Familia yakamatwa kwa kuozesha watoto wa miaka 12 na 16

Shida kubwa ni ubabe watu hawataki kuelekezwa na kukubali kutii.
Shida kweli maana hii inaathiri pia hata viongozi wao kama Wasira anayelilia ubunge toka kwa Bulaya kila uchwao. Mara amtishie kumwachisha na jamaa yake mara akimuona anamvunja miguu na kumwagia tindikali ili tu mtoto wa watu aachie ubunge.
 
Shida kweli maana hii inaathiri pia hata viongozi wao kama Wasira anayelilia ubunge toka kwa Bulaya kila uchwao. Mara amtishie kumwachisha na jamaa yake mara akimuona anamvunja miguu na kumwagia tindikali ili tu mtoto wa watu aachie ubunge.
Ni kweli unaweza kuona hapo tu ni mfano mmoja,watu wana viburi hatari,Pro.mmoja wa kutoka huko alikuwa anatukana, anabeza anavyojisikia kisa amesoma.

Miradi mingi inakwama si kwasababu hakuna watendaji bali ni ushirikiano hafifu kutoka kwa jamii.

Kuna sehemu nimeona wamechimbiwa kisima cha maji masafi wakajenga miundombinu mizuri, utaratibu ukawekwa kwamba walipie ndoo shs 50 ili wapate pesa ya kununulia luku.

Cha ajabu baadhi ya akina mama wakakataa eti hawajazoea kuchota maji kwa kulipia bora waende wachote maji ya madimbwi tena wanayasafiria mbali.

Serikali na asasi za kiraia zijikite kutoa elimu jamii ili kuwakomboa hawa. Vitendo vya ukeketaji navyo vimeshamiri katika jamii zinazokeketa kama siyo wanaongoza hapa Tanzania basi ni miongoni mwa mikoa iliyo na idadi kubwa ya wanawake wanaokeketwa.

Muraaa acheni ubabe kwenye vitu vya kuleta maendeleo, nyinyi ni wachapakazi wazuri , mkoa wenu mzuri sana mtaufanya watu wasiwe wanakuja kwenu kwa kuogopa kupewa vitasa na sime.
 
Hawa ndio wale kina Vita ni Vita Muraaaa.Jaman kuna mura mmoja hapa mjin nishaingia mkenge nina mimba yake basi km mambo yenyewe ndio haya nijipange tu.
Siyo wote wako hivyo japo wengi wanaamini mwanamke ni kiumbe dhaifu. Omba usimkute ni mwenye hasira.

Ngoja nikupe kisa kimoja. Kuna rafiki yangu mmoja ni muraa tulikuwa tunafanya kazi ofisi moja tumejiajiri, sasa bwana hilo jengo tulipoweka ofisi kuna baadhi ya vitu tunavitumia ni vya mwenye jengo.

Huku tukiwa tunajipanga kwamba siku tukikaa sawa tutanunua vya kwetu tusimtegemee kwa kutumia vitu vyake.

Siku ya siku hatuna hili wala lile mwenye jengo si akaliuza hata hatujui. Tunashtukia tunaambiwa vitu vyote ni mali ya mmliki mpya na kodi mtakuwa mnamlipa yeye.

Tukapigwa na butwaa tusijue cha kufanya. Tukakaa na kuwaza tunafanyaje? Kodi siyo shida na vifaa je?

Unajua aliniambiaje huyu rafiki yangu. Alisema hivi 7seven mambo mengi hayawezekani pasipo kutumia ubabe!

Akaendelea kusema tutazuia hivi vitu visiondoke mpaka tutakapokamilisha mipango yetu. Nikamwambia sawa muraa.

Ndivyo ilivyotokea tukagoma kwamba mmetushtukiza hatujajipanga, tupeni muda tutawapa vifaa vyenu. Kweli baada ya muda tulikaa sawa. Kwahiyo kuanzia siku hiyo huwa tunasema tutumie ubabe, tutumie ubabe.
Ubabe mwingine una faida. Siku zote nilimuona akiishi vizuri sana na mke wake hajawahi hata kumtukana. Siyo wote wako hata huyo wako naweza kuwa huyu brother wangu from another mother.
 
Sherehe gani ilkkosa hata mpigapicha wa simu, isijekuwa wamebambikiwa kesi hao
 
Esther Bulaya ana kazi ya kuwafunda wananchi wake.
 
Waende Bariadi vijijini hali ni mbaya kuliko uko Mara na sherehe wanafanya kama kawaida unaweza ukafikiri upo nje ya Tanzania
 
warudi kwenye sheria ya ndoa,halafu waje ktk sheria inayomlinda mwanafunzi.Itafahamika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…