Family Marriages VS Love Marriages: Which is which?!

Family Marriages VS Love Marriages: Which is which?!

Geoff on my side I would like very much to turn around and go back to where we came from enzi za Family Marriages hasa kwa kuwa kwangu mie naona ndizo zilizokuwa na amani, utulivu, respect you name it- No one alikuwa anajifanya anajua kumzidi mwenzie kila mmoja alijua responsibilities zake kama mke au mume.

Zaidi ya hayo, maadili yalikuwepo kwani mume anaoa mke ambaye amepasishwa mtihani wa tabia na heshima, utulivu e.t.c lakini mume pia anakubaliwa kupewa binti kwa kuwa anafahamika vema tabia na utendaji wake kikazi. Respect inakuwepo kwa kuwa mtu unajua ukifanya upuuzi unakuwa unawaaibisha wazazi wako ambao wanawajibika kw awazazi wa mwenzi wako. Hii ilikuwa inaact kama displine mechanisms kwa wanandoa.

Lakini kwenye love marriage ni ugonjwa mtupu maana tumekwishakuwa brainwashed hadi hatuna tena cha asili. Tunakutana mtaani in the name of 'we love each other' tunakokotana hadi tunapofikia makubaliano ya kuoana ndipo wazazi wanapopata fursa ya kukutana na wazazi wa mkwe wao tena kukutana kwenyewe ni siku ya send off na arusi basi- no more attachment wala nini kiasi kwamba hata watoto wakigombana wazazi hawana mshikamano wowote sana sana kila mmoja anaona mwana wa mwenzie hakumfaa wa kwake! Na sisi tunapogombana/fanyiana uhuni hatuipati ile ladha ya 'ah wazazi wangu wataaibika kwa wazazi wa mwenzangu'

Westerners wametuambukiza ugonjwa mbaya sana unaoitwa haki za binadamu ambazo tumezitafsiri kwenda kuwa haki za mke v/s haki za mume! Mwanamke anajua haki zake (Including haki ya kucheat kama mumewe kacheat!!! ukorofi kama mumewe ni mkorofi!! yaani wenyewe wanasema anamwaga mboga kama mumewe kamwaga ugali ngoma droo yaani ubabe ubabe tu)

I would prefer to go back kule ambako you dont care kama mtu anakupenda au la (kupenda ya kizungu -ya sijui maua , card) all you care ni kuwa amekuchagua wewe uwe wake (kwa kigezo chochote kile) anakuheshimu na kukujali, anaelewa wajibu wake kama mume/mke na baba/mama wa familia. But kurudi kule a lot has to be changed ambayo si rahisi
100% UPO CORRECT!...na kwakweli mtu yoyote anayeamua kuangalia the majority situation atakuwa upande wako!niko na wewe mama.THANK YOU
 
hahaha, huenda mwenzio alikuwa ana maanisha mafanikiwa kwa maana ya kwamba hawajagombana hadi sa ivi manake wengine huwa wanagombana huko huko?

By the way carmel wataka kurudi honeymoon ili uweze kuonja mafanikio?
I am really thinking about doing just that! si unajua hizi story za honemoon zimekuwa nyingi hapa recently hadi nafikiria kurewind lol!
 
Westerners wametuambukiza ugonjwa mbaya sana unaoitwa haki za binadamu ambazo tumezitafsiri kwenda kuwa haki za mke v/s haki za mume! Mwanamke anajua haki zake (Including haki ya kucheat kama mumewe kacheat!!! ukorofi kama mumewe ni mkorofi!! yaani wenyewe wanasema anamwaga mboga kama mumewe kamwaga ugali ngoma droo yaani ubabe ubabe tu)

You see! nilikuwa najiulizza umeenda wapi kumbe ndo ukiandaa vitu vya nguvu kama hivi

Hivi yale maandamano ya wanaharakati ni kesho ama leo? Ningependa baada ya kuandamana dhidi ya bunge, waaanda menhine juu ya issue kama hizi

Bravo MJ1 that was a nice piece (AGAIN)
 
I am really thinking about doing just that! si unajua hizi story za honemoon zimekuwa nyingi hapa recently hadi nafikiria kurewind lol!
HEHEHE!ni bora ukarudi hanemuni...!remember LIFE IS TOO SHORT TO SPEND IT UNHAPPY
 
Hahaha! Kale ka kwangu nilijichagulia mwenyewe.
By the time nimekolea sasa nataka nikakaintrodyuzi kwa wazee, Matesha alikuwa kwa tumbo tayari!
Then tukakamata baraka za wazee.
Afu Mwenyezi Mungu akaaprovu seleksheni yangu. Akagonga muhuri.
Tangu siku hiyo najilia vyangu kitakatifu!
Sijawahi kujuta. Akchuale huwa nashangaa kwanini nilichelewa kukaoa.
Ni kazuri na katamu kwelikweli! Kanajali na kunipenda mpaka najionea wivu!
mi simo we tangaza tu, watu watakaandalia mpango mzima ili waprove shaurilo we!
 
I am really thinking about doing just that! si unajua hizi story za honemoon zimekuwa nyingi hapa recently hadi nafikiria kurewind lol!

hahaha usiambie zimegusa Medula Oblangata.....umeamsha nerves nyingine zilikuwa zimelala eeh...subiri tare 25/3 umpate Emannuel😀😀
 
You see! nilikuwa najiulizza umeenda wapi kumbe ndo ukiandaa vitu vya nguvu kama hivi

Hivi yale maandamano ya wanaharakati ni kesho ama leo? Ningependa baada ya kuandamana dhidi ya bunge, waaanda menhine juu ya issue kama hizi

Bravo MJ1 that was a nice piece (AGAIN)
Ukiamua kusifia mtu,lolz!......😀
 
Usifanye mchezo kuchaguliwa mume ati Geoff si jambo zuri kabisa
JS kwa zamani haikuwa mbaya kiivyo na si wanasema hakuna mzazi amwombeaye mwanae mabaya? So ni wazi uchaguzi wao ungekuwa makini.

Ila ndo kama nilivyosema ukiliangalia hili jambo katika context ya sasa si rahisi kwa sababu kuna mengi yameshatuharibu kiasi kwamba hata tukisema tuapply ya wazazi haita work.

Kumbuka pia unawezamchagua wako ambaye umempenda na mnapendana but kwa kuwa hakuna ile attachment ya wazazi iko siku anawezakukugeuka na ukabakia kutoa kilio cha ajabu- soma visa vyote vinavyotokea mara mume kajiservia tigo kwa nguvu, mume kaleta hawara nyumbani, mume kapiga mama mjamzito au mke kafumwa na houseboy, mke na kiserengeti, yaani ni mtafaruku tu na hao wote walichaguana kwa slogan ya 'we love each other'.
 
dah hutajwi mpwa? Nilikuwa nazungumzia authorities za watu hapa mara umaingia

welcome back!

Hehehehe thanks wapwa kwa kuniokoa na kichapo.
Lakini nilirudi kudumisha mila kama kawa.
Off topic
 
JS kwa zamani haikuwa mbaya kiivyo na si wanasema hakuna mzazi amwombeaye mwanae mabaya? So ni wazi uchaguzi wao ungekuwa makini.

Ila ndo kama nilivyosema ukiliangalia hili jambo katika context ya sasa si rahisi kwa sababu kuna mengi yameshatuharibu kiasi kwamba hata tukisema tuapply ya wazazi haita work.

Kumbuka pia unawezamchagua wako ambaye umempenda na mnapendana but kwa kuwa hakuna ile attachment ya wazazi iko siku anawezakukugeuka na ukabakia kutoa kilio cha ajabu- soma visa vyote vinavyotokea mara mume kajiservia tigo kwa nguvu, mume kaleta hawara nyumbani, mume kapiga mama mjamzito au mke kafumwa na houseboy, mke na kiserengeti, yaani ni mtafaruku tu na hao wote walichaguana kwa slogan ya 'we love each other'.
....ukweli mtupu!wewe unaeleweka kuliko maelezo!nisaidie kumwelewesha kaizer😀
 
Usifanye mchezo kuchaguliwa mume ati Geoff si jambo zuri kabisa

Jana nikiwa stand nilikutana na binti mmoja tukiwa shule nilimpenda sana tena mno nikataka nimchumbie alinipiga kibuti cha ugoko jana nikaonana nae dah Mungu si athumani nikakumbushia ahadi yangu ile naona anakuja sasa huyu nimfanyaje kipindi kile alinitosa sasa anakubali nimuoe hajachuja kweli?
 
Back
Top Bottom