Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Hatimaye familia ya mfanyabishara Daisle Ulomi aliyefariki na mwili wake kukutwa mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, imesema kuwa ndugu yao ni kweli alifariki kwa ajali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 17, 2024, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema ajali hiyo ilitokea Ubungo Extenal Makuburi mchana na walitokea wasamaria wema waliosaidia kumpeleka mwili huo hospitali.
"Tukio lile lilitokea mchana kweupe na wasamaria wema waliojitolea wenye ubinadamu na utu licha ya kwamba ilikuwa ajali mbaya ambayo kama ukiona ule mwili utajua ni kwa nini hata ndugu walipopita mochwari walishindwa kumtambua," amesema.
Akizungumza na wanahabari leo Mikocheni ambako familia imeweka msiba, msemaji wa familia hiyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko amesema baada ya mwili kupatikana Mwananyala walipigiwa simu kisha baadhi ya ndugu walienda kuangalia na kuutambua.
"Tupo kwenye taratibu za maombolezo ya kwenda kumstiri ndugu yetu ambaye alipata ajali Desemba 11, 2024 saa 7:55 mchana katika maeneo ya Gereji akiwa anatokea Barabara ya Mandela baada ya kutokea ajali watu wema walimpeleka kituo cha afya Makuburi," amesema.
Soma, Pia: