DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 32,386
- 83,431
Dada wa aliyekuwa Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juma Hassan Kasailo ametaja sababu ya kifo chake.
Hassan alifariki ghafla siku ya Ijumaa, ambapo kifo chake kilithibitiswa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta.
Kabla ya kuthibitishwa, taarifa za kifo cha hakimu huyo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiambatana na taarifa ya mtu aliyetajwa kwa jina la Mng’oa kucha ikitishia maisha ya hakimu huyo.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni akizungumzia kifo hicho na vitisho hivyo vya mtandaoni alisema hana taarifa za kifo cha hakimu huyo na hakuwahi kuripoti kuhusu kutishiwa maisha.
Akizungumza jana baada ya mazishi ya kaka yake kijijini kwao Kwamsisi wilayani hapa, dada wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Rehema Kileo alisema kwamba ndugu yao alipoteza maisha baada ya kuugua ugonjwa wa shinikizo la damu..
Dada huyo alisema familia yao haina taarifa zozote kuhusu utata wa kifo cha ndugu yao kuwa alipata vitisho, lakini wanachojua wao alifariki kwa ugonjwa.
“Chanzo cha kifo cha kaka ni ugonjwa wa presha, ilishuka sana hadi kusababisha kifo chake na si vinginevyo labda kama kuna hilo mlilosikia nyie,” alisisitiza Rehema akipinga uvumi wowote kuhusishwa na kifo cha kaka yake.
Awali, ujumbe uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii ulionyesha kuandikwa Februari 17 ukiwa na kichwa cha habari, “Tuondoleeni mtu huyu hakimu Ilala kabla hatujachukua sheria mkononi.”
Ujumbe huo ulimtaja hakimu huyo kwa majina yake na kumtuhumu kutoa hukumu kandamizi na kwamba huu ndio mwezi wake wa mwisho.
“Tumeripoti sehemu mbalimbali tumechoka sasa huu ndio mwezi wake wa mwisho, yeyote anayemjua salam hizi zimfikie...” inasomeka sehemu ya ujumbe huo.
Hata hivyo, uvumi huo unapingwa na familia ikieleza kuwa ndugu yao alikuwa na shinikizo la damu na ndilo lililochukua uhai wake.
Chanzo: Mwananchi