Familia za VIP's Tanzania tafadhali muwe mnawahi ' Kukanusha ' taarifa za Kuzushiwa 'Vifo' Ndugu zenu kuliko Kuzinyamazia tu

Familia za VIP's Tanzania tafadhali muwe mnawahi ' Kukanusha ' taarifa za Kuzushiwa 'Vifo' Ndugu zenu kuliko Kuzinyamazia tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kuendelea tu Kunyamaza Kwenu kama sehemu ya ( za ) Familia ni kutoa mwanya kwa Wazushi na Wambea ' Kutudanganya ' Watanzania na kuanza kuishi kwa Taharuki ( Wasiwasi ) kitu ambacho nakiona kama vile hakina Ustawi Kwetu.

Ila GENTAMYCINE huwa nikisia Taarifa za chini chini ( za Uzushi ) kuwa Mkubwa ( VIP ) fulani amefariki dunia huwa naogopa kwani taarifa hizi katika Kuzifuatilia Kwangu kwa 85% huwa zina usahihi.

Ewe Mwenyezi Mungu nakuonba tuepushe na Misiba ya Wapendwa ( VIP's ) wetu nchini Tanzania kwani bado tunawahitaji sana ukiwachukua utatunonesha tena Vidonda vya Vilio ambavyo vitaiingiza Serikali Gharama kubwa na hatimaye mwakani kushindwa Kupandisha ' Mishahara ' kwa Watumishi ( Wafanyakazi ) wake.

ANGALIZO

Uzi huu hauhusiani na Taarifa yoyote ile ya ' Kizushi ' inayoendelea ama ndani au nje ya Tanzania bali ' Malaika ' wangu wazuri ambao huniongoza Kuandika na Kuanzisha Mada hapa JamiiForums Usiku huu ' wamenilazimisha ' nilisisitize hili kutokana na Umuhimu ( Unyeti ) katika Jamii yetu na Masikio yetu.
 
Back
Top Bottom