Askofu gwajima huku akijua kwamba shemeji yake ndiye amepewa dhamana ya kusiamamia mambo ya chanjo. kiungwana tu hata kama hakubaliani na chanjo kwa kumheshimu shemeji yake angeweza kusema natumia hiari kutochanjwa basi akaishia hapo ili kuepusha migogoro ya kifamilia isiyokuwa ya lazima na pengine kumharibia shemeji yake kazi.
Ni kama vile wewe hujui usemalo..
Dr Dorothy Gwajima na naibu wake ndiyo walioanza kumkashfu Mch. Gwajima na kutukana zaidi ya watanzania 70% wasiotaka kuchanja chanjo hii kwa usalama wao. Walifikia hatua ya kuwaita hawa 70% wote ni wajinga...!!
HAPANA!. Mlango uleule alioingilia shetani, ndiyo huohuo anaotakiwa kutokea baada ya kufukuzwa...
Lakini badala yake askofu gwajima amegeuza suala la chanjo kuwa mahubiri yake ya kila siku kanisani kwake huku akihamasisha na watu wengine kutochanjwa.
Ofcoz, lazima iwe ni mahubiri ya kila siku kwa sababu ni kuhusu maisha ya watu...
Labda nikuulize, wewe ulitaka ahubiri nini?
Na in case kama ulikuwa hujui, basi ni hivi;
Biblia (Neno la Mungu) yote toka MWANZO hadi UFUNUO ni kuhusu options kwa mwanadamu kuchagua aidha maisha/uhai au kifo/mauti...!!
Si hivyo tu, pia kwenye mahubiri yake, askofu gwajima amekuwa akitumia mahubiri hayo kumshambulia shemeji yake na kuvuruga jitihada anazofanya kuhamasisha wananchi kuchanjwa chanjo ya UVIKO-19.
Nani alianza? Hebu rudi nisome hapo juu👆👆
Mlango alioingilia shetani, anatakiwa afukuzwe na atokee mlango uleule na atokomee anakostahili kuwa...!!
Kwa sababu ya busara ndogo ya askofu gwajima na kwa sababu ya kusaka umaarufu wa kisiasa amepelekea kuwepo kwa mzozo wa kifamilia na hata kuhatarisha ndoa ya mdogo wake.
Gwajima atafute umaarufu kupitia kwa shemejie Dr Dorothy..? Really?
Please, you have to try to be serious at least for a little bit...
Na nadhani kumbe wewe humjui Rev. Josephat Gwajima, siyo bure. Huyu mchungaji Gwajima ni famous DUNIANI na MBINGUNI zaidi ya miaka 20 iliyopita hawezi kuutafuta leo tena kupitia kwa mwanamke possessed aitwaye Dr. Dorothy ...!!
Licha ya ndoa ya mdogo wake kuwa mashakani, pia anamharibia shemeji yake kwani mwitiko mdogo wa zoezi la chanjo unatokana na kauli zake anazozitoa akiwa madhabahuni.
Sijui kama utaelewa. Lakini in spiritual perspective YESU KRISTO anasema hivi;
Mathayo 10: 34 - 39
"..Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani: la! Sikuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nalikuja KUMFITINI mtu na babaye, binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; na ADUI ZA MTU NI WALE WA NYUMBANI MWAKE. Ampendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye maana au binti kuliko mimi, hastahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake, ataiona...."
Haya yalishapangwa na lazima yatokee kabla ya ule mwisho Wa dunia hii haujafika. Mtazame aliyesimama upande wa Mungu muumba, msikilize na mfuate huyo...!!
Kwenye ibada ya leo, askofu gwajima ndio kaharibu kabisa kwani inaonyesha ameamua kumvunjia heshima na kumdhalilisha shemeji yake wazi wazi kwamba yeye kuolewa na mdogo wake ni hasara kwa familia yao na kwamba wamekuwa hawaelewani kwa sababu yake.
Ulitaka aseme nini iwapo kweli ndivyo alivyo? Unatetea nini hasa wewe? Tangu lini GIZA na NURU vikapatana? Palipo na NURU, basi lazima GIZA likimbie...
Soma tena kwa makini biblia yako MATHAYO 10: 34 - 39 na uelewe...
Mbaya zaidi mzee gwajima naye pamoja na uzee wake inaonyesha hana hekima wala busara kwa sababu alipaswa kuwa sehemu ya usuluhishi kwa kumshauri mwanaye 'askofu' kuacha kulumbana na shemeji yake hadharani lakini naye amezidi kukoleza moto kwa kumpa go ahead ya kumdhalilisha dorothy ambaye ni 'mwenga' wake.
Hakuna SULUHU kati ya SHETANI na MUNGU YEHOVA. Hakuna ushirika kati ya DHAMBI na HAKI. Hakuna ushirika kati ya NURU na GIZA...!!!
Soma tena NATHAYO 10: 34 - 39 na uelewe...
Nakuhakikishia jambo moja kutokea soon or later, kwamba, Dr. Dorothy Gwajima ndiyo kwa heri katika uwanja wa siasa na utawala wa nchi hii....
Yeye ndiye aliyekosea kutaka kumtumia mtumishi wa Mungu kama stepping stone kwenye political manoeuvre za nchi hii ili zimnufaishe yeye kimwili...!
Kwakweli kitendo kilichofanywa na askofu gwajima pamoja na mzee wake kumtweza Dorothy ni kitendo cha aibu na kiungwana wamtafute wamuombe radhi hili jambo walimalize kifamilia kwani msingi wa matatizo yote haya bila kupepesa macho ni askofu gwajima.
Mtu hawezi kujitweza mwenyewe halafu uanze kulaumu wengine na kujaribu kuwatwisha mzigo wa dhambi ya ujinga wako...!!
Mjadala ulikuwa ni chanjo. Huyu waziri, badala ya kujibu hoja tu zinazohusu chanjo, yeye ndiye akaanza kukosa HEKIMA na BUSARA kwa kuanza kumshambulia personal life ya shemejie Mch. Gwajima kwa kashfa za uongo. Ulitegemea anyamaziwe tu na asijibiwe..?
Nasema tena, mwiba ulipoingilia ndipo unapotokea. Vivyo hivyo, mlango alioingilia shetani ndiyo huohuo atatokea...!!