The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,778
- 8,232
Wayahudi hawakuwahi kuachana na Israeli - kumekuwa na uwepo unaoendelea kwa miaka 3000. Idadi yao ilikuwa kubwa kati ya wakazi wa Yerusalem katika zama zote. Walipungua kutokana na kukabiliwa na kufukuzwa mara kwa mara na tawala za wakazi wa kigeni (Wazungu na Waarabu) katika ardhi hiyo lakini hawakukoma kurudi. Muda mwingine walilazimika kubadilisha dini ili kulinda uhai wao.
Mnamo 1850 idadi ya Wayahudi ilizidi kuongezeka katika wengi huko Yerusalemu na maeneo mbalimbali. Sehemu kubwa za maeneo yenye rutuba yalikuwa yamekaliwa na wasio Wayahudi. Hivyo Wayahudi walilazimika kubadilisha ardhi kame ya jangwa kuwa ardhi ya kilimo kwa mikojo na vinyesi vyao. Humo waliunda vijiji vyao walivyoviita kibutiz, wakafanya kilimo, ufugaji na biashara. Wakawa matajiri kuliko wakazi wengine hasa Waarabu ambao walikuja kuomba ajira katika vijiji vya Wayahudi. Waarabu sababu ya ukata walilazimika kuuza ardhi zao zenye rutuba kwa matajiri wa Kiyahudi. Zama hizo jina Palestina lilibeba aina zote za wakazi, hakukuwa na jamii ya pekee inayoitwa Palestina bali jamii zilitofautishwa kwa majina yafuatayo;
1) Wayahudi
2) Waarabu
3) Wakristo
4) Wadruze
Jina Palestina lilianza kutumika kwa Waarabu kwa upekee kuanzia 1948 baada ya Wayahudi kutangaza taifa la Kiyahudi. Hivyo Waarabu wa hapo wakajulikana kuwa Wapalestina hadi leo hivi na wakaunda bendera yao kufuatana na rangi za bendera za nchi za kiarabu na kuanza kupigania ardhi yote kwa motto wa kuwafuta ama kuwaondoa Wayahudi hapo. Waarabu walikumbuka shuka pakiwa pameshakucha. Wamejaribu mara nyingi kuwaondoa hapo Wayahudi kwa mtutu wa bunduki lakini wameshindwa mara kwa mara na kuishia kupoteza zaidi badala ya kupata.
Idadi kubwa ya Wayahudi ilianza kuongezeka kuanzia mnamo 1917 na idadi hiyo ikaongezeka zaidi kuanzia 1940-1950 kutokana na chuki dhidi ya Wayahudi (antisemitism). Wayahudi wakatoka Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kwa kufukuzwa.
Sasa vizazi vya Wayahudi huunda idadi kubwa ya wakazi wengi katika Israeli. Nchi hiyo wameibadilisha kuwa nchi ya kupendeza. Ingawa zaidi ya Wayahudi milioni sita wanaishi nje ya Israeli na wengi wao wakiwa Marekani.
Nchi ya Israeli imetoa uraia kwa kila Myahudi aliye raia wa nchi nyingine. Hivyo hata ukiwa Myahudi uliyezaliwa na Tanzania, serikali ya Israeli inakutambua kama raia wake na inakutetea pale utakapofanyiwa dhuluma. Wanajeshi wenye asili ya Kiyahudi wameruhusiwa na Marekani kwenda kupigana endapo taifa lao la asili likiwa limekabiliwa na changamoto ya vita.