msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Askofu gwajima huku akijua kwamba shemeji yake ndiye amepewa dhamana ya kusiamamia mambo ya chanjo. kiungwana tu hata kama hakubaliani na chanjo kwa kumheshimu shemeji yake angeweza kusema natumia hiari kutochanjwa basi akaishia hapo ili kuepusha migogoro ya kifamilia isiyokuwa ya lazima na pengine kumharibia shemeji yake kazi.
Lakini badala yake askofu gwajima amegeuza suala la chanjo kuwa mahubiri yake ya kila siku kanisani kwake huku akihamasisha na watu wengine kutochanjwa.
Si hivyo tu, pia kwenye mahubiri yake, askofu gwajima amekuwa akitumia mahubiri hayo kumshambulia shemeji yake na kuvuruga jitihada anazofanya kuhamasisha wananchi kuchanjwa chanjo ya UVIKO-19.
Kwa sababu ya busara ndogo ya askofu gwajima na kwa sababu ya kusaka umaarufu wa kisiasa amepelekea kuwepo kwa mzozo wa kifamilia na hata kuhatarisha ndoa ya mdogo wake.
Licha ya ndoa ya mdogo wake kuwa mashakani, pia anamharibia shemeji yake kwani mwitiko mdogo wa zoezi la chanjo unatokana na kauli zake anazozitoa akiwa madhabahuni.
Kwenye ibada ya leo, askofu gwajima ndio kaharibu kabisa kwani inaonyesha ameamua kumvunjia heshima na kumdhalilisha shemeji yake wazi wazi kwamba yeye kuolewa na mdogo wake ni hasara kwa familia yao na kwamba wamekuwa hawaelewani kwa sababu yake.
Mbaya zaidi mzee gwajima naye pamoja na uzee wake inaonyesha hana hekima wala busara kwa sababu alipaswa kuwa sehemu ya usuluhishi kwa kumshauri mwanaye 'askofu' kuacha kulumbana na shemeji yake hadharani lakini naye amezidi kukoleza moto kwa kumpa go ahead ya kumdhalilisha dorothy ambaye ni 'mwenga' wake.
Kwakweli kitendo kilichofanywa na askofu gwajima pamoja na mzee wake kumtweza Dorothy ni kitendo cha aibu na kiungwana wamtafute wamuombe radhi hili jambo walimalize kifamilia kwani msingi wa matatizo yote haya bila kupepesa macho ni Askofu Gwajima.