Fanikisha mahusiano ya mbali. . .

kwa uzoefu wangu wanawake ndo wengi hawawezi
mume anafungwa jela mwaka mmoja tu..
akitoka anakuta 'nyumba ina harufu za watu wengine kabisa' lol

huyo mke alikuwa hampendi mume wake, hawezekani mtu unayempenda kiukweli km unavyojipenda wewe uje umsaliti kirahisi hivyo.
 
Time frame ya kuwa mbali inahusu sana.
Mko mbali kwa kipindi gani?
Mi nadhani ili muweze hii muwe watoto sana mcheze ki-egoli egoli au muwe watu wazima sana kifikra ili mtakapokutana hakuna kuulizana the past au kuchunguzana.

vinginevyo ya nini kufa na vifaa vipya kabisa ambavyo havijatumika?
 
Babu hii inahusu wanandoa na wale wanaoanza mahusiano yao wakiwa karibu ila baadae, kwa sababu ambazo ni muhimu kwao wote au kwa mmoja wao ikabidi mmoja kwenda mbali kidogo mf. kusoma, kuuguza mgonjwa, kazi, ugonjwa na mengineyo.

Kuna vitu vingi sana ambavyo vinaweza sababisha wapenzi wakatengana kwa muda. . . na hapa ndipo nnapopaongelea. Kwa wale wanaoanza tayari wakiwa mbali mbali nao sioni ubaya vile vile, maana muhimu ni kumpata yule mtu unaemtaka na uliyeridhika nae.Sasa kama huyo uliyeridhika nae yuko mbali kwa muda?Je ujitoe mhanga na kubebana na mwingine kisa tu yuko karibu? Matokeo yake ndio yake mtu anarudi toka alipokuwepo unatama mkeo/mumeo atoweke ili uende kwa huyo unaempenda toka moyoni, au unaanzisha affair.
Hivyo hapa watu waangalie nini ni muhimu kwao. . . kupata mtu anaempenda kwa dhati au kupata mtu wakutimiza mahitaji yake tu.
 
Inawezekana but ngumu pia!

Hata kuwa karibu tu kunaweza kukawa na challenges kibao.

@Kongosho unaposema msiulizane una maana kwamba huko uendako au aendako awe huru kujihusisha na watu wengine ehhh?
 


Hapa sasa nimekuelewa Lizzy,

Katika maisha ya ndoa, kutengana kwa muda ni jambo la kawaida sana halizuiliki!! Ila mara nyingi inatakiwa kuwa muda mfupi mfupi tu. Ukizidi sana basi ni mwaka mmoja. Sishauri watu kukaa mbali kwa zaidi ya mwaka....Hata kama ni shule...The meaning of life should always come first!! Hakuna sababu na pia ni vigumu kwa mtu ambaye yuko kwenye mahusiano kuanza kukumbatia mito kwa zaidi ya mwaka....!! Halafu ukutane na winter kama ya 2010!!...No way, hicho kikombe sikitaki kabisa!!

Kuna mifano mingi ya watu ambao walijaribu haya mambo eti kwa sababu ya shule na kazi...Matokeo yake ni mabaya sana!! Wengine ndoa ziliisha baada ya masomo au zimebaki zikichechemea kwa mguu mmoja kama uyoga!
 
 
Sio uwe huru but bya any means mkikutana hamna kuuliza what happened when the Monitor wasnt there

uwe ulisikia kwa mbali, unaichunia kiutu uzima.
Hata hivyo haya ya watoto zaidi ndo inapendeza. Ndo maana sasa hivi ukikiuliza kidada, are u dating?

Unapewa jibu, my fiance is in UK, Yugoslavia, Chechnia. uSA

yanawafaa hao
Hata kuwa karibu tu kunaweza kukawa na challenges kibao.

@Kongosho unaposema msiulizane una maana kwamba huko uendako au aendako awe huru kujihusisha na watu wengine ehhh?
 


Lizzy thanks for the thread,as always it is such a great thread with unbelievable educative ideas.I have just came along in this javi though i have been visiting for sometimes.Very sorry for this,i have some questions which might be personal but it is n't,what is your profession?are you relationship expert,life couch or just someone with so much life experience.I got so much to ask please PM me if you do not mind
 

Nimekusoma babu.
Kukaa mbali kwa zaidi ya mwaka mmoja kwakweli sio afya kwa mahusiano. Ni vizuri katika huo muda wa masomo/kazi watu wajitahidi kukutana angalau mara mbili kwa mwaka ili wasisahau kile walichonacho. Pia warekebishe kama kuna sehemu walikoseana kabla mto haujawa bahari.
 
Thanks.
I don't mind, niPM ntakujibu maswali yako yote.
 
Hahahahah. . .
Boyfriend Dubai, mchumba US na mume Darisalama.
 
Huyo ni wewe. Utakuwa na uhakika gani na mwenzio Shantel?
Sitajali wala kumuwazia as long as yuko in touch na mie kwa sana na ananihakikishia im the one and all those love staff wala sijali
kuaminiana ni kitu kizuri sana japo ni kitu kigumu kwa mahusiano ya mbali
 
Sitajali wala kumuwazia as long as yuko in touch na mie kwa sana na ananihakikishia im the one and all those love staff wala sijali
kuaminiana ni kitu kizuri sana japo ni kitu kigumu kwa mahusiano ya mbali
Bora wewe mwaya.
Kuna watu wanaishi kwa wasiwasi mpaka basi weee.
 
Huyo ni wewe. Utakuwa na uhakika gani na mwenzio Shantel?

Babu kwani unaeagana nae asubuhi na kukutana jioni una uhakika gani nae?

@AirTanzania. . .never ni neno la ajabu.Ukiliendekeza huwezi fanikisha chochote maishani mwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…