Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 6,559
- 12,518
Familia ya mateka wa Israel Evyatar David anayeshikiliwa na Hamas huko Gaza imelishutumu kundi hilo kwa kumuua njaa kimakusudi kama sehemu ya kampeni ya propaganda.
Taarifa ya familia hiyo iliyoitoa siku ya jana Jumamosi Agosti 2, 2025 imejiri siku moja baada ya Hamas kutoa video ikimuonyesha Bw David aliyedhoofika kwenye handaki nyembamba ya zege. Bwana David, 24, amekuwa kifungoni tangu alipokamatwa na Hamas kwenye tamasha la muziki kusini mwa Israel mnamo tarehe 7 Oktoba 2023.
"Tunalazimika kushuhudia mtoto wetu mpendwa na kaka, Evyatar David, kwa makusudi na kwa kejeli akifa njaa katika vichuguu vya Hamas huko Gaza - mifupa hai, iliyozikwa hai," taarifa ya familia ilisema na kuitaka serikali ya Israeli na jumuiya ya ulimwengu kufanya kila linalowezekana kumwokoa Evyatar.
Katika video hiyo iliyotolewa na Hamas, Bw David anasikika akisema "Sijala kwa siku nyingi... nilipata tu maji ya kunywa" na anaonekana akichimba anachosema kuwa litakuwa kaburi lake mwenyewe.
Wakati Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ikisema kuwa, Netanyahu alizungumza na familia za Bw David na mateka mwingine, Rom Braslavski, hapo jana Jumamosi, Mjumbe wa Marekani Steve Witkoff ambaye amezuru nchini humo, alikutana na familia za baadhi ya mateka.
Wakati wa shambulio lake dhidi ya Israeli karibu miaka miwili iliyopita, Hamas ilikamata mateka 251. Bw David ni mmoja wa mateka 49 ambao Israel inasema bado wanazuiliwa huko Gaza. Hii ni pamoja na mateka 27 ambao wanaaminika kuwa wamekufa. #EastAfricaTV