Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Mtu aliyepora uchaguzi nchi nzima ashindwe kufanya kitu km hiko… tatizo jiwe alikuwa na mihemko na hapendi kukosolewa.!!

Muhimu wote wamekufa wahukumiane huko huko walipo.!! Sijui alishapewa uongozi wa kuongoza malaika 🤣
 
Naunga mkono hatua kuchukuliwa, lakini kwa mkondo tofauti. Aliyetuhumiwa ni aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio baba wa familia ya Magufuli. Kwahiyo, Mimi nashauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio inatakiwa ilifanyie kazi hili ili kuondoa dhana kwamba Marais wetu wanafanya vitendo vya kukiuka Katiba wakiwa Ikulu.
 
Mahakama zipi, hizi zilizokaa na kesi ya kina Mdee kwa miaka zaidi ya minne? Au unadhani hatujui kwanini Magufuli na genge lake waliweza kutekeleza uovu ndani ya nchi hii?
Mbona sanga kaachiwa juzi na makada wa chadema wameishukuru mahakama kwa kutenda Haki au ni mpaka Chadema ishinde kesi ndio mahakama ionekane inatenda Haki?
 
Marais wetu wengi huwa wanafanya uhalifu sana wakiwa ikulu, ila tuna katiba inayowafanya kuwa miungu watu. Kwakuwa Magufuli alikuwa ni kiongozi muovu, alifanikiwa kufanya uovu wake kwa katiba hii mbovu.
 
Ndugu Kabendera ni mtu wa ajabu sana....

Sisi ni waafrika....watanzania...wajamaa.....

Kamwe huwezi kumchafua KIONGOZI WETU MKUBWA KABISA kwa sababu ya maslahi yako KOKO ya nchi za nje na maadui wa Tanzania yetu na TURATHI ZAKE......

#Nchi Kwanza kwa njia yoyote ile.
#Viongozi wakuu wa taifa ni tunu yetu.
#Sisi ni waafrika ,sisi ni wajamaa wa Afrika.
 
Mbona sanga kaachiwa juzi na makada wa chadema wameishukuru mahakama kwa kutenda Haki au ni mpaka Chadema ishinde kesi ndio mahakama ionekane inatenda Haki?
Acha upotoshaji wa kijinga, hawajaishukuru mahakama kwa kutenda haki, bali wameshukuru hao jamaa kuachiwa. Mahakama ingekuwa inatenda haki wasingekaa ndani miaka minne kwa kesi ya kubambikiwa.
 
Kuwa kiongozi hakukufanyi kuwa mtakatifu, na Magufuli alikuwa mfano mmojawapo wa viongozi waovu.
 
I’m all for it. Ila Kabendera naye ni lazima atoe ushahidi na awataje waliomwambia.
The truth is, hakuna sababu ya msingi za kwanini serikali imeshindwa kuleta majibu kuhusu Ben. Alishatoa taarifa, kwa polisi na hata hapa JF kuhusu vitisho, mpaka namba ya simu ya wanaomtishia aliweka hapa. Inakuwaje with all the leads, hakuna chochote kuhusu kupotea kwake?

It's time hili jambo lirudi kwenye vichwa vya watanzania, he may be wrong kutoa serious allegations kama hizi, lakini kuna namna Watanzania tulichezewa sana kwenye issue ya Ben.
 
Kusema ukweli ndiyo kumchafua? Magufuli alikuwa muuaji hilo halina ubishi ndiyo maana Mungu aliamua huu ugomvi kwa kumtowesha kwenye uso wa dunia.
 
Unajaza hadithi za Mudi humu fungua uzi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…