DOKEZO Familia ya Rais Kikwete yahusika ufisadi wa ESCROW

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
kumbe sio Rizimoko peke yake ndio jizi, hadi boya miradji kastuka now though to late, hilo changa la macho 50% ni ya jakaya mwenyewe hao watoto wamewekwa kama geresha tu
 
Yericko angekuwa mzima angeweka hata kipande cha ushahidi ningemuona mtu lakini kutunga tunga tu kama isha mashauzi haina mashiko.



Na ni sababu hiyo pia baada ya Dr Hosea kuwasilisha report kwa rais, JK alisoma na kumjibu achana nayo na ndio maana mpaka sasa report hiyo haijapelekwa kwa DPP ili.wahusika wafikishwe mahakamani.
 

Je ni kweli Brela haiwajui wamiliki wa Simba Trust? Hapa ndipo kuna mzizi wa fitina kwa nini ESCROW haigusiki; kila anayejaribu kuigusa anaungua vidole. Huyo mhindi koko Harbinder Sing Sethi kweli anajua kucheza karata zake!
 
Duuu! fedheha kubwa kama kweli,yani mapesa yote hayo na mnalala usingizi wakati watoto wawenzenu wakufa kwakukosa dawa hospitali nyie mnajivutia mipesa na watoto wenu,mwenyezi mungu hamfichi dhalim,dua za wanyonge hulipwa na mungu,sasa wamegeuka samaki walana wao kwa wao.....
 

Slaa alishinda kwa kura nyingi tu,ishu yote ikowazi,ccm huwa haishindi kihalali siku zote,matokeo halisi yanajulikana hata wewe unajua,jk wako alishindwa vibaya kwenye huo uchaguzi,kilichomsaidia ni huruma ya watu kuwa ni aibu yeye kukaa kipindi kimoja ili hali wenzake walikaa vipindi vitatu,ndipo aliposaidiwa kushinda kwa kuchakachua.
 
Hii ni zaidi ya Richmond. Lakini ni watanzania wangapi wanaoelewa hii kitu, ni wengi wa kutosha kuweza kufanya mabadiliko. Kwanini wako kimya? NI ama wanafaidika na mfumo dhalimu wa kiunyonyaji au wanahusika na kutengeneza njia mbovu za kifisadi kuweza kuishi maisha ya anasa.

Yote kwa pamoja yanaondoa heshima na thamani tuliyoipata kama wanataaluma. Nikupongeze Yericko Nyerere na wengine kwa kutokukata tamaa na kuendelea kupigia kelele uozo huu wa makusudi na kimkakati wa kuumiza mamilioni ya watu kwa kuwakosesha huduma muhimu.

Ifike mahala mafisadi waogope hata kufikiria kujaribu..!
 

Weka ushahidi wa nyaraka, haya maneno matupu hata mie ningeweza kuyatunga na kuyaandika humu JF

mkuu, huo ushahidi ataupata wapi ilhali hayo ni maneno ya kutunga? Lengo ni kumchafua Rais na familia yake
 
Kama alishinda halafu ikaweje mbona anazunguka mitaani kuuza sura wenzake wanatumikia waliowachagua yeye alishida ikawaje?
 
Nimepata mshtuko sana, zaidi kuna watu hapa badala tuungane pamoja kupinga ubadhirifu huu wao wanakejeli tu hii ni hatari sana,

Tusubiri tuone kati ya wananchi na familia ya Rais nani muhimu zaidi? nina hofu kuwa report hizo zitakanyagwa sana hadi kuletwa bungeni zitabaki mifupa tu....
 
mkuu, huo ushahidi ataupata wapi ilhali hayo ni maneno ya kutunga? Lengo ni kumchafua Rais na familia yake
Hata hivyo Rais hachafuki angalia wanaomuunga mkono lakini wanaomchafua ni bavicha tu.
 
Kama alishinda halafu ikaweje mbona anazunguka mitaani kuuza sura wenzake wanatumikia waliowachagua yeye alishida ikawaje?

mkuu, hawa jamaa wanajifariji sana. Mtu anashindwa hata kuoa ataweza kushinda urais? Aoe kwanza ndipo afikirie kugombea urais
 

Yericko ili kuondoa utata na ukakasi wa hili jambo..ni vyema utuambie pasipo shaka hiyo Kampuni ya Simba trust ya Australia imesajiliwa hapo BRELA kwa majina hayo halisi au..na kama kuna ushahidi pia uweke ili usije ukaambiwa unafanya ushabiki wa wa kisiasa tu ama unaichukia familia ya Mheshimiwa Rais japo kwa kweli ni hatari. Tusaidie katika hili mkubwa japo lisemwalo lipo......
 

umeandika kwa staha sana. Ningekuwa mimi ningemwambia Yeriko alete ushahidi la si vyo nitamchukulia hatua kwa kujaribu kuihusisha familia ya Rais na maovu
 
Simba trust ni nan.? Uchunguzi umeonesha kuwa Simba trust ya Australia inamilikiwa na watu wawili ambao ni salima Kikwete na Miraji Kikwete.

Simba Trust inayomiliki 50% ya IPTL/ PAP ya nani?
Mkuu Yeri, asante kwa taarifa hii, ila kama huko juu umeishasema uchunguzi umekuonyesha wamiliki wa hii kampuni ni kina fulani!, huwezi tena kumalizia kwa kuuliza swali ambalo tayari uchunguzi wako umeisha lijibu!.

Hii inamaana moja tuu, ama huna uhakika na hiyo ripoti ya uchunguzi, ama unajua kabisa kuwa sii kweli, ndio sababu ya hiyo inconsistance yako!.

Lakini ikitokea ikawa ni kweli, fuatilia umri wa hao wamiliki, kama wote wamevuka the age of the majority, then sio lazima kuwa ni mali ya familia, kwa sababu mtu akiisha vuka 18, ni legal person on her/his own independent of wazazi wake!.

Kama walikuwa hawajavuka 18!, hii inamaanisha na jamaa anafuata nyanyo za mtangulizi wake, "kufanya biashara "mahali patakatifu" pale!.

Pasco
 

mwambie nduguyo Yeriko aweke ushahidi humu kutokana na huu upuuzi aliouweka vinginevyo ajiandae kuwajibika kwa uzushi huu
 
Ndio maana wamechakachua katiba mpya. Kungekuwa na katiba bora inayobana watawala Rais angetakiwa ajiuzulu mara moja na watoto wake wafunguliwe mashtaka.

Kinachonishangaza ni ujinga wa mwafrika kushabikia hata kifo chake kisa anashabikia chama na kiongozi. Wale wanaopiga debe humu ndani kutetea katiba mpya iliyopendekezwa na bunge maalum la CCM hawana mbele wa nyuma zaidi ya pesa ya leo wanayopewa na watawala lakini hawajui wapo watoto wa shangazi zao, kaka zao, ukoo wao au kabila lao wanaokufa kwa kukosa dawa kwa ufisadi wa kishenzi kama huu wa mtawala anayemshabikia kijinga.

KATIBA MPYA ILIYOPENDEKEZWA YA WATAWALA TUIPIGE CHINI TUTENGENEZE KATIBA MPYA BORA ITAKAYOTUPA HESHIMA NA KUJENGA NCHI YETU. SIYO HIZI AIBU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…