashamra ni nyingi
kweli katika mtaa huu,
muziki unasikika kwa sauti
ya chini lakini ya kupendeza,
majirani na wageni wengine
kutoka mbali wanaendelea
kumiminika katika nyumba
hii yenye eneo kubwa kwa
ndani.
Katika eneo la jukwaa,
lililotayarishwa rasmi kwa
ajili ya watu kucheza wakati
wa burudani ukifika,
mafundi walikuwa
wanamalizia kufunga
vyombo, huyu akijaribu kile
na huyu akijaribu kile.
Juddy, licha ya kwamba
ilikuwa ndiyo siku yake, naye
alikuwepo uani hapo
kuwapokea ndugu, jamaa na
marafiki waliojitokeza
kwenye shughuli hiyo.
Hadi ilipofika saa mbili na
nusu za usiku, ukumbi
ulionekana kujaa, kwani
maeneo machache tu ndiyo
yaliyoonekana kuhitaji watu.
Juddy alishaingia ndani
kubadili nguo na tayari
alisharejea akiwa amekaa
meza kuu.
Antony, kijana mwenye umri
wa miaka 14, mtoto wa tatu
wa mzee Komba, alionekana
akiingia ndani ya nyumba ya
mzee Linus akiwa amebeba
mfuko mweusi wa rambo,
ndani yake kukionekana
kuwa na kitu
kisichofahamika. Mama yake
Juddy, aliyekuwa akitokea
jikoni alimuona.
“Nini hicho Tonny?”
alimuuliza Antony, ambaye
alifahamika zaidi kifupi
kama Tonny, kijana wa jirani
yao.
“Mama, wee subiri, kuna
sapraizi nataka kuifanya
hapa,” alisema Tonny huku
akielekea chooni.
Mama yake Juddy akaguna
na kutikisa kichwa, kisha
akasema: “Mambo ya watoto
bwana…” huyoo akaenda
zake uani kuungana na
wageni wengine!
Tonny akaingia chooni,
akaufungua mfuko wake wa
rambo. Akatoa sanamu ya
kishetani sehemu ya kichwa,
akaitazama, akatabasamu.
Akaijaribu kuivaa na kwenda
kujiangalia kwenye kioo. Yes,
alifanana na shetani kabisa!
“Sasa subiri uone moto wake
hapo uani,” alijisemea
kimoyomoyo, akafungua
mlango na kutoka nje ya
choo, akaanza kutembea
taratibu kuelekea uani…!!!!
Nini kitatokea? Usikose
kufuatilia simulizi hii ya
kusisimua toleo lijalo!
 
kwi kwi furahia mzigo kama haujaipenda waweza pita hivi
 
Iko poa sana

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
vuta subira hapa ndiyo mpango mzima majungu peleka fb kwa wale wanaotaka niweke mwendelezo hapa semeni ndiyo
 
Du? Eti tusikose sehemu ijayo...... :-d:-d
 
sasa Endelea...JUDDY
aliondoka meza kuu na
kwenda katika jukwaa
lililotayarishwa tayari kwa
sherehe. Pale alipokaa,
alisikia kama vile kuna
mkwaruzo kwenye kipaza
sauti, akasogea ili
kumwelekeza fundi mitambo
arekebishe kasoro hiyo.
Wageni wengine wote
walikuwa tayari kwenye viti
vyao na wahudumu
waliifanya vizuri kazi yao,
vinywaji mfululizo
viliendelea kutolewa na stori
za hapa na pale zikipamba
moto miongoni mwa wageni.
Watoto wadogo waliokuwa
wakicheza muziki wa msanii
Mr Nice, uitwao Kidali Poo,
ndiyo waliokuwa wa kwanza
kumuona Tonny katika
mavazi yake ya kishetani.
Walipiga kelele kubwa na
kukimbilia upande wa watu.
Kelele zile ziliwashtua watu
wote akiwemo Juddy
aliyekuwa akizungumza na
fundi mitambo, alipotazama
mlangoni, akamuona mtu
aliyeamini ni shetani…!
“Mamamaaaaaa,” Juddy
alipiga kelele na kuanza
kukimbia jukwaani. Akitafuta
sehemu salama ya
kukimbilia, kwa bahati
mbaya akakanyaga waya,
akaanguka na bila kutarajia,
kichwa chake kikaenda
kuangukia kwenye maungio
ya nyaya za umeme!
Waya mmoja ukachomoka,
ukaishia kwenye shingo
yake. Ndani ya sekunde
chache, mwili wake
ukabadilika rangi….
Kelele za kukimbia kwa
watoto na vijana wengine
zilidumu kwa muda kadhaa
kabla Tonny hajavua kinyago
kile na kuanza kucheka.
Shughuli ilishaharibika.
Wakati watu wanaanza
kurejea katika hali ya
kawaida, wakagundua mtu
aliyelala kimya ametulia
chini, pembeni ya jukwaa.
Ni Juddy!
Haraka watu wakakusanyika,
wakaogopa kumsogelea.
Fundi mitambo alijua
kilichotokea. Akazima
umeme wa jukwaani,
akamsogelea na kumgusa,
akawatazama watu kwa
huzuni.
“Jamani tumbebe, mambo
yameshaharibika,” alisema
fundi mitambo.
“Hebu subiri, nini?” Mzee
Komba aliuliza baada ya
kubaini utulivu aliokuwa nao
Juddy, moyoni mwake akajua
mambo hayako sawa.
“Hebu watoto tokeni hapa,
sogeeni kule,” alisema mzee
huyo na watoto, wakiwa
kimya, wakasogea pembeni.
Mzee Linus akasogea, mama
Juddy alikuwa amesimama
mbali, mwili ukimtetemeka!
Mmoja kati ya wageni
waalikwa alikuwa daktari, Dr
Junior. Akasogea na kwenda
kumgeuza Juddy, akamshika
moyo, akaonyesha uso wa
huzuni pia. Akatoa ishara ya
kumbeba msichana huyo.
Akabebwa na kupelekwa
kwenye gari kwa safari ya
kuelekea hospitalini.
Wakati magari yanafuatana
kuelekea hospitali ili kupata
uhakika wa nini kimetokea,
wageni waliokuwa hapo
wakaonekana wamejipanga
makundi makundi, mama
Juddy alikimbilia chumbani
kwake kujifungia, akilia kwa
uchungu.
“Sijui kama atapona, ”fundi
mitambo aliwaambia watu
waliomzunguka kutaka kujua
nini kimetokea. “Alikanyaga
waya wakati anakimbia,
bahati mbaya alipoanguka
akaangukia hapa, hizi nyaya
zikachomoka moja ikamgusa
mwilini na bahati mbaya
akailalia,” alisema fundi
huyo na kusababisha vilio
kutoka kwa watu
waliokusanyika eneo hilo.
Mzee Linus, Komba, Dr
Junior na majirani wengine
kadhaa walikuwa nje ya
Hospitali ya IMTU, eneo la
Mbezi jijini Dar es Salaam
wakisubiri ripoti ya daktari,
ingawa wote walitambua
kwamba Juddy alishafariki.
Hakuna aliyekuwa akisema
chochote, wote walionekana
kujiinamia kwa huzuni.
Aliyekuwa na hali mbaya
zaidi, alikuwa ni mzee
Komba. Kijana wake ndiye
aliyesababisha tafaruku
yote, hakuelewa nini hatima
yake.
Baada ya nusu saa, daktari
wa hospitali hiyo
aliyetambulika kwa jina la
Rama, alitokea kwenye
ukumbi waliokuwa
wamejazana watu, akaomba
wahusika wa karibu
kumfuata ofisini kwake.
“Poleni sana, mpendwa wetu
amefariki dunia. Inaonekana
ameunguzwa vibaya na
umeme, poleni sana,” Dk.
Rama aliwaambia mzee
Linus na mzee Komba
waliokuwa wamekumbatia
mikono vifuani mwao!
Nini kitaendelea?
 
sasa Endelea...JUDDY
aliondoka meza kuu na
kwenda katika jukwaa
lililotayarishwa tayari kwa
sherehe. Pale alipokaa,
alisikia kama vile kuna
mkwaruzo kwenye kipaza
sauti, akasogea ili
kumwelekeza fundi mitambo
arekebishe kasoro hiyo.
Wageni wengine wote
walikuwa tayari kwenye viti
vyao na wahudumu
waliifanya vizuri kazi yao,
vinywaji mfululizo
viliendelea kutolewa na stori
za hapa na pale zikipamba
moto miongoni mwa wageni.
Watoto wadogo waliokuwa
wakicheza muziki wa msanii
Mr Nice, uitwao Kidali Poo,
ndiyo waliokuwa wa kwanza
kumuona Tonny katika
mavazi yake ya kishetani.
Walipiga kelele kubwa na
kukimbilia upande wa watu.
Kelele zile ziliwashtua watu
wote akiwemo Juddy
aliyekuwa akizungumza na
fundi mitambo, alipotazama
mlangoni, akamuona mtu
aliyeamini ni shetani…!
“Mamamaaaaaa,” Juddy
alipiga kelele na kuanza
kukimbia jukwaani. Akitafuta
sehemu salama ya
kukimbilia, kwa bahati
mbaya akakanyaga waya,
akaanguka na bila kutarajia,
kichwa chake kikaenda
kuangukia kwenye maungio
ya nyaya za umeme!
Waya mmoja ukachomoka,
ukaishia kwenye shingo
yake. Ndani ya sekunde
chache, mwili wake
ukabadilika rangi….
Kelele za kukimbia kwa
watoto na vijana wengine
zilidumu kwa muda kadhaa
kabla Tonny hajavua kinyago
kile na kuanza kucheka.
Shughuli ilishaharibika.
Wakati watu wanaanza
kurejea katika hali ya
kawaida, wakagundua mtu
aliyelala kimya ametulia
chini, pembeni ya jukwaa.
Ni Juddy!
Haraka watu wakakusanyika,
wakaogopa kumsogelea.
Fundi mitambo alijua
kilichotokea. Akazima
umeme wa jukwaani,
akamsogelea na kumgusa,
akawatazama watu kwa
huzuni.
“Jamani tumbebe, mambo
yameshaharibika,” alisema
fundi mitambo.
“Hebu subiri, nini?” Mzee
Komba aliuliza baada ya
kubaini utulivu aliokuwa nao
Juddy, moyoni mwake akajua
mambo hayako sawa.
“Hebu watoto tokeni hapa,
sogeeni kule,” alisema mzee
huyo na watoto, wakiwa
kimya, wakasogea pembeni.
Mzee Linus akasogea, mama
Juddy alikuwa amesimama
mbali, mwili ukimtetemeka!
Mmoja kati ya wageni
waalikwa alikuwa daktari, Dr
Junior. Akasogea na kwenda
kumgeuza Juddy, akamshika
moyo, akaonyesha uso wa
huzuni pia. Akatoa ishara ya
kumbeba msichana huyo.
Akabebwa na kupelekwa
kwenye gari kwa safari ya
kuelekea hospitalini.
Wakati magari yanafuatana
kuelekea hospitali ili kupata
uhakika wa nini kimetokea,
wageni waliokuwa hapo
wakaonekana wamejipanga
makundi makundi, mama
Juddy alikimbilia chumbani
kwake kujifungia, akilia kwa
uchungu.
“Sijui kama atapona, ”fundi
mitambo aliwaambia watu
waliomzunguka kutaka kujua
nini kimetokea. “Alikanyaga
waya wakati anakimbia,
bahati mbaya alipoanguka
akaangukia hapa, hizi nyaya
zikachomoka moja ikamgusa
mwilini na bahati mbaya
akailalia,” alisema fundi
huyo na kusababisha vilio
kutoka kwa watu
waliokusanyika eneo hilo.
Mzee Linus, Komba, Dr
Junior na majirani wengine
kadhaa walikuwa nje ya
Hospitali ya IMTU, eneo la
Mbezi jijini Dar es Salaam
wakisubiri ripoti ya daktari,
ingawa wote walitambua
kwamba Juddy alishafariki.
Hakuna aliyekuwa akisema
chochote, wote walionekana
kujiinamia kwa huzuni.
Aliyekuwa na hali mbaya
zaidi, alikuwa ni mzee
Komba. Kijana wake ndiye
aliyesababisha tafaruku
yote, hakuelewa nini hatima
yake.
Baada ya nusu saa, daktari
wa hospitali hiyo
aliyetambulika kwa jina la
Rama, alitokea kwenye
ukumbi waliokuwa
wamejazana watu, akaomba
wahusika wa karibu
kumfuata ofisini kwake.
“Poleni sana, mpendwa wetu
amefariki dunia. Inaonekana
ameunguzwa vibaya na
umeme, poleni sana,” Dk.
Rama aliwaambia mzee
Linus na mzee Komba
waliokuwa wamekumbatia
mikono vifuani mwao!
Nini kitaendelea?

Mkuu endelea, mana nlikua nasoma kitabu cha mdunguaji nimekieka pembeni kwa hii story.

So pls usiikatishe namna hio
 
ILIYOPITA
...Juddy aliyeangukia
katika nyaya za umeme
wakati akikimbia
kumuogopa mtu aliyekuwa
amevaa kinyago.
Wakiwa hospitali, waliitwa
ofisini kwa daktari kupewa
matokeo ya uchunguzi wa
Juddy na kuambiwa kuwa
alikuwa amefariki dunia.
Sasa Endelea...
Taarifa rasmi ya kifo cha
Juddy ikatolewa kwa watu
waliokuwepo pale uani
nyumbani kwa mzee Linus.
Vilio vikaongezeka na ghafla
sherehe ikageuka na kuwa
msiba mkubwa. Hata hivyo,
vinywaji vilivyokuwa
vimetayarishwa kwa ajili ya
mnuso huo, vikaendelea
kuteketea.
Mzee Linus, Komba na
majirani wengine wakaingia
ndani kuuchukua mwili wa
Juddy hospitalini IMTU na
safari ya kuupeleka katika
Chumba cha kuhifadhia
maiti kwenye Hospitali ya
Mwananyamala ilianza.
Hospitalini Mwananyamala,
mtu wa chumba cha maiti
aliwapokea. Taratibu
zikaanza kufanywa ili mwili
huo uhifadhiwe.
“Poleni sana, marehemu
amefariki katika mazingira
gani?” aliwauliza. Dr. Junior
akajitokeza na kumwelezea
kwa kifupi kilichotokea.
“Aisee, sasa hii ni lazima
tupate karatasi kutoka polisi
kwa sababu hili ni tukio
linaloweza kufananishwa na
jinai,” mtu yule aliwaambia.
Walitakiwa kwenda kutoa
taarifa katika kituo cha
polisi kilichopo karibu na
eneo la tukio, jambo
lililomaanisha walitakiwa
kwenda kituo cha Wazo au
Kawe.
Mzee Komba akachukua
simu yake ya kiganjani,
akabonyeza namba kadhaa
na kuiweka sikioni. Upande
wa pili ulipokea, naye
akatoa maelezo mafupi ya
tukio lao.
Akatoa ishara ya kumtaka
mhudumu wa chumba cha
maiti kusubiri. Dakika mbili
baadaye, simu ya mezani ya
chumba cha maiti iliita,
mhudumu aliipokea.
Alionekana akipewa
maelekezo kwani muda wote
alikuwa akiitikia ‘ndiyo’ huku
akitikisa kichwa.
“Nimeambiwa niipokee maiti
lakini nyinyi lazima muende
mkapate karatasi ya Polisi
na muilete hapa ili tuweze
kuandikisha maelezo yake
kama ulivyo utaratibu,”
aliwaambia baada ya
kumaliza kuzungumza na
simu, iliyotoka kwa mganga
mkuu wa hospitali hiyo.
Wote waliitikia na kusaidia
kuihifadhi maiti katika
jokofu. Kisha wakaondoka
kuelekea Kawe ambako
baada ya maelezo, walipewa
askari mmoja na kuambiwa
watakutana na wenzao wa
Wazo tayari kwa safari ya
kwenda eneo la tukio.
Saa nane za usiku msafara
wa watu waliokwenda
hospitalini uliwasili
nyumbani kwa mzee Linus,
wakiwa wameongozana na
gari mbili za polisi aina ya
Difenda.
Baada ya kuzungumza na
wenyeji na kupata maelezo
ya jinsi tukio hilo
lilivyotokea, askari
aliyeonekana kuwa kiongozi
wao alisema.
“Yuko wapi kijana
aliyesababisha hali hii?”
Kwa mara ya kwanza watu
wakamkumbuka Tonny,
hakukuwa na yeyote
aliyemfikiria.
“Tonny, Tonny…..” watu
wakaanza kuliita jina lake,
lakini hakuonekana.
“Ni lazima apatikane,” askari
huyo alisema, hali iliyoanza
kuzua hofu miongoni mwa
waombelezaji waliojazana
ndani ya nyumba hiyo.
Akatafutwa nyumba nzima
hakuonekana, nyumbani kwa
mzee Komba pia hakuwepo.
“Anaweza kuwa amekimbia?”
askari huyo aliuliza tena na
mzee Komba akasema
hadhani kama kijana huyo
anaweza kukimbia, hasa
kutokana na udogo wa umri
wake, haonekani kuelewa
lolote.
Polisi wakaagiza kufunguliwa
kwa vyumba vyote ndani ya
nyumba ya mzee Komba.
Wakaanza chumba cha
wazazi, kisha watoto, stoo,
jikoni na kila mahali, Tonny
hakupatikana.
Wakafikia vyoo vya ndani,
mlango ulionekana
umefungwa kwa ndani.
Wakagonga, wakaita
haukufunguliwa wala
kusikika sauti yoyote.
“Antony, Antony, fungua
mlango, Antony!!!” Mzee
Komba aliita kwa sauti huku
akigonga kwa nguvu mlango,
hakukuwa na majibu.
“Inabidi uvunjwe,” askari
alisema. Mzee Komba
akatikisa kichwa kukubali.
Kazi hiyo ikafanyika, kitasa
kikavunjwa na mara mlango
ukawa wazi.
Tonny alionekana akiwa
amelala sakafuni!!!!!!
Je, nini kimempata Tonny?
Usikose kufuatilia simulizi
hii ya kusisimua katika
toleo lijalo.
 
vuta subira hapa ndiyo mpango mzima majungu peleka fb kwa wale wanaotaka niweke mwendelezo hapa semeni ndiyo

Mkuu mbona hii tunaisoma kwenye mikasa ya kusisimua ??? na bado inaendelea
 
ILIYOPITA
huku akigonga kwa nguvu
mlango, hakukuwa na
majibu.
“Inabidi uvunjwe,” askari
alisema. Mzee Komba
akatikisa kichwa kukubali.
Kazi hiyo ikafanyika,
kitasa kikavunjwa na mara
mlango ukawa wazi.
Tonny alionekana akiwa
amelala sakafuni.
SASA ENDELEA...
ASKARI alimsogelea Tonny,
akamwangalia vizuri usoni
mwake, mwili ulionekana
kuloa maji. Mzee Komba
naye akaingia chooni na
kumtazama mwanaye. Askari
akamgeuza uso ukatazama
juu.
Dr Junior, jirani yao ambaye
kwa muda wote amekuwa
karibu na tukio hili,
akawaomba wambebe kijana
huyo na kumtoa nje, kwa
sababu ya nafasi ndogo
ndani ya choo.
Tonny akatolewa na kulazwa
kwenye korido. Dr Junior
alimtazama, akamshika
kifuani kupima mapigo ya
moyo wake.
“Amepoteza fahamu,
nadhani ataamka baada ya
muda mfupi,” aliwaambia
watu ambao sasa
walishakuwa wengi ndani ya
nyumba ya mzee Komba.
“Apepewe,” askari aliamuru
na mara moja, ndugu zake
Tonny wakaanza kumpepea
kwa khanga na vitenge.
Baada ya dakika chache za
kupepewa, Tonny
alijitingisha, dalili kuwa
fahamu zinaanza kumrejea,
kisha akafunua macho,
akainuka na kukaa. Wote
walimtazama kwa hofu.
“Unajua nini kimetokea?”
Baba yake alimuuliza
mwanaye huku ameingiza
mikono kwenye mifukoni ya
suruali yake.
“Ndiyo baba,” Tonny alijibu,
machozi yakimlengalenga
machoni mwake.
“Nini kimetokea?,” mzee
Komba alimuuliza tena.
“Kule kwa kina Juddy
baba….,” Tonny akashindwa
kumalizia, akaanza kulia kwa
sauti.
“Mbadilishieni nguo,” askari
alisema, akachukuliwa na
kuingizwa ndani,
akabadilishwa nguo.
“Mzee, poleni kwa matatizo,
inauma sana. Hata hivyo,
huyu kijana itabidi twende
naye kituoni kwa mahojiano
zaidi. Mambo mengine
nadhani mtayajua huko,”
askari alimweleza mzee
Komba aliyetingisha kichwa
kukubaliana naye!!!
***
Baada ya gari la polisi
kuondoka alfajiri ile, huzuni
ilirejea upya. Mama yake
Tonny alikuwa akilia pamoja
na mama Juddy, ni tukio
ambalo halikutarajiwa na
liliwagusa wote kwa pamoja.
“Dada hata sijui nikuambie
nini, naumia sana yaani..,”
mama yake Tonny
alimwambia mama Juddy,
akimfuta machozi wakati
yeye mwenyewe akiwa
analia.
“Usijali dada, mipango ya
Mungu, ni bahati mbaya,
sote nafsi zetu zitaonja
mauti,” naye alimjibu
mwenzie, kitu ambacho
kilimfariji sana.
Siku hiyo ilitumika
kusambaza habari kwa
ndugu jamaa na marafiki
sehemu zote duniani. Msiba
huo uliwashtua watu wengi.
Aliyeumia zaidi alikuwa ni
Asfat, dada yake Tonny
aliyekuwa swahiba mkubwa
wa Juddy.
Alikuwa Birmingham nchini
Uingereza anakosoma,
akisubiri kupanda treni
kuelekea London kumpokea
shosti wake alipopokea simu
ya kaka yake, Amani. Ilikuwa
ni saa moja na nusu asubuhi
kwa saa za huko.
“Usiniambie ameshapanda
ndege tayari kaka,” Asfat
alimwambia Amani mara tu
alipoweka simu yake sikioni.
“Si bora hata angepanda
baadaye, hatapanda tena,”
Amani aliongea kwa sauti
ndogo, yenye majonzi,
iliyomshtua sana dada yake.
“Heee, imekuaje tena kaka
Amani mbona unanishtua,
baba amegoma kwani…,”
aliuliza kwa hamaki.
“Dah, dada wee acha tu,
Juddy amefariki,”
“Ni...ni...ni...?!!
Amani alimtuliza dada yake,
akamwelezea kisa kizima
kilivyokuwa, habari ambazo
zilimsikitisha na kumliza
sana. Aliyekufa ni rafiki yake
wa kufa na kuzikana na
aliyeua ni mdogo wake wa
damu!
Shughuli za msiba
zikaendelea, ukapangwa
kufanyika siku nne baadaye
ili kuweza kuwakusanya
ndugu na marafiki
waliokuwa mbali.
Kama ilivyo kawaida ya siku
zote, licha ya msiba ule
kusababishwa na wao, lakini
walishiriki kwenye shughuli
kama kawaida, wote
wakionyesha kuwa na
uchungu. Katika hali ya
kawaida, hakuna mtu
aliyetegemea yaliyokuwa
yakitokea.
Mzee Komba na familia yake
walishiriki kila hatua ya
tukio lile na mzee Linus na
familia yake nao
hawakuonyesha kinyongo
chochote, wote waliamini
kilichotokea ilikuwa ni
mipango ya Mungu.
Je, nini kilitokea?
 
Utam unakuja' utamu unakata!! Acha longolongo basi shigongo.
ILIYOPITA
huku akigonga kwa nguvu
mlango, hakukuwa na
majibu.
“Inabidi uvunjwe,” askari
alisema. Mzee Komba
akatikisa kichwa kukubali.
Kazi hiyo ikafanyika,
kitasa kikavunjwa na mara
mlango ukawa wazi.
Tonny alionekana akiwa
amelala sakafuni.
SASA ENDELEA...
ASKARI alimsogelea Tonny,
akamwangalia vizuri usoni
mwake, mwili ulionekana
kuloa maji. Mzee Komba
naye akaingia chooni na
kumtazama mwanaye. Askari
akamgeuza uso ukatazama
juu.
Dr Junior, jirani yao ambaye
kwa muda wote amekuwa
karibu na tukio hili,
akawaomba wambebe kijana
huyo na kumtoa nje, kwa
sababu ya nafasi ndogo
ndani ya choo.
Tonny akatolewa na kulazwa
kwenye korido. Dr Junior
alimtazama, akamshika
kifuani kupima mapigo ya
moyo wake.
“Amepoteza fahamu,
nadhani ataamka baada ya
muda mfupi,” aliwaambia
watu ambao sasa
walishakuwa wengi ndani ya
nyumba ya mzee Komba.
“Apepewe,” askari aliamuru
na mara moja, ndugu zake
Tonny wakaanza kumpepea
kwa khanga na vitenge.
Baada ya dakika chache za
kupepewa, Tonny
alijitingisha, dalili kuwa
fahamu zinaanza kumrejea,
kisha akafunua macho,
akainuka na kukaa. Wote
walimtazama kwa hofu.
“Unajua nini kimetokea?”
Baba yake alimuuliza
mwanaye huku ameingiza
mikono kwenye mifukoni ya
suruali yake.
“Ndiyo baba,” Tonny alijibu,
machozi yakimlengalenga
machoni mwake.
“Nini kimetokea?,” mzee
Komba alimuuliza tena.
“Kule kwa kina Juddy
baba….,” Tonny akashindwa
kumalizia, akaanza kulia kwa
sauti.
“Mbadilishieni nguo,” askari
alisema, akachukuliwa na
kuingizwa ndani,
akabadilishwa nguo.
“Mzee, poleni kwa matatizo,
inauma sana. Hata hivyo,
huyu kijana itabidi twende
naye kituoni kwa mahojiano
zaidi. Mambo mengine
nadhani mtayajua huko,”
askari alimweleza mzee
Komba aliyetingisha kichwa
kukubaliana naye!!!
***
Baada ya gari la polisi
kuondoka alfajiri ile, huzuni
ilirejea upya. Mama yake
Tonny alikuwa akilia pamoja
na mama Juddy, ni tukio
ambalo halikutarajiwa na
liliwagusa wote kwa pamoja.
“Dada hata sijui nikuambie
nini, naumia sana yaani..,”
mama yake Tonny
alimwambia mama Juddy,
akimfuta machozi wakati
yeye mwenyewe akiwa
analia.
“Usijali dada, mipango ya
Mungu, ni bahati mbaya,
sote nafsi zetu zitaonja
mauti,” naye alimjibu
mwenzie, kitu ambacho
kilimfariji sana.
Siku hiyo ilitumika
kusambaza habari kwa
ndugu jamaa na marafiki
sehemu zote duniani. Msiba
huo uliwashtua watu wengi.
Aliyeumia zaidi alikuwa ni
Asfat, dada yake Tonny
aliyekuwa swahiba mkubwa
wa Juddy.
Alikuwa Birmingham nchini
Uingereza anakosoma,
akisubiri kupanda treni
kuelekea London kumpokea
shosti wake alipopokea simu
ya kaka yake, Amani. Ilikuwa
ni saa moja na nusu asubuhi
kwa saa za huko.
“Usiniambie ameshapanda
ndege tayari kaka,” Asfat
alimwambia Amani mara tu
alipoweka simu yake sikioni.
“Si bora hata angepanda
baadaye, hatapanda tena,”
Amani aliongea kwa sauti
ndogo, yenye majonzi,
iliyomshtua sana dada yake.
“Heee, imekuaje tena kaka
Amani mbona unanishtua,
baba amegoma kwani…,”
aliuliza kwa hamaki.
“Dah, dada wee acha tu,
Juddy amefariki,”
“Ni...ni...ni...?!!
Amani alimtuliza dada yake,
akamwelezea kisa kizima
kilivyokuwa, habari ambazo
zilimsikitisha na kumliza
sana. Aliyekufa ni rafiki yake
wa kufa na kuzikana na
aliyeua ni mdogo wake wa
damu!
Shughuli za msiba
zikaendelea, ukapangwa
kufanyika siku nne baadaye
ili kuweza kuwakusanya
ndugu na marafiki
waliokuwa mbali.
Kama ilivyo kawaida ya siku
zote, licha ya msiba ule
kusababishwa na wao, lakini
walishiriki kwenye shughuli
kama kawaida, wote
wakionyesha kuwa na
uchungu. Katika hali ya
kawaida, hakuna mtu
aliyetegemea yaliyokuwa
yakitokea.
Mzee Komba na familia yake
walishiriki kila hatua ya
tukio lile na mzee Linus na
familia yake nao
hawakuonyesha kinyongo
chochote, wote waliamini
kilichotokea ilikuwa ni
mipango ya Mungu.
Je, nini kilitokea?
 
Back
Top Bottom