USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 10,904
- 26,184
Baada ya mwanaharakati na mtungeneza maudhui Fortunatus Buyobe kudai kuwa SSP Fatuma Kidongo ndio anayetajwa kama afande na wabakaji wakati sio kweli mwanasheria wa familia amedai kuwa mteja wake atafungua kesi (Defamation)
Familia ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (SSP), Fatuma Kigondo imesema inafikiria kufungua mashtaka dhidi ya wote waliosambaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa ndugu yao amehusika kutuma vijana kufanya ukatili kwa binti wa Yombo Dovya, Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Mwanasheria wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Emmanuel Muga, kupitia ukurasa wake wa X (Twitter) ilieleza kuwa ndugu wa Askari polisi huyo waliwasiliana naye na kumweleza kusudio lao hilo, wakiwa na maelezo kuwa wanataka kuhakikisha haki inatendeka na ukweli wa jambo hilo unafichuliwa.
Alisema familia hiyo ilimweleza kuwa SSP Fatuma siyo afande aliyezungumziwa kwenye video hiyo na kuwa ndugu yao ni ofisa wa polisi mwenye cheo cha SSP na si ASP kama ilivyodaiwa mtandaoni.
"Aidha, familia imethibitisha kuwa SSP Fatuma ni mjane na hana mume ambaye angeweza kuporwa kama ilivyosemwa," alisema.