Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Katika madai yote dhidi ya Rais Magufuli, hili dai la huyu mwandishi Eric Kabdendera, kuwa Rais Magufuli alimuua Ben Saanane kwa kumpiga risasi ya kichwa hapo Ikulu [nasadiki ni Ikulu ya Dar], ni dai kubwa na zito sana.

Ni kashfa kubwa sana. Kwa mtu tu wa kawaida, kutuhumiwa kuua mtu mwenzio si jambo dogo. Seuze Rais wa nchi?

Wengi wetu kwa sasa tutakuwa tumeshaiona hii excerpt ya hicho kitabu:
View attachment 3190381

Napata wakati mgumu sana kuamini kuwa Rais Magufuli anaweza kumuua kijana wa Kitanzania, ambaye ni mtu mdogo sana, in the grand scheme of things, kwa mikono yake mwenyewe tena kwenye nyumba ya wananchi, Ikulu.

Tumeshawazoea akina Lissu na wenzake kuropoka na kutoa tuhuma za ajabu ajabu bila kutoa wala kuonyesha ushahidi wowote ule zaidi ya kusema ‘nimeambiwa’ au ‘niliambiwa’.

Lissu keshawahi kusema mara kadhaa kuwa baada ya Magufuli kufariki, eti nyumbani kwake yalikutwa mabulungutu ya mahela, dola za Kimarekani, kwenye mamilioni.

Bila ushahidi wowote ule zaidi ya ‘kuambiwa’, tuhuma hizo zinabaki kuwa ni porojo tu za Lissu.

Na ndo maana pengine hata familia ya Rais Magufuli haijawahi kusema wala kufanya chochote dhidi ya madai hayo.

Ila hili la Magufuli kutuhumiwa kuwa ni cold-blooded murderer, si la kawaida na halipaswi kupuuziwa.

If not true, what Kabendera did is libelous and should sued.

Mimi si mtaalamu wa sheria za Tanzania. Lakini naamini sheria za libel zipo.

Licha ya kwamba Rais Magufuli alikuwa ni public figure, kuna vitu huwezi kuvisema dhidi yake bila ushahidi.

Tuhuma za mauaji kwa mtu yeyote yule, humtia doa kubwa sana kwenye jamii, mtu huyo.

Majuzi hapa tumeona kituo cha televisheni cha Marekani, ABC, kilikubali kumlipa Rais Trump $15 milioni kwa sababu mmoja wa watangazaji wake alisema kimakosa kuwa Trump alipatikana na hatia ya ubakaji wakati si kweli.

Kubaka ni moja ya makosa yanayompa mtu doa la maisha.

Uuaji, kwangu mimi, ni kosa lililo juu ya ubakaji.

Sasa huyu jamaa Kabendera anakuja na tuhuma nzito namna hiyo tena kwa Rais mzima bila hata ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kaambiwa na vyanzo vyake.

Hapana kwa kweli. Tuhuma kama hizo ni nzito sana kuachwa hivi hivi tu, la sivyo kama ni za ukweli.

Familia ya Rais Magufuli ikimwacha huyu jamaa bila kumburuza mahakani akatoe testimony yake huko under the penalty of perjury, itakuwa ni usaliti mkubwa sana kuwahi tokea nchini.

Yaani kabisa Rais Magufuli ampige risasi ya/za kichwa huyo Ben Saanane hapo Ikulu, halafu watu wa Magufuli waichukue maiti yake na kwenda kuitupa kwenye moto Rufiji?

Vigumu sana kuamini hilo.

Familia ya Rais Magufuli ni lazima ichore mstari mchangani na kuchukua hatua.

La sivyo, mtatufanya watu kama mimi tuamini kuwa yanayosemwa ni ya kweli.

Kama kweli hiyo picha ipo kwenye hilo cover la kitabu. Huyu jamaa alipaswa sasa hivi awe ameshatiwa nguvuni na vyombo husika na siyo vinginevyo
 
Waruhusu taasisi kutoka nje ya kimataifa kufanya uchunguzi wake tusikie .....kama mnaweza kumshauri raisi wenu shauri na ilo .........aw walikufa wangekua ndgu zenu pimbi nyie msingekua nakiherehere icho
 
Angalau sasa umejaribu kujibu japo historia inakupinga. Muhammad hakuwahi kuwa kiongozi wa kisiasa pale Madina na ilifika wakati mamlaka za mji zilianza kumsaka/kumtafuta kwa kosa la kuhamasisha vurugu na chuki na akakimbilia milimani huko. Huo uongozi alipewa na nani ikiwa alikimbia mji kwa kusakwa na mamlaka!?
Ww ni Chakubanga
 
Sasa wewe na makafiri wenzio wasomi maprofessor nani anajua? Wewe mvuta bangi wa ubungo unapinga. Professor mkatoliki wa marekani anaandika wewe unapinga. CHUKI ZAKO HAZIONDOSHI UKWELI
Eti Professor Mkatoliki Mmarekani.... Simple research ingekupa majibu sahihi. Thomas Carlyle was never a Catholic and not an American. He was Scottish and a protestant. Learn to get your facts straight, punguza upotoshaji
1735794851375.jpeg
 
Hiyo ni tuhuma ya serkali wala sio ya familia. Akifikishwa mahakamani yeye ndio atathibitisha hayo pasipo shaka kuwa Magufuli alimpiga risasi kwa mkono wake. Lkn kwa kuwa kuna watu watudanganya ymeti hiyo nayo ni sehemu ya 4R na demokrasia wanapiga kinya,, simetime kuogopa nchi wanaotupa ugali ilitule tuzaane wauze bidhaa zao. Israeli inapiga watu hakuna cha ICC wala Human right wala nani wanaongea lkn haiwasikilizi hiyo ndio inaitwa kujitambua., huwezi kuja kuteka watu na wattoto halafu eti waje sijui Human right waanze maneno walitakiwa wamkemee kabla hajafanya ujinga. Wakati fulani bora uwe maskini lkn utu wako ubaki . Labda kamaserkali wanajua ni wahusika na dhamira zao zinawasuta. Waafrika na Waarabu tuko na shida mkichwa
 
Story za Muhammad zinachanganya sana! Mpaka anaagiza uchunguzi alikuwa kiongozi wa kijamii au kidini? Na kama alikuwa kiongozi mbona jina lake si kati ya historia ya majina ya viongozi wa Maka/Madina?
Ni logic tu ndogo wewe unadhani kuna mtu angeweza kumuongoza mtume? yeye ndo alikuwa kiongozi na alihusika na ukuzaji wa dola ya kiislamu na viongozi wanne maswahaba waliofuatia baada ya yeye kufariki wanaitwa makhalifa yaani waliokaa nafasi yake.

Alikuwa ndio amri ya mwisho katika wakati wake na ndio maana aliwapelekea barua mbalimbali viongozi wa roman, Persia n.k kuwaita kwenye uislamu.
 
Saa100 aliibukia Tanga,anatumbia Yuko ziara ya kikazi akitokea Unguja, anatuambia magufuli anatusalimia,wakati hatujamuuliza ,usiku anavaa gauni jeusi bila kupeperusha bendera ya Taifa,anasema Magufuli amefariki.
As simple as that!
Na Waziri Mkuu anasema Magu yupo ofisini anachapa kazi.
 
Mtume alisisitiza kuwa kuchelewesha haki au kuzembea katika kushughulikia dhuluma kunaweza kusababisha Mtaarufuku mkubwa katika jamii
Sahihi kabisa.....

Kutotolewa ripoti za uchunguzi za kupotea kwa watu na mamlaka husika ndio kunafanya watu binafsi kama kina 'Kabendera' kufanya chunguzi zao binafsi na kuibuka na tuhuma kama hizi.
 
Katika madai yote dhidi ya Rais Magufuli, hili dai la huyu mwandishi Eric Kabdendera, kuwa Rais Magufuli alimuua Ben Saanane kwa kumpiga risasi ya kichwa hapo Ikulu [nasadiki ni Ikulu ya Dar], ni dai kubwa na zito sana.

Ni kashfa kubwa sana. Kwa mtu tu wa kawaida, kutuhumiwa kuua mtu mwenzio si jambo dogo. Seuze Rais wa nchi?

Wengi wetu kwa sasa tutakuwa tumeshaiona hii excerpt ya hicho kitabu:
View attachment 3190381

Napata wakati mgumu sana kuamini kuwa Rais Magufuli anaweza kumuua kijana wa Kitanzania, ambaye ni mtu mdogo sana, in the grand scheme of things, kwa mikono yake mwenyewe tena kwenye nyumba ya wananchi, Ikulu.

Tumeshawazoea akina Lissu na wenzake kuropoka na kutoa tuhuma za ajabu ajabu bila kutoa wala kuonyesha ushahidi wowote ule zaidi ya kusema ‘nimeambiwa’ au ‘niliambiwa’.

Lissu keshawahi kusema mara kadhaa kuwa baada ya Magufuli kufariki, eti nyumbani kwake yalikutwa mabulungutu ya mahela, dola za Kimarekani, kwenye mamilioni.

Bila ushahidi wowote ule zaidi ya ‘kuambiwa’, tuhuma hizo zinabaki kuwa ni porojo tu za Lissu.

Na ndo maana pengine hata familia ya Rais Magufuli haijawahi kusema wala kufanya chochote dhidi ya madai hayo.

Ila hili la Magufuli kutuhumiwa kuwa ni cold-blooded murderer, si la kawaida na halipaswi kupuuziwa.

If not true, what Kabendera did is libelous and should sued.

Mimi si mtaalamu wa sheria za Tanzania. Lakini naamini sheria za libel zipo.

Licha ya kwamba Rais Magufuli alikuwa ni public figure, kuna vitu huwezi kuvisema dhidi yake bila ushahidi.

Tuhuma za mauaji kwa mtu yeyote yule, humtia doa kubwa sana kwenye jamii, mtu huyo.

Majuzi hapa tumeona kituo cha televisheni cha Marekani, ABC, kilikubali kumlipa Rais Trump $15 milioni kwa sababu mmoja wa watangazaji wake alisema kimakosa kuwa Trump alipatikana na hatia ya ubakaji wakati si kweli.

Kubaka ni moja ya makosa yanayompa mtu doa la maisha.

Uuaji, kwangu mimi, ni kosa lililo juu ya ubakaji.

Sasa huyu jamaa Kabendera anakuja na tuhuma nzito namna hiyo tena kwa Rais mzima bila hata ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kaambiwa na vyanzo vyake.

Hapana kwa kweli. Tuhuma kama hizo ni nzito sana kuachwa hivi hivi tu, la sivyo kama ni za ukweli.

Familia ya Rais Magufuli ikimwacha huyu jamaa bila kumburuza mahakani akatoe testimony yake huko under the penalty of perjury, itakuwa ni usaliti mkubwa sana kuwahi tokea nchini.

Yaani kabisa Rais Magufuli ampige risasi ya/za kichwa huyo Ben Saanane hapo Ikulu, halafu watu wa Magufuli waichukue maiti yake na kwenda kuitupa kwenye moto Rufiji?

Vigumu sana kuamini hilo.

Familia ya Rais Magufuli ni lazima ichore mstari mchangani na kuchukua hatua.

La sivyo, mtatufanya watu kama mimi tuamini kuwa yanayosemwa ni ya kweli.
Kama hakuhusika ufanyike uchunguzi huru na sio kumtetea mwendazake.
 
‘nimeambiwa’ au ‘niliambiwa’ -

Siri ipo hapa, Hakuna mahakama inayoweza mfunga ulimwengu huu kwa hayo maneno
 
What you soul you shall reap .

Familia haina sababu ya kuhangaika kumtetea baba yao , ipokee kila kitu na kukichukulia Kama sehemu ya mavuno ya Kazi ya mzee wao.

Kabendera yupo katika marking time yake anaamua kwenda mbele au arudi nyuma tofauti na hapo atajiumiza .

Kama ameamua kutoa ya moyoni aendelee kuyatoa tu na Kama ameamua kukaa kimya akae kimya .
 
Back
Top Bottom