chama mpangala
JF-Expert Member
- Sep 3, 2015
- 623
- 942
FAMILIA YA WAHHABI NA NGUVU YA ILLUMINATI KWENYE DINI YA KIISLAMU ILI KUTIMIZA MALENGO YAO.
Illuminati walikuwa hawamtaki tena Shah, na Khomein ndiye aliyekuwa kibaraka wao mpya. Akiwa hapo alipokea msururu wa wageni kutoka BBC, CIA na kutoka kwenye shirika la kijasusi la Uingereza. BBC wakawa ni promota namba moja wa Khomein. (Angalia, Goodgame, Globalists and the Islamists. The British, the Middle East, and Radical Islam)
BBC wakahusika vilivyo katika kusambaza kaseti za Khomein kwa watu mbalimbali wa Iran hasa kwa viongozi wa kidini. Kwenye kaseti hizo Khomein alizungumzia kuhusu ubaya wa utawala wa Shah. BBC wakaenda mbali zaidi, wakauonesha ulimwengu ubaya na mateso yanayofanywa na kundi la kijasusi la Shah, kundi la SAVAK.
Asasi hii ya ujasusi hakuiunda Shah peke yake bali kwa msaada mkubwa wa nchi zilizomuwezesha kuingia madarakani, lakini kwa vile leo hatakiwi basi kila ubaya wake ambao mwanzo ulifanywa siri ulianikwa. Mchezo huu waliufanya tena kwenye miaka ya tisini na elfu mbili pale ajenda ilipomchoka Saddam Hussein.
Ilipofika Septemba na Octoba mwaka 1978 BBC ilianza kurusha matangazo yenye mawazo na fikra za kimapinduzi moja kwa moja Iran kwa lugha ya Kifursi, lugha ya Taifa la Iran, hivyo kila mtu aliweza kumsikia Khomein kupitia lugha yao ya asili kupitia BBC. Gazeti la Washington Post likatoka na kichwa cha habari kuwa ‘BBC ni adui namba moja wa nchi ya Iran’.
Haikuchukua muda wimbi la watu hasa vijana wanafunzi na wasomi wakachukuliwa na vuguvugu la kimapinduzi la Khomein ambao kupitia kwa propaganda za BBC waliona kuna haja ya kurudishwa kwa utawala wa kidini wa Kishia na hivyo Shah aondoke na Khomein aingie ili atekeleze maono hayo kwa faida ya nchi yao.
Lakini walikosea kitu kimoja, haikuwa kwa faida yao bali kwa faida ya Illuminati. Utawala wa Carter kutoka kwenye White House za Marekani, ukifuata muongozo wa Zbgniew Brzezinski mwanamikakati mkubwa wa Illuminati na kinara wa New World Order, ulishirikiana na utawala wa Uingereza kumtoa Shaha nchini, Iran na kumuingiza Khomein ndani ya Ikulu.
Kuanzia kipindi hicho mpaka Khomein alipofariki mwaka 1989, Iran ikawa ni kituo cha kimataifa cha kuendesha sera za chuki dhidi ya mataifa ya magharibi, kwa maneno mengine kituo cha kimataifa kwa kuendesha sera za ugaidi dhidi ya mataifa ya magharibi.
Mtu mwerevu atajiuliza ni vipi utawala wa Khomein uliosaidiwa kuingia madarakani na nchi za Magharibi leo uendeshe mapambano dhidi ya mataifa hayo ambayo ndiyo wafadhili wake wakubwa? Jibu ni kuwa utawala huo ulitakiwa uingie madarakani ili uweze kuendesha vita hivyo na hivyo kutengeneza mazingira ya kuwepo kwa makundi mbalimbali ya kigaidi ambayo yatategemea msaada wa moja kwa moja kutoka Tehran.
Na hapa tunakutana na Hizbullah, tunakutana na makundi mbalimbali ya kipalestina mbayo yanapokea misaada yao kutoka Tehran kupambana na adui wa Uislamu na muislamu, kupambana na mataifa ya magharibi, na hapa tunapata vita dhidi ya ugaidi na hii ndiyo picha kubwa ambayo wengi walishindwa kuiona.
Na wengi bado hawaioni, vita dhidi ya ugaidi si kwa faida ya Uislamu, na kama tulivyoona vita hivi havikuzaliwa ndani ya Uislamu na wala havihusiani chochote na Uislamu, bali ni kwa faida ya Illuminati, ambao kwao ni hatua muhimu kulifikia lile lengo la milenia nyingi, lengo la kuwa na Serikali moja na dini moja kwa dunia yote na walimwengu wote, lengo litakalofikiwa kupitia mapinduzi na vita vikubwa.
Mapinduzi na vita hivyo yamekwisha tokea katika zama tofautitofauti, na sasa imebaki hatua moja kubwa ya mwisho, nayo ni vita ya tatu ya dunia, ambayo itafikiwa kupitia vita dhidi ya Ugaidi.
Mwaka 1979 Bernad Lewis, alipewa fursa ya kuhudhuria kwenye mkutano uliofanyika mara moja kwa mwaka. Mkutano wa siri wa asasi ya Bilderberg, Lewis, alitoa maoni yake jinsi Mashariki ya Kati itakavyoendelea kutawalika na wakati huohuo kutumika kuipigisha ajenda ya New world order, hatua kwa hatua kupitia vita dhidi ya ugaidi.
Lewis aliwataka Illuminati kukitengeneza kile kitakachoitwa ‘Waislam wenye siasa kali’ ndani ya Mashariki ya kati, Waislam hao watasaidia migawanyiko mbalimbali yenye sura ya kisiasa, kidini, kiuchumi na kijamii.
Migawanyiko hii pia ipewe fursa ya kuanzisha vuguvugu la kimapinduzi, na kupigania uhuru wa wachache ambao wanaonekana kunyonywa au kutengwa na wengi, mfano wa-Kurdu, Armeniani, Druze, Azerbaijani Turk, Copto wa-Ehiopia, Sudan na makabila yao, Waarabu na makabila yao.
Mpango huu utafanikiwa kwa kutumia mbinu zote chafu na za siri za Illuminati kupitia kwa CIA ambao kwa mlango wa nyuma watafadhili na kutoa mwongozo kwa vikundi hivi.
Kupitia mpango huu Iran ilitoa ushirikiano na kutoa msaada wa kiukombozi kwa watu walioitwa wapigania Uhuru wa Palestine, Ireland ya Kaskazini, Sudan na Ivory Cost.(Angalia, Labeviere, Richard. Dollars for Terror. Uk. 215)
Illuminati ndiyo walioitengeneza na kuipa nguvu Urusi na hatimaye kuifanya kuwa ndiyo taifa lenye nguvu duniani kuliko yote (Super Power), mchakato huo ulifanyika baada ya vita ya kwanza ya Dunia na vita ya pili ya dunia, kati ya sababu mojawapo ya Urusi kufanywa Super Power ni ili kutengeneza taifa lenye nguvu na lisilo na dini (Ukomunisti). Hata hivyo U-Super power wa Urusi ulitakiwa kufa na kile kilichojulikana kama vita baridi (Cold war).
Ajenda ilikuwa inapiga hatua nyingine kubwa, hatua ambayo itaifikisha kwenye vita ya tatu ya dunia. Nchi iliyochaguliwa kuifikisha ajenda hiyo haikuwa Urusi bali Marekani, taifa teule la Illuminati, taifa ambalo maelfu ya miaka nyuma, hata kabla ya zama za Plato tayari lilishateuliwa kuifanikisha kazi hii muhimu na mahususi kwa Illuminati.
Hivyo vita baridi na harakati za kuliteka anga kwa njia ya kumfikisha binadamu mwezini kwa mara ya kwanza katika historia yake vyote vilikuwa ni maagizo ya kuangusha utawala wa kisovieti na kulikaribisha taifa teule la Marekani kwenye ulingo wa kuwa Super Power.
Hakuna binadamu aliyekwenda mwezini, si Urusi wala Marekani walioweza kumpeleka binadamu mwezini, huu ulikuwa na bado ni uongo mkubwa katika historia ya binadamu kupata kutolewa na mataifa makubwa duniani, na bado mpaka sasa tunaendelea kufundishwa kwa namna na njia mbalimbali kuwa binadamu alikwenda mwezini, lakini ukweli ni kuwa hakuna binadam aliyekanyaga mwezini, kifupi hakuna binadamu aliyepata kutoka nje ya Orbiti ya dunia.
Kwenye vitabu vya kidini mathalani Biblia na koran kuna hadithi kuhusu mitume waliopaa kwenda mbinguni, hii ni hadithi tofauti na tunayoizungumzia, sisi tunazungumzia binadamu kwenda mwezini katika zama zetu zinazoitwa za sayansi na teknolojia, katika zama zetu hizi ambazo teknolojia yetu inasemwa ipo juu.
Teknolojia hii ni duni mno kiasi cha kwamba haiwezi hata kumtoa binadamu nje ya orbiti ya dunia na kumrudisha akiwa hai, achilia mbali kumpeleka mwezini, haiwezi kufanya hivyo, ni duni mno, hivyo safari ya kwenda mwezini ilikuwa ni danganya toto.
Hivyo sakata la vita baridi na nguvu zake zilikuwa na lengo la kuliingiza taifa la Marekani kwenye ulingo wa Super Power na kumuondosha Urusi. Lakini Urusi haikuwa imesambaratika mpaka pale watu walioitwa mujaheedina kutoka Afghanistani, na kutoka katika kila kona ya dunia walipopambanishwa na Urusi.
Hii ndiyo iliyo kuwa picha kubwa ambayo CIA na mawakala wengine wa Illuminati waliifahamu. Kupitia sera chafu za kupigania uhuru kwa njia ya silaha, kupitia mafunzo yaliyo potoshwa ya dini ya Uislam waliweza kuwaandaa vijana hawa kutoka sehemu mbalimbali kwenye uso wa dunia na kuwaleta mahala pamoja kama wapigania jihadi.
Vijana hawa wa Mujaheedina watakapo maliza kazi yao ya kuiangusha USSR kama Super power, watapewa kazi nyingine na waajiri wao, kazi ambayo katika zama zetu tunaifahamu vyema kama Ugaidi.
Kazi hii mwongozo wake pamoja na maudhui yake havitoki kwenye mafunzo ya dini ya Uislamu bali kwenye mahekalu ya kimasoni na mawakala wa Illuminati.
Mwanastratejia wa Illuminati bwana Brzezinski ambaye kwa sasa anashikilia wadhifa muhimu kwenye serikali ya kibaraka mwingine wa Illuminati na Freemason wa daraja la 32 Barak Obama, alipokuwa akihojiwa mwaka 1998 kwenye mazungumzo aliyoyafanya na Le Nouvel Observateur alikiri kuwa CIA iliwasaidia mujaheedina kwenye mapambano dhidi ya USSR.
Alisema kuwa Julai 3, mwaka 1979 aliyekuwa Rais wa Marekani kipindi hicho Jimmy Carter alisaini na kupitisha mwongozo wa kwanza wa kuwasaidia Mujaheedina kwa siri.( Angalia, “Interview With Zbigniew Brzezinski”, Le Nouvel Observateur.<AOL.de | Kostenlose Email, Nachrichten & Wetter, Finanzen , Sport und Star-News auf AOL.de>😉
Ni katika kipindi hichi mwanastratejia huyu alianza kuziita nchi za Iran, India na Afighanistani kuwa ni muhimili wa maovu duniani, sera ambazo ziliendelea kutumiwa hata na Rais Bush na zilitumiwa na Obama pia.
Kuzipachika nchi hizo jina hilo sababu yake ni kutengeneza na kuwapa nafasi ya kutanuka kwa vikundi vinavyo julikana kama ‘Waislam wenye siasa kali’, hivyo nchi hizi zilijulikana na bado zinafahamika kwa mujibu wa sera za Marekani kuwa ni nchi zenye kusaidia ugaidi duniani.
Lakini hayo hayakumzua Carter kusaini mwongozo wa kuvisaidia vikundi hivyo ambapo kitendo hicho ni kinyume na katiba ya Marekani na ni kinyume na mwongozo wa Umoja wa mataifa.
Kwa nini basi Carter aliwasaidia, Carter aliwasaidia kwa vile vikundi hivi ni wao ndiyo wamevianzisha kupitia mtandao mpana unaozihusisha nchi kadhaa za bara la Ulaya na mashirika yao ya kijasusi na pia zikiwemo nchi za Kiarabu na malengo ya vikundi hivi si kuusaidia Uislamu kwa kupambana na nchi za Ulaya na washirika kama watu walivyoaminishwa.
Bali kuubomolea mbali Uislamu na wakati huohuo vikitekeleza matakwa mengine ya Illuminati kama lile la kuiangusha USSR ili Marekani inyanyuke kama Super Power, na kwa sasa vikundi hivi kama tunavyoona vinashirikishwa vilivyo kuhakikisha vinaukokota umma wa kiislamu kwenye uwanja wa Vita ya tatu ya dunia.
Mpango huu wa CIA kuwasaidia Mujaheedina huko Afghanistan ulikuja kufahamika kama Iran-Contra-Affair ambapo mbali na mambo mengine Marekani walihusika na kuwauzia Iran silaha kwa ajili ya kupambana na Iraq na pia ikawauzia Iraq nao silaha katika mpango ulioitwa Iraq-Gate, huu ni mchezo wa kawaida kwa Marekani na Illuminati kufadhili pande mbili za vita kwa wakati mmoja, kwani mwisho wa siku ni wao wanaofaidika na vita hivyo.
Hapa utaona Marekani inaziuzia silaha nchi ambazo yenyewe inazitambua kuwa ni nchi za kigaidi duniani. Mkutano wa asasi ya siri ya Bildeberg uliofanyika mwaka 1973 kwenye mkutano huo walijadili kuhusu kupandishwa kwa bei ya mafuta duniani na baadaye mwaka 1974 bei hiyo ikapanda kwa kasi sana, faida kubwa iliyopatikana katika ongezeko hilo la bei ya mafuta ilitumika kati ya mengi ni ufadhili shughuli ya Iran-Contra-Affair, na mipango mingine michafu ya kuunda vikundi vya kigaidi sehemu mbalimbali duniani.
Wakati haya yote yanafanyika mshirika mkubwa wa Marekani kwenye hili alikuwa na bado anaendelea kuwa ni Saudi Arabia chini ya uongozi wa Wahhabisim.
Wakati Marekani na washirika wake walipotaka kuing’oa USSR kupitia kwa Mujaheedina iliwabidi CIA kushughulika vilivyo katika kuwaandaa, kuwapa mafunzo, kuwalipa na hatimaye kuwasafirisha watu ambao waliitwa wapigania uhuru, au ukipenda mujaheedina na au kwa uwazi zaidi magaidi kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja Afghanstan kuuangusha utawala wa USSR. Mpango huu ulifanyika ukiwashirikisha Muslim Brotherhood. Watu walitolewa kutoka Ulaya,
Afrika ya kaskazini, Afrika Mashariki, Mashariki ya Kati, Asia na ndani ya Marekani kwenyewe. Mpango huu ulilenga kuwaandaa watu watakao tumika kama mawakala wa ugaidi kote duniani pale vitakapomalizika vita baina ya wapigania uhuru na Urusi kupinduliwa.
Hivyo vijana hawa waliojitolea kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa nia safi kabisa ya kupigana Holy war kwa kipindi hicho walifahamika kama wapigania uhuru, lakini baadaye walitumika kutengeneza mtandao uliofahamika kuwa ni wa kigaidi dhidi ya Marekani na marafiki zake, na hiyo ndiyo picha kubwa ambayo wengi hatukuiona kipindi hicho.
Msingi waliopatiwa vijana hawa kutoka sehemu mbalimbali duniani ulilingana na mafunzo ya karne ya kumi na nane yaliyotolewa na wakala wa Uingereza bwana Mohamed Abdul Wahhab. Uongozi wa Saudi Arabia nao haukuwa nyuma kwenye hili King Fahd naye akazimwaga dola kupitia kwenye benki ya BCCI kuwasaidia Mujaheedina.
Shirika la kijasusi la Pakistan lilihitaji mwanamfalme wa Saud Arabia kuviongoza vita hivyo vya jihad dhidi ya Urusi. Hata hivyo hakuna aliyejitolea kutoka kwenye familia hiyo hivyo viongozi wa Saud wakampendekeza kijana kutoka kwenye familia tajiri na ambayo ipo karibu na familia ya kitawala ya Saud, naye hakuwa mwingine bali ni Osama Bin Laden.
Hadithi ya Osama ni moja ya hadithi zilizofanywa na za kusisimua kwelikweli na vyombo vya magharibi
Osama alishakufa tangu mwaka 2001, lakini kwa takribani miaka 10, CIA wamekuwa wakirusha kaseti ‘mpya’ za audio na video za Osama Bin Laden, na kila CIA ‘walipozindua’ kaseti hizo zilipata mauzo ya kutosha kwenye vyombo vya habari vya magharibi na muuzaji wa ‘jumla’ wa kaseti hizo walikuwa ni Al-jazeera. Kwa muda wote huo hakuna kiongozi wowote wa Talibani au wa Al-Qaeedah aliyejitokeza hadharani na kusema kaseti hizo ni uzushi na uongo
Obama alipokuja kutangaza kifo cha ‘kutengeneza’ cha Osama bin Laden, ikiwemo kuandika kitabu kuhusiana na namna Osama alivyouliwa na kikosi maalum, filamu na taarifa mbalimbali.
Al-Qaeedah wakaibuka huko walipotoka na kusema watalipiza kifo hicho cha kiongozi wao, walisema mbona mtu huyu alishakufa kifo cha kawaida tangu mwaka 2001, ni kifo kipi mnachokwenda kulipiza?
Al-Qaedah, makundi ya waasi, Al-shabab, Boko Haram na makundi mengine yanayoitwa ya kigaidi, lao, na Washington, lao na Ulimwengu wa kimataifa wa kimasonia, lao na Illuminati ni moja! Binadamu ndiye adui, wanapigana vita, na ni vita dhidi yake na familia yake.
Mpango wa Brzezinski kupitia kwa Obama ulikuwa ni kutengeneza mitandao ya kisiasa ambayo itaweza kuiporomosha Urusi, utakumbuka mpango wake huu ulianza tangu wakati wa Jimmy Carter ambapo yeye alikuwa ni msimamizi wa siasa za mambo ya nje za Marekani ambapo akapelekea kuundwa kwa Taliban ambao waliifanya kazi hii vizuri sana nyuma ya kile kilichoitwa ‘Holy War’, lakini safari hii mpango huu hautailenga Urusi peke yake bali pia China nayo itaingizwa ndani ya nyumba.
Brzezinki amekuwa makini akisambaza propaganda zinazolenga kuchora mstari wa kutokuelewana baina ya Umoja wa Ulaya na Urusi kupitia Kosovo ambayo mustakabali wake wa kisiasa unaonekana kuachwa katika hali ya utata kwa makusudi ili Moscow iweze kunyooshewa vidole kwa aina yoyote ya uozo unaotokea hapo. Sasa hivi Cremea hali ya mambo inavyokwenda sio nzuri.
Obama alitakiwa kuwatoa wachina nje ya Afrika kwa namna yeyote inayo wezekana. Hata hivyo Brzezinki ana picha kubwa zaidi juu ya hili la kuwafukuza wachina nje ya Afrika. Kupitia kwa Obama, maarufu kama, Kennedy Mweusi kama alivyokuwa akiitwa wakati wa uchaguzi wa Marekani.
Brzezinki anao mpango wa kuwapora Wachina kila aina ya rasilimali wanayonunua kutoka Afrika, ikiwemo mafuta, gesi za asili, madini na kila kile ambacho kimebakia kama makombo baada ya vile walivyopora wakati wa ukoloni, baada ya ukoloni na kwenye ukoloni mambo leo.
Mpango uliochaguliwa juu ya hili ni njia ile ile iliyopendekezwa na mababu wa Freemasons, Priory of Zion kwenye kile walichokiita Protocal of Zion, njia hiyo ni kuzivunjavunja nchi za kiafrika kupitia vita vya wenyewe kwa wenyewe kitu kitakachowakimbiza wachina nje ya Afrika.
Na hili litasimamiwa vilivyo na kile kinachoitwa Africom ambayo imeundwa na Marekani na mawakala wao wengine.
Kupitia mpango wa Brzezinki Afrika itakuwa ni uwanja wa mapambano baina ya Marekani na China, mapambano ya kiuchumi na siasa, lakini mapambano ya bunduki itakuwa ni baina ya waafrika sisi kwa sisi.
Afrika itawaka moto, mauaji ya watu chini ya jangwa la Sahara yatakuwa ya kutisha. CIA wataingilia kati na hata kuingilia siasa za nchi za ndani za Afrika kwa uwazi kabisa nyuma ya kile kitakachoitwa vita vya ugaidi ambavyo wakala wake ni Al-Qaeda ambao kwa sasa kutokana na taarifa za vyombo vya habari za kimagharibi na hata vya hapa Afrika Al-Qaeda tayari wako ndani ya Afrika, Algeria na Tunisia na kazi zao chafu zimeshaanza kuonekana, kumbuka Algeria ni mojawapo ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi Afrika.
Al-Qaeda ilikuwa ikidhaminiwa na CIA kupitia fedha za dawa za kulevya, wakati Taliban wakidhaminiwa na Brzezinki na mtandao wake wa Trilateral Commission. Hakuna vita vitakatifu wala Jihadi kama alivyo Kennedy mweusi.
Moto umeshawaka Nigeria moja ya wazalishaji wakubwa wa Mafuta Afrika, Boko Haram wananguruma na wanaokufa ni waafrika.
Afrika, yametokea, moto umewaka, serikali zimepinduliwa, Wachina wamekimbia, Illuminati wanabeba chao na Waafrika bado tunapigana risasi kwa faida yao.
Uingereza na Israeli kwa pamoja kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiivunjavunja Sudan, lakini leo picha iliyoko Darfur inatumiwa na Marekani pamoja na Uingereza kama kisingizio cha kuitawalia nchi hiyo mambo yake nyuma ya kile wanachotuambia kuwa kuna uvunjwaji mkubwa wa haki za kibinadamu katika eneo hilo.
Kwamba Sudan inakiuka haki za binadamu, hakuhusiani kabisa na mpango wa kuondoa zahama hilo kama vyombo vya habari vya kimagharibi na mawakala wao wanavyodai, lakini zaidi inahusiana na mpango wa kukata 7% ya mafuta ya China ambayo yanatoka Sudan.
Habari zinasambazwa kwa kasi kuwa shughuli za kiuchumi za China nchini Sudan zinazorotesha kwa kiasi kikubwa utaratibu wa kuondoa baa la njaa na tatizo la mafuta duniani.
Aina hii ya propaganda muda si mrefu inapokelewa na vikundi vinavyojiita vinasimamia haki za binadam ambavyo ni vikundi vya watu walewale katika sura tofauti lakini nyuma ya ajenda ileile.
Nchi yoyote duniani ambayo kwa namna moja ama nyingine inanufaika kiuchumi na au kiviwanda kutokana na ushirika wake na China na kwa maneno mengine China nayo inajijengea misuli yake ya kiuchumi na viwanda kutokana na miradi yake mbalimbali iliyomo nchini humo, nchi hiyo haiwezi kuepuka mpango huo wa Brzezinki. Mfano ni Burma na Venezuela ambazo historia ya maendeleo yao kiuchumi haijakamilika bila kuitaja China.
Shughuli inayoendelea Pakistan ambapo Kennedy mweusi alikiri yuko tayari kuipiga bomu la nyuklia Pakistan endapo itaonekana kushindwa kupambana na Taliban na Al-Qaeda.
Shughuli hiyo haina lolote kwenye kile kinachosemwa vita dhidi ya ugaidi bali zaidi, ni vita vya kuizorotesha nchi hiyo ambaye muda mrefu imekuwa mshirika wa China, vurugu hizo ni za kuwakimbiza wachina kutoka humo. Tunaona siasa za vuta ni kuvute baina ya Pakistan na Marekani sasa.
China itakapotengwa na kupokonywa washiriki wake wote wa kiuchumi, na kunyimwa uwezekano wowote wa kupata mafuta na malighafi zozote kutoka nje ya China, hatua itakayo fuata ni kuizorotesha serikali ya China na wakati huohuo kuipambanisha na Urusi, suala la kuizorotesha serikali hiyo tumeliona linavyoshika kasi kupitia Tibet kwa kiongozi wao wa kiroho Dalai Lama.
Lakini kwa vile Urusi na China zote zinafahamu kuhusu njama hizi za Brzezinki mchezo unakuwa mgumu ,na hasa pale utakapojenga mazingira ya kuunganisha mahusiano yenye chuki ya Urusi na China dhidi ya Marekani na washirika wake wapya.
Upande mwingine wa shilingi mwanasesere huyu atakuwa na kazi ya kuiunganisha Iran na Syria na kwa pamoja zisimame kuwapinga wachina na warusi.
Kilichotakiwa ni Bashir Al Assad atoke pale na pawekwe kibaraka mwingine, ambaye moja kwa moja atakuwa ni adui wa Urusi na China, kama tunavyo ona, aliyempa kiburi Assad ni Mchina na Urusi, sasa hali hiyo inabidi ibadilike, halikadhalika kwa Iran, atafuatia baada ya Syria.
Mwandishi wa kitabu cha (Barack H. Obama🙂 anajaribu kutupa taswira kuhusu Iran na Marekani kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa dhidi ya Urusi na China namna utakavyo kwenda, haya ndiyo maoni yake.
Amasema, "Iran itashawishiwa iwe rafiki na Marekani kwa ahadi ya kupewa nguvu sawa na Marekani ndani ya Mashariki ya kati, si mchina wala mrusi, si mpakistan wala Mmisri atakayekuwa na sauti ila Iran mshirika wake mpya Marekani."
Rasilimali za Iran zinazozuiliwa na Marekani kwa muda wote huo, sasa zinafikia thamani ya dola bilioni mia na zaidi, Iran anaweza kupewa ahadi hii ya kupata rasilimali zake hizo.
Iran alipewa ahadi ya kutolewa kwenye orodha ya nchi zinazodhamini ugaidi na vikundi vyake (hatua hii imeshaanza kufanyiwa kazi). Bila kuwasahau washirika wakubwa wa Iran Hezbollah kuwa na wao watapata chochote.
Bush Baba alimkabidhi Saddam silaha nyuma ya mapazia halafu Bush mwana akaja kuzidai mbele ya hadhara, Iran anaweza kupewa ruhusa ya kuendeleza mradi wake huo nyuma ya mapazia (Hili nalo limeshapatiwa baraka na Washington).
Wanaweza kuwapatia teknolojia bora kushinda hii waliyonayo, silaha bora na mabomu ambayo wanaweza kuyarusha kokote pale duniani na yakafika Moscow, Iran aliulizwa, "sema tu kama ndiyo hilo unalotaka, sasa hivi tutakupatia."
"Ujue tu kwamba adui yako mbaya kuliko wote hajawahi kuwa Marekani bali Urusi. Si unakumbuka namna walivyo kufanya walipochukua baadhi ya maeneo yako wakati wa vita ya pili ya dunia?
Ule ulikuwa ni uharibifu mkubwa. Sisi hatujawahi kufanya kitu kama hicho na wala hututajaribu kufanya hivyo. Tunachotaka sisi ni kuwa marafiki na kukusaidia kuwa na nguvu za kutosha kupambana na adui yako wa kweli, Moscow
"Kama unavyofahamu mheshimiwa Rais wananchi wako wanaichukia Urusi kuliko wanavyoichukia Marekani na Uingereza na wakati wowote utakapowachukia warusi ujue unawaridhisha watu wako na sisi tutakusaidia."
"Sema tu unataka nini? unaonaje kuhusu manuwari, tukakupatia manuwari inayokwenda mpaka bandari za kusini ya Urusi zikiwa na mizinga ya kinyuklia ,hapo utawazuia Urusi wasiendelee kukuibia mafuta yako kutoka kwenye bahari ya Caspian, na kama wakijaribu kujibu mapigo usiwe na hofu tutakuwepo kukupa sapoti.
Fikiri mwenyewe kuhusu hili. Halafu kuna hawa wachina, kwa nini unapenda kufanya nao biashara sana?, muda si mrefu watakuweka kwenye mfuko wao wa suruali yao kutokana na jinsi unavyowauzia mafuta, halafu tunajua hulipendi hilo, bora ufanye biashara na sisi hata kama ni kwa dola. Tunachotaka ni kuwa ufahamu kwamba sisi ni wa kweli vibaya mno.
Mwandishi huyu hayuko mbali sana na ukweli kwasababu ni mchezo huu huu aliufanya Brzezinki kwa waafghanistan kupitia Mujaheedina ambao ni zao la mpango wake, akawapambanisha na Urusi na kilichobakia hapo ni historia, alifanya hivyo kupitia kwa Jimmy Carter, leo mchezo uleule wa mtu yule, yule ulifanyika kupitia kwa Obama.
Halafu wasyria nao watafuatwa, (tayari Syria kulishawaka moto) watashikwa kama walivyoshikwa kwenye vita ya ghiba ya mwaka 1991. Lengo si kuwapambanisha wairan na wasyria bali kuwaunganisha dhidi ya China na Urusi. Usisahau Khomeini kufanya mapinduzi yale ulikuwa ni mpango wa Freemasons nyuma ya asasi zake za siri.
Kinachoendelea Afrika na duniani leo ni kazi mahsusi ya kuandaa pande za mahasimu kwa ajili ya vita ya tatu ya dunia, Pakistani tunajua anazo nyuklia, Iran nyuma ya mapazia kama ilivyo kuwa kwa Iraq ameshawashiwa taa ya kijani kuendelea na mradi wake.
Zinazojiita nchi za kiislamu, na zile ambazo tunaona zinapinduliwa na waasi kama Egypti, Libya, Syria, Iraq, Pakistani, Iran na wengine watakaopitiwa na upepo huu, wanaandaliwa kuunda upande mmoja au muungano mmoja dhidi ya maadui wa Uislamu na Waislam.
Utasikia vikundi hivi vikija na dai la Khilafa kote duniani, hivyo hawataishia, Syria au Libya au Somalia, wataingia kila pale watakaporuhusiwa na mabwana zao wakubwa kuingia, kumbuka upande mmoja wa vita unaandaliwa, dhidi ya Ulaya, Marekani, Israeli na washirika wao.
Kipindi hichi siyo Marekani wala Uingereza atakayeanzisha vita hivyo, chokochoko baina ya Israel na Iran ndiyo cheche zitakazowasha moto huo ambapo baadaye kila mmoja ataita washirika wake, Israel washirika wake wapo tayari na tunawafahamu, lakini washirika wa Iran ndiyo kwanza wanaanza kupanga safu, kitakacho fuata ni vita ya tatu ya dunia.
Malengo ya makuu ya vita hivyo ni kuisimamisha Israel kama ‘New Super Power’, hii ni muhimu kwa vile ni kutokea hapo Jerusalem ndipo Dajjal anatakiwa atawale, na tunajua Illuminanti kwa zaidi ya miaka 2000 wamekuwa wakiandaa zulia ambalo Dajjal atatembea juu yake.
Na mahali ambapo dola ya Dajjal itakapoanzia ni Israel, na kama yeye atataka kuwa kiongozi wa dunia na hatimaye kujiita mungu, hili haliwezekani kama atasimama nyuma ya dola dhaifu, lazima asimame nyuma ya dola yenye nguvu na iliyoundwa na kuandaliwa kwa muda mrefu kwa ajili hiyo, dola hiyo si nyingine ila ni Israel, na hapo ndipo patakapokuwa makao makuu ya serikali ya dunia ya New World Order.
Hivyo basi Issa (Yesu) atakapo kuja kazi ya kwanza ni kumuondoa Dajjal ndani ya Israel, hichi ndicho kipindi ambacho miji mitakatifu itaachwa na waumini wa kweli kwa ajili ya kwenda kuungana na jeshi la Issa (Yesu Kristu) dhidi ya Dajjal.
Mpinga Kristo huyu atauwawa sehemu inayoitwa Baablud, leo hii panaitwa TelAviv, na hapo itakuwa ndiyo mwisho wa kitimbi hichi cha Babylon Brotherhood kilichofanyiwa kazi kwa zaidi ya miaka 2000 na vizazi kadha wa kadha vya Illuminati.
Kazi ambayo imekuwa ndiyo mzizi na chemchem ya kila dhila, mateso, shida, chuki matatizo na kila baya unaloliona leo kwenye uso wa dunia. Kazi hiyo mbaya iliyofanywa kwa milenia nyingi itakwisha pale Baablud. Freemason, Illuminanti, Babilon Brotherhood, asasi zao nyingine nyingi za siri na kazi yao ya milenia nyingi itazikwa hapo.
Mwisho