DOKEZO Familia ya Rais Kikwete yahusika ufisadi wa ESCROW

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwa mara nyingine nashuhudia mtambo wa kupika majungu ukiendelea kukaanga majungu ili Watanzania wale. Pole sana Ndugu. Prof Kikwete na familia yake hawawezi kuchafuliwa kijinga kama unavyoiga swaga za Yeriko
Kwa mtanzania mwenye mapenzi mema anajua nchi yetu imejaa viongozi wezi. Hawezi kukanusha tuhuma za Yeriko maana anajua hiyo ndiyo kazi ya wezi. Lakini kama mtanzania huyo analipwa na lumumba basi atakanusha
 

kumbe ukweli ndo huo? Kwanini wengine wanatakiwa kutolewa kafara ili watoto wa wakubwa wapone? Basi kuanzia leo tukome kuwashambulia watu wasiohusika kama prof. Anna tibaijuka ila kama ww ulijenga kwenye open space ukabomolewa basi endelea maana unahasira ya kubomolewa kwa kutokufuata sheria maana eneo la wazi unaweka mjengo na masikini wakose pakuchezea au pakukaa
 
inasikitisha sana haya mambo yanatokea kwenye nch maskin kama tanzania.
maoni yangu, bado watanzania ni wajinga na sio werevu.
 
Mimi najua kashfa yote hii kwa Rais ni kwa sababu tu ameoneha msimamo wa Taifa kutogawanywa vipande vipande kwa kivuli cha SERIKALI TATU. tunaopenda kuona Tanzania inadumu milele hakika tutamuunga mkono

TataMadiba kwetu sisi WAZALENDO tatizo ilikuwa siyo serikali tatu,sababu serikali tatu bado inahitaji research nk nk,tatizo letu kubwa ni kuyaondoa yote yaliyokuwa yameshika pabaya WATAWALA ambao kwa namna moja au nyingine ndiyo wahusika wakuu kwenye kulihujumu TAIFA,na mbaya zaidi RAIS wetu tuliyemtegemea akisema anakemea RUSHWA na UFIOSADI basi aonekane na SURA yake,mikono,miguu vyote kuwa anakemea UBADHIRIFU,lakini pale anapopigia chapuo KATIBA ya MAFISADI simwelewi na sitamwelewa kamwe!

Hivyo kubaliana nami kuwa tatizo siyo muungano,muungano umekuja ili kutoa sababu tu za kuchakachua RASIMU ya Warioba.Ubaya na wao wenyewe wamekiri,kumtukana Warioba ilikuwa ni mbinu chafu tu ili kupitisha BORA KATIBA.
 
Mkuu, ni vigumu sana kuutetea uongo. Ndivyo alivyojivua nguo Yeriko

Yawezekana kuna uwongo. Je, una uhakika yote yaliyoandikwa na Yeriko ni uwongo? Anyway umesema Yeriko anatetea uwongo wewe unatetea nini? Je, ni maisha yako? Au maisha ya chama chako cha siasa? Au unatetea nini?
 
Ewe Mungu muumba wa mbingu na nchi, ikiwemo Tanzania na watu wake walio wema na wabaya. Tunashukuri kutupatia viongozi; wengine ni waadilifu na waovu pia wamo hasa wanaohujumu rasilimali za nchi hii. Wanatumia vibaya madaraka uliyowapa kupitia kwetu wananchi. Wanaendelea kuiba rasilimali fedha na nyinginezo hata kupelekea hospitali kukosa dawa, shule kukosa walimu mahiri na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Wao wanatibiwa nje ya nchi, wanasomesha watoto wao kwenye shule nzuri nje ya nchi. Hawataki kushughulika na maendeleo ya wananchi.

Ee Mungu tuokoe Taifa lako kwa kuwapa viongozi wezi adhabu stahiki hapra hapa duniani ili sisi watu wako tunusurikge.Wasaidie watu wote wanaotetea uovu waweze kubadilika ili wasimamie haki kwa ajili ya ustawi wa Taifa lako. Waadhibu wale wote wasiokubali kubadilika kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wako ambao wanaishi kwa taabu kwa kukosa huduma mbalimbali za jamii kwa sababu ya wezi. AMINA
 

Nadhani sitamlaumu kwani ni hulka ya wanaCCM ,ukiangalia hata bungeni wanaongoza kwa kuwakashfu wenzao,na hakuna Kiongozi anayesimama kukemea.

Nadhani ulimsikia yule Mbunge wa Zanziba kwa jina la Fatma,alivyoanza kumvua Mjumbe mwenzake nguo kwa matusi machafu ya nguoni,je uliona kiongozi yeyote akimkemea?Na wa pili alivyorudisha matusi yake uliona jinsi alivyonyamazishwa na kuonywa?

Ukishayawekea alama haya,hawa wanaopenda kutukana watu hovyo na watetezi wakubwa wa viongozi siwashangai ni hulka yao na wamejijenga wao kuwa kwao kutukana ni haki yao lakini ni mwiko kutukanwa!
 
Acheni kuropoka humu jf,tunachohitaji ni ripoti ya CAG na PCCB,tujue mbivu na mbichi,mngejua maumivu tunayopata walah msingeingiza siasa ktk hili jambo,lkn sababu baadhi yenu hamjielewi basi GOD WILL FORGIVE YOU,mnashabkia ubadhirifu whle hosp hazna dawa.
 

mkuu hujaeleweka au labda mimi sijakuelewa. Hebu twende taratibu. Tuamini vipi kuwa miraji ana kampuni bila ushahidi wowote, lakini hapo hapo tumtake miraji akanushe akiwa na ushahidi? Unatakiwa uwe na ushahidi gani kuwa hauna kampuni hiyo?
 

Watakuwa na hisia za kuwa Watanzania ni wajinga lakini hawatajua ni lini ujinga utakoma na kudai tulichodhulumiwa....Pole Mtanzania
 
Viongozi wakuu wa upinzani......watakuwa ni Mbowe na Dr Slaa
 
mkuu hujaeleweka au labda mimi sijakuelewa. Hebu twende taratibu. Tuamini vipi kuwa miraji ana kampuni bila ushahidi wowote, lakini hapo hapo tumtake miraji akanushe akiwa na ushahidi? Unatakiwa uwe na ushahidi gani kuwa hauna kampuni hiyo?

Wewe ndio haujamuelewa Olesaidimu, ngoja sasa nikueleweshe ni hivi ukichafuliwa kuna chombo maalum cha kusafisha watu nacho ni mahakama.

Mahakama ndio itamtaka mtuhumu athibitishe tuhuma dhidi ya mlalamikaji na akishindwa kuthibitisha mahakama inakusafisha na unaweza funguwa na kesi ya madai.

Angalia mfano hapa Billionare Manji amemfungulia kesi Billionare Mengi akimdai fidia ya shilling moja kwa sababu shida siyo pesa bali anataka mahakama imsafishe.

Kwa maelezo haya kama hujaelewa basi inabidi ukafanyiwe check up Baltmore.
 
.......ukiwa kiongozi hodari ni tiketi ya kula na kuvimbiwa mkuu?? (hoja yako bado ni nyeupe kwa utetezi, japokuwa kushindwa kwako kutetea hakumaanishi kwamba tuhuma ni za kweli)
 



Yericko Nyerere uliyeleta huo uongo, leta ushahidi.
 
Last edited by a moderator:
Basi waengine wasitolewe kafara. Watolewe kafara kwanza ikulu na familia ya mh. Kwanza then basi
 
Balaaaa kubwa kabisa hili jamani

Minimeamua kuludi shamba nalima, huku situmii umeme wala staki kuusikia sasa muibiane hukohuko town, atakae jipendekeza kuja kuninyanganya shamba langu nazaa nae apa niko full nina ak na mabomu kibao na polisi mje kujipendekeza kuniuliza nimevipata wapi mtakula risasi za ------ wote ninahasira mbaya , yaani kumbe mrisho ndio master mind hapo hakuna cha c.a.g wala takukuru watazuga tu, watz hii ni vita hao sio watu nimakenge na inaonekana wako tayari kwa lolote tujipange sio story tu
 

Hoja hapa si miraji hoja ni hawa wanaotoa tuhuma bila ushahidi kutaka anayetuhumiwa ndie athibitishe. kama hujaelewa hili.....
 
.......kila post Lizabon anapewa 7000 kama wale vijana walionyanyua mabango wakati wa mdahalo; ndio rate zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…