Familia yangu Mke na Mtoto wangu Mkubwa wamepata tatizo la Akili naomba ushauri wakuu

Familia yangu Mke na Mtoto wangu Mkubwa wamepata tatizo la Akili naomba ushauri wakuu

Mungu hayupo na hajawahi kuwepo , hakuna Mungu unayemfahamu wewe au mimi kama yupo mthibitishe uwepo wake hapa .
Thibitisha kwanza wewe kuwa hayupo sio kuropoka maneno "Hayupo". Njoo na ushahidi
 
Mganga na mchawi wakapambane. Uwanja ni upi? Familia itaendelea kuumia
Kama Mwamposa Ataendelea Kuwa Pale Kawe Na Kushindwa Kwenda Mahospitalini Kuponya Wagonjwa Nitakuwa Mtu Wa Mwisho Kuamini Drama .Mleta Mada Utoto Unakusumbua Au Ushamba Pia Inaweza Kuwa Sababu Katoro Yote Bukoba Yote Hakuna Waganga? Kwa Akili Ya Kawaida Tu Inaonyesha Kuna Uchawi Umetembelea Nyumba Yako Huko Milembe Wataambulia Kupewa Dawa Za Kuwazubaisha Ila Sio Za Kumaliza Hilo Tatizo.
Ninachokushauri Kuna Mdau Hapa Jf Alileta Uzi Wake Una kichwa Cha Habari Kinachosema "CHANGAMOTO YA KUTEMBEA"Kama Kuna Mdau Anaweza kuupandisha Ule Uzi Afanye Hivyo.
Ukishausoma Mfuate Pm Mwenye Uzi Muulize Akupeleke Kwa Mganga Wake Aliyemtibia Ninatumai Utasaidika Acha Mambo Ya Hospitali Huu Ni Ushauri Wa Mwafrika Kwenda Mwafrika Ukibisha Shauri Yako .
 
Tulia kwenye kile unacho kijua ila ukishindwa kuthibitisha unavunga tu
Sikia Wewe Hiyo Akili Sijawahi Kuiona Wala Kuihisi Ila Kila Siku Natamba Kwamba Nina Akili Wakati Wala Sijui Iko Wapi.
 
Pole sana mkuu.

Hebu nunua mafuta ya mzeituni umpake mwili wote na umnyweshe kijiko Cha chakula kimoja.

Baada ya hapo, Ukiona ametulia, Yani amepata afueni, basi jua huo ni ugonjwa wa kulogwa...

Unaweza fanya Kwa Binti Yako pia.

NB:
Mafuta ya mzeituni sio sumu kwani hutumika kupikia chakula Kwa watu walio na uchumi mzuri sababu yana gharama kubwa.
 
Kila mtu ana haki ya kuamini anachokitaka ili mradi asivunje sheria, umeamini uwepo wa Mungu humu na sio jukwaa la dini ninayo haki ya kuhoji uwepo wake bila kuvunja sheria za humu, na nina hoji hivyo ili nijue ni hakiki .
Ukisema una haki ya kuhoji una maanisha nini? Yani mtu kutumia uhuru wake wa kuamua kuamini Mungu wewe unapewa na nani haki ya kumhoji huyo mtu ambaye ameamua kuamini anachoamini? Kwa nini huyo mtu ahojiwe kwa kuamua kuamini Mungu? Kuonyesha unaamini Mungu kwenye hili jukwaa ni kosa? Au kuna sheria yenye kutaka kuhojiwa endapo utatangaza kuamini Mungu katika jukwaa hili?

Mimi nashangaa watu ambao mnajitambulisha kuwa hamuamini uwepo wa Mungu yani hamna imani kwenye madai ya uwepo wa Mungu na sababu ni kwamba hakuna uthibitisho, ila kutwa mpo humu kubishana habari za kuhusu Mungu.

Kama kweli kukosekana uthibitisho ndio sababu ya nyinyi kutokubali uwepo wa Mungu na kwamba hitaji lenu ni uthibitisho basi muusubirie huo uthibitisho hadi siku utakapopatikana maana mnajua kuwa hadi sasa haujapatikana, ila kutwa mpo kwenye kubishana habari za Mungu kana kwamba hamna uhakika na mnachokisimamia.
 
Jina La Yesu Lipo Ila Kila Siku Watu Wanataabika Na Magonjwa,Njaa,Vita Na Makolokolo Kibao Mungu Alipokuumba Alikuwekea Akili Ikawe Msaada Kwenye Maisha Yako Acha Kuigeuza Akili Yako Kama Sofa La Pale Sebuleni .
Kama Kweli Jina La Yesu Linatenda Mbona Wachungaji Hawanunulii Magari Kwa jina La Yesu Makanisa Kila Siku Yanajengwa Kwa Pesa Za Michango Yenu Mbona Hamumwambii Ajenge Kwa Jina La Yesu? Acha Uzezeta Amka.
Kuffar
 
Wakuu sijafanikiwa bado Ila ambaye yupo tayari tuzungumze kuhusu kiwanja namkaribisha

Mawasiliano yangu 0624 117 794

Ningependa nianzie Milembe hospital Kwa Matibabu huku nikiendelea na Maombi kama mlivyonipatia ushauri.
Umejaribu kushirikisha upande wa kwao kama kuna changamoto zozote za namna hiyo zilishawahi kutokea kwenye ukoo wao?
 
Mkuu Kuna Komenti Yangu Humu Nimemwambia Mleta Mada Atafute Uzi Wako Wa Changamoto Ya kutembea Nimemshauri Ausome Alafu Akutafute Pm Nami Nimehisi Unaweza Kumsaidia.
Kama Yuko Siriasi Naomba Msaidie.
Hakika mkuu changamoto ya humu ndani ni unawez jikuta una msaidia adui pasipo kujua
 
Habari wanaJF .

Kiufupi Mimi Baba wa watoto watatu ambao wote ni wa kike.

Naishi nao pamoja na Mama yao .

Tumefanikiwa kuishi miaka 12 mpaka sasa katika ndoa yetu.

Changamoto kubwa ambayo ninaipitia ni hii hapa.

Mimi kazi yangu kubwa ambayo huwa nafanya ni kuuza mazao , kuku wa kienyeji huwa naenda kijijini naangalia bei ndogo ya bidhaa Kama mahindi au kuku nanunua na kuja kuuza mjini.

Kiufupi Mimi ni mjasiriamali wa kiwango cha chini ambaye bado napambana.

Jambo Ambalo limenifanya nije ni changamoto iliyompata mke wangu na watoto.

Familia yangu ilikuwa vizuri Ila ilianza kuingia changamoto ambazo zimeniumiza Sana Akili na kunipa mawazo.


Mwezi wa kumi Mke wangu alianza kuumwa kawaida kabisa nikampeleka hosptali kumpima ikaonekana hana tatizo .

Ila nikikaa nae usiku halali anaongea mambo Kama ya kuchizika Anapasua vitu ndani .

Sasa nikaona hii hali itakuwa mbaya nimempeleka hosptali zote za mkoa Government na private Ila tatizo lipo pale pale .

Napoandika hapa mke wangu amefungiwa ndani , sasa hii hali Kama ya Mke wangu imeanza kumungia mtoto wangu wa kwanza Ana umri wa miaka 10 anaongea peke yake anaharibu vitu ndani .

Akikaa kidogo na wadogo zake wanapigwa kipigo kikali Sana hivyo mtoto na mama yao ambaye ni mke wangu ni Kama wanaumwa ugonjwa unaofanana.

Nimefatilia Sana katika familia zetu kujua Kama kuna mtu amewahi kupitia hali Kama hii sijafanikiwa kupata majibu.

Baada ya yote haya nimeamua nisafiri nimpeleke hosptali inaitwa milembe ipo Dodoma nimpeleke Mama na mtoto wawafanyie uchunguzi.

Wakuu naumia Sana Kazi haziendi mtaji umekata .

Ikiwa kuna wadau wanaweza nisaidia 400K nikapata nauli na kumsafirisha huyu Mama na binti yetu nitashukuru , Endapo nikifika Dodoma gharama zikahitajika zaidi nafikiria pia kuuza kiwanja ambacho nilikinunua Kwa ajili ya ujenzi.

Mrejesho

Wakuu nashukuru Kwa ushauri wenu mpaka sasa niseme nitaufanyia Kazi kadri nitakavyojaliwa.


Pia nimeona nianze na hii hatua ya maandalizi ya kumpeleka mgonjwa Dodoma yeye na Binti yetu pale Milembe , nitafanya huduma za hosptalini Ila pia sitoacha kumuombea kila siku.

Ikiwa unataka kuwasiliana na Mimi au Kwa chochote Ni-PM.

Pia nina kiwanja Heka moja ni kiwanja kipo katika muundo wa shamba ninakiuza ili pia kinisaidie katika hiki kipindi .

Gharama ya kiwanja ni maelewano kipo Katoro Bukoba Vijijini (Kagera)

Mungu awabariki nyote.🙏🏽

Mrejesho:
- Mrejesho changamoto ya Mke wangu ambaye alionekana kuwa na shida ya ugonjwa wa akili yeye na binti yetu mkubwa

Nguvu za Giza hizo, nenda kanisani ukaombewe kwa jina la YESU watapona...
 
Back
Top Bottom