Fanikisha mahusiano ya mbali. . .

Fanikisha mahusiano ya mbali. . .

Sorry I meant miaka 5. . . ..

Lizzy,

Miaka 5 ni mingi sana...Hebu fikiria, mtoto ambaye ulimwacha tumboni unakuta yuko anamalizia chekechea au tayaria kaingia darasas la kwanza.

Kama inawezekana, hiyo kamari ni ya kukwepa kabisa.....

Nitakuja na mfano wa hii miaka 5 baadaye kidogo! Ngoja nikawapigie hadith wajukuu walale!!
 
Heheheheh. . . hata mimi nimeona hiyo ni too much babu.Mkikutana tena unakuta mpaka sura zilishabadilika,inawabidi kuanza upya na sio kuendelea.

Twasubiria mfano. . .
 
Linda chako, ikibidi njoo na gobole
mie changu nakihifadhi kama hela zinavyowekwa na wamama
kwenye engachifu afu kifuani
hadi mpolee atoe atakuwa kafanya kazi ya ziada

Babu you're invading my territory...lol
 
Kibunango nasubiria hiyo mifano mingine. . . .

Huyu ni rafiki yangu toka Kongo, mwanamuziki wa reggae, ana account myspace, facebook, skype na networking zingine... Tatizo kubwa kwake ni kuwa na uhusiano wa kawaida. Amejaribu kujichangaya na local girls pasipo mafanikio yoyote zaidi ya kuambulia "one night stand".

Siku moja alikutana na comment nzuri sana katika myspace kwenye moja ya muziki wake. Alivutika na comment ile na kujikuta anamtafuta aliyeitoa. Hakupata usumbufu wowote kumpata, na baada ya muda mfupi walijikuta wakihama kuongelea muziki wa reggae na kujichimbia kwenye mapenzi. Hatua hii ilikwenda sambamba na kuwa pamoja kwenye facebook, ambapo wote walionyesha dunia kuwa wapo pamoja.

Mdada aliyetoa comment kwenye myspace anaishi Canada, na ni mwendo wa KM nyingi hadi hapa kwa Mkongo. Hilo halikuwa tatizo kwake, kwani aliona tayali ameshampata mwenza wake. Mahusiano yao yaliendelea vema na kwa kasi ya ajabu, kiasi kwamba Mkongo yule kujihisi kuwa Mcanada anaishi nae nyumbani kwake ilhali ilikuwa ni online tu!

Mcanada akaona isiwe shida, kapanda ndege hadi mtaani. Mkongo katupa taarifa kuwa bibie leo atakuwepo mtaani, ila anaona noma kumkaribisha nyumbani kwake, kwani hana chochote cha maana kama alivyokuwa akijisifu kwa binti huyo. Tukamshauri ni vema amwonyeshe mahali anapoishi ili kuendelea kujenga mapenzi yao, isitoshe binti keshasafiri umbali wote huo kwa ajili yake. Hata hivyo kwa mshangao wa wengi alikataa kabisa kumkaribisha nyumbani kwake.

Mcanada aliyeumbika vema alifika na hamu tele ya kumwona mpenzi wake na ni baada ya mwaka mmoja wa kuwasiliana online. Mkongo yule alimchukua mgeni wake hadi dukani, wakafanya shopping ya vyakula na vitu vingine. Njiani akaniambia break ya kwanza ni nyumbani kwako! Nikashangaa!

Pale nyumbani kwangu, niliwakaribisha vizuri, chakula kikapikwa, na unywaji ukaendelea kama kawaida. Tatizo lilikuwa kwa binti Mcanada, kwani kila mara alikuwa akiulizia ni saa ngapi wataenda kwenye nyumba yao!. Masaa yakapita bila dalili yoyote ya Mkongo kumpeleka kwake. Hata walipochoka Mkongo alitonya kuwa niwapeleke kwenye hoteli ya karibu. Nikafanya hivyo.

Baada ya wiki nzima kukaa hotelini Mcanada yule akaondoka na ikawa ndio mwisho wa mawasiliano na Mkongo.
 
@kibunango
wakongo ni exceptional case kwenye mahusiano
hata hapa dar wanawateka sana wadada wanaofanya kazi
ila akili zao ziko kwenye sox wakivua tu sox hawana akili
ndo mikongo ilivyo
 
Heheheheh. . . hata mimi nimeona hiyo ni too much babu.Mkikutana tena unakuta mpaka sura zilishabadilika,inawabidi kuanza upya na sio kuendelea.

Twasubiria mfano. . .

Iko hivi,

Kuna jamaa yetu mmoja alipata nafasi ya kwenda nje (naomba nisitaje nchi) kwa ajili ya PhD. Alitakiwa kukaa huko 4-5yrs. Huku nyuma, alikuwa na mpenzi wake ambaye walikuwa tayari wamevishana pete ya uchumba....Basi wakakubaliana kusubiri hadi muda muafaka ili wafunge ndoa..Na hii ilikuwa ama jamaa akipata pesa arudi au ikiwezekana binti amfuate. Vinginevyo ilibidi wasubiri hadi jamaa amalize shule. Pamoja na ugumu wa mawasiliano enzi hizo (mid 1990s), lakini waliweza kuongea walau kila baada ya siku 2 kupitia kwa jirani wa yule mchumba wake. Yule binti alihamia mji mwingine kwa hiyo nilionana naye baadaye sana.... Inasemekana jamaa baadaye alipunguza mawasiliano ila bado walikuwa wako pamoja. Hata hivyo siku anatua airport Dar (5 yrs later), alikuja na dada mwingine ambaye wakuwa wamezaa pamoja mtoto wa kiume. Mbaya zaidi binti wa watu alienda kumpokea!!

Babu DC!!
 
@kibunango
wakongo ni exceptional case kwenye mahusiano
hata hapa dar wanawateka sana wadada wanaofanya kazi
ila akili zao ziko kwenye sox wakivua tu sox hawana akili
ndo mikongo ilivyo

Mhhhh Dada Mkuu,

Mbona umemuacha solemba Babu???
 
lizzy leo umenigusa sana na mimi ni mmoja wapo wa mahusiano ya mbali na ni kweli kuwa bila hayo mambo ulliyohainisha hapo huwez kufika na mwenzio
 
lizzy leo umenigusa sana na mimi ni mmoja wapo wa mahusiano ya mbali na ni kweli kuwa bila hayo mambo ulliyohainisha hapo huwez kufika na mwenzio

Ni mahusiano ya kudumu au ya muda??

Na mnategemea kukaa mbali na mwenzio kwa muda gani???
 
Iko hivi,

Kuna jamaa yetu mmoja alipata nafasi ya kwenda nje (naomba nisitaje nchi) kwa ajili ya PhD. Alitakiwa kukaa huko 4-5yrs. Huku nyuma, alikuwa na mpenzi wake ambaye walikuwa tayari wamevishana pete ya uchumba....Basi wakakubaliana kusubiri hadi muda muafaka ili wafunge ndoa..Na hii ilikuwa ama jamaa akipata pesa arudi au ikiwezekana binti amfuate. Vinginevyo ilibidi wasubiri hadi jamaa amalize shule. Pamoja na ugumu wa mawasiliano enzi hizo (mid 1990s), lakini waliweza kuongea walau kila baada ya siku 2 kupitia kwa jirani wa yule mchumba wake. Yule binti alihamia mji mwingine kwa hiyo nilionana naye baadaye sana.... Inasemekana jamaa baadaye alipunguza mawasiliano ila bado walikuwa wako pamoja. Hata hivyo siku anatua airport Dar (5 yrs later), alikuja na dada mwingine ambaye wakuwa wamezaa pamoja mtoto wa kiume. Mbaya zaidi binti wa watu alienda kumpokea!!

Babu DC!!
Babu hili wala sio swala la umbali ila jamaa alipania.Mpaka akazaa na kuzaa, naakafungasha mwanamke na mtoto kuja nae sio swla la LDR bali ni swala la ubinafsi.Kilichomfanya asimwache huyo dada wa watu baada ya kuopoa mwingine ni nini?Watu wengine hovyo sana.

@Kibunango asante sana.
Mfano wa kwanza naona umeongozwa ile ishu ya maneno ya watu+kutokuwepo kwa imani.

Wa pili unasikitisha maana imani ilikuwepo ila aliyepewa hakustahili.Ukishaanza kuchomekea chomekea uongo mahusiano hata ya karibu mwisho wake unakua karibu kuliko kawaida. Mbaya zaidi ni kwamba siku hizi hata yule mnaekutana mtaani na kupelekana lunch na dinner anaweza akakudanganya hivyo hivyo,watu sijui wana matatizo gani. Maana sioni faida yoyote wanayopata zaidi ya kupoteza muda wao na wa mwenzao kisha kuishia kupata aibu mwishoni.
 
lizzy leo umenigusa sana na mimi ni mmoja wapo wa mahusiano ya mbali na ni kweli kuwa bila hayo mambo ulliyohainisha hapo huwez kufika na mwenzio

Jitahidini mwaya mfikoe malengo yenu. . ..
 
Babu hili wala sio swala la umbali ila jamaa alipania.Mpaka akazaa na kuzaa, naakafungasha mwanamke na mtoto kuja nae sio swla la LDR bali ni swala la ubinafsi.Kilichomfanya asimwache huyo dada wa watu baada ya kuopoa mwingine ni nini?Watu wengine hovyo sana.

Umeona sasa Lizzy,

Ndiyo maana nikasema kuwa mahusiano yanawahusisha watu wawili, na kila mtu ana kichwa chake mwenyewe na akili zake zinamtosha mwenyewe...Ni vigumu kujua analilowaza.

Halafu kwenye hii story,...huyo dada anaomboleza hadi leo kwani alitema wachumba kibao kwa kumsubiri mtu ambaye hakustahili kupewa hiyo share!!
 
Kama wanaume wote wenye nyumba ndogo wake zao wako safarini ntakubaliana na wewe.
Au labda unambie kwa walio safarini waume zao wana nyumba ndogo more than one.

Kikubwa mkikutana ni kupima HIV maisha yanasonga; waliokuwa wanatoa service wanapigwa stop.

Na sipendi hilo neno la trust; trust ndo inayotumaliza. Dawa ni kupima for both partners' sake.

Watu samtaimu munachanganya madawa bana, Ishu sio uaminifu ishu ni binadamu ameumbwa na udhaifu flani kimaumbile, acheni kudanganywa na mapenzi ya kwenye movie.

Kuna vitu kama temptation na situation, vishaiwishi na vidugushi all in all, mapenzi ya mbali haya work. This is the plain truth
 
Umeona sasa Lizzy,

Ndiyo maana nikasema kuwa mahusiano yanawahusisha watu wawili, na kila mtu ana kichwa chake mwenyewe na akili zake zinamtosha mwenyewe...Ni vigumu kujua analilowaza.

Halafu kwenye hii story,...huyo dada anaomboleza hadi leo kwani alitema wachumba kibao kwa kumsubiri mtu ambaye hakustahili kupewa hiyo share!!
Ndio maana ameniboa maana alimfunga dada wa watu pasipo sababu. Mbaya sana hiyo kitu kwakweli. . . mimi kama mtu hanitaki/hanipendi/hanihitaji ni bora anieleze mapema niangalie ustaarabu mwingine.Mtu kama huyo jamaa ana tabia mbaya sana. . . kaniboa sana.
 
Kama wanaume wote wenye nyumba ndogo wake zao wako safarini ntakubaliana na wewe.
Au labda unambie kwa walio safarini waume zao wana nyumba ndogo more than one.

Kikubwa mkikutana ni kupima HIV maisha yanasonga; waliokuwa wanatoa service wanapigwa stop.

Na sipendi hilo neno la trust; trust ndo inayotumaliza. Dawa ni kupima for both partner's sake.

Karibu sana dada yetu kwenye home yetu hii ya MMU,

Suala la uaminifu ni tatizo ila pia kuna jambo la msingi ambalo hatujaligusia....Malengo ya ndoa ni kuishi pamoja, ...kwenye paa moja na kulala kitanda kimoja!! Labda kama kuna mtafaruku kwenye ndoa... Hii inasaidia wanandoa kuwa karibu na kusaidiana katika mambo yanayowatokea siku hadi siku.. Na pia kuwa na mipango ya pamoja ya maisha ikiwemo kulea watoto!!

Kwa hiyo uzinzi upo hata bila kuwa mbali ingawa umbali unaweza kusaidia watu wanaopenda unzinzi kuwa na opportunity ya kufanya upuuzi wao.
 
Ndio maana ameniboa maana alimfunga dada wa watu pasipo sababu. Mbaya sana hiyo kitu kwakweli. . . mimi kama mtu hanitaki/hanipendi/hanihitaji ni bora anieleze mapema niangalie ustaarabu mwingine.Mtu kama huyo jamaa ana tabia mbaya sana. . . kaniboa sana.

Kweli Lizzy,

Ndo maana mie binafsi nachukia LDRs ambazo zinakuwa za muda mrefu sana. Kama hillo suala linechukua muda mfupi lisingemkwanza dada wa watu kiasi hicho.

Ila ujue kuwa wa namna hiyo hawawezi kukueleza lolote!
 
Babu huyo kaka ni type ile mko mji mmoja alafu siku tu anakuibukia na kukwambia naoa, au unaishia kusikia kwa marafiki zake. Yani huo umbali sio tatizo. . . tatizo ni yeye.

Asante hapo juu kwa kukumbusha wajukuu kwamba uzinzi unawezekana hata kwa yule unaebanana nae kila siku.
 
Kibunango nasubiria hiyo mifano mingine. . . .
Nilibahatika kupata udhamini wa kusoma nje ya TZ kwa miaka miwili. Sikuwa peke yangu, tulikuwa ni wengi na ni wengi sana. Tofauti miongoni mwetu ilikuwa ni muda wa masomo. Wapo waliopata udhamini wa miaka mitatu, miwili na miezi tisa.

Kundi la miezi tisa wengi wao walikuwa tayali wana mahusiano ya kindoa, uchumba na uhusiano wa kawaida wa kimapenzi. Wengi tuliona kwa miaka miwili/mmoja ama miezi tisa ni muda mfupi sana. Zaidi waliokuwa kwenye mahusiano walipenda kusisitiza kuwa huo ni muda mfupi sana na utakwenda haraka pasipo kujua. Mie niliyekuwa single sikuwa na chochote cha kujadili katika hilo, kwani ndoto zangu zilijiweka zaidi katika kukutana na marafiki wapya wa kike.

Baada ya miezi mitatu ugenini mambo yalianza kubadilika. Hapa napenda kuweka wazi kuwa mwezi wa kwanza huko ugenini, ulikuwa ni mwezi Mtukufu, Jiji lilikuwa limepoa na utulivu usio kifani. Mwezi uliofuata ulikuwa wa kuzoea shule mpya na kujaribu kupata hili na lile katika mazingira ya ugenini.

Vituko vilianza mapema baada ya kumalizika kwa miezi mitatu, ingawa dalili za kupotoka zilianza mapema kidogo ya hapo. Ni siku ambayo kijana mmoja aliposhauri kufanyike party nyumbani kwake, akinadada wakiandaa vyakula mbalimbali na akina kaka wakiingia madukani kutafuta kila aina ya vinywaji kwa party hiyo. Huu ulikuwa ni mwanzo wa kuona ni jinsi gani long relationship inavyoweza kutofanikiwa kwa sababu mbalimbali ... Hapa chini naweka mifano kadhaa kwa yale niliyoweza kuyaona baada ya watu kufunguka baada ya party hiyo.

Ashura
Ni mke wa mtu wa kawaida hapo nyumbani (TZ). Mumewe ni fundi mkubwa wa magari na wamejariwa watoto wawili katika ndoa yao ya miaka sita. Ashura ni mfanyakazi serikalini na ni msichana mwenye kujipenda sana. Sio mimi ama mumewe ambaye alikuwa anajua nini Ashura anapenda siku zote. Kumbe binti huyu anapenda sana watu maarufu.

Kupitia party hiyo na baadae baada ya party hiyo alianzisha uhusiano wa kudumu na kijana moja ambaye alikuwa ni maarufu sana huko nyumbani (TZ). Hakuona aibu yoyote ya kumsaliti mume wake. Alifanya kila alichoweza kumweka karibu kijana huyo kwa muda wote wa miezi tisa aliyokaa hapo.

Fatuma
Hakuwahi hata siku moja kuamwamini mume wake. Mume wake ndie aliyemchongea mchongo wa kwenda kusoma nje ya Tanzania. Siku zote alikuwa kwenye simu akiongea na mume wake, hatukujua ni mapenzi ama ni wivu tu. Wiki moja kabla ya party hiyo alionekana kuwa ni mnyonge sana. Shoga zake walisema kuwa mume wake ameondoka TZ na kwenda nje ya nchi kikazi.

Fatuma kwa upande wake aliona kuwa mume wake atakuwa ameenda kufanya ufuska kwa kimada mmoja ambae alikuwa nje ya TZ lkn nchi tofauti na yetu. Tokea siku hiyo nae akaona isiwe shida, wenye bahati wakabahatika

Mwaka mmoja baada ya kurudi Tanzania ndoa yao iklivunjika.

Grace
Baada ya kudumu katika ndoa kwa miaka zaidi ya sita, alijikuta hana hamu tena na mume wake. Na zilipotekea nafasi za kusoma nje aliona ndio wakati pekee ambao ataweza kurejesha upendo kwenye ndoa yake iliyoweza kutoa watoto wazuri wawili. Akiwa ni afisa mkubwa serikalini na mume akiwa ni afisa katika idara ya nje ya serikali maisha yao yalikuwa ni mazuri sana.
Aliwabeza sana wale wote ambao wameshindwa kuvumilia katika kipindi hicho kifupi cha kwa na wapenzi hao. Alijiangalia matatizo yake kwenye ndoa yake na nafasi yake aliyokwa nayo, na akaona bado anaweza kuhimili mahusiano ya mbali.

Miezi sita baada ya ile party, alionekana kapendeza sana, kulikoni? Kumbe nae tayali kesha ingia kundini! Uzalendo ulimshinda na kuamua kutafuta kijana... Baada ya kurudi nyumbani aliamua kujitenga na mume wake.. dhamiri imemponza?

Juma
Huyu ndie aliyekuwa kinara wa kuchambua wale wote walioshindwa kuwa wahaminifu kwenye mahusiano yao ya mbali. Zaidi umaarufu wake ulizidi kwa kuwa ndie Mtz pekee aliyekuwa analeta mawasiliano ya simu kwa watz.(Mobile phone in early 90's ilikuwa issue)

Akiwa ameacha watoto watatu na mke nyumbani, alijikuta akiingilia ndoa ya mtu kwa kujihushisha na mke wa mtu. Uhusiano wao ulidumu kwa muda mrefu sana, kabla ya mwanamke huyo kujua kuwa hakuwa peke yake.

Mwanamke amepoteza ndoa yake na Jamaa sasa ana wake watau.

Zuhura
Hakuwahi kuwa kwenye serious relationship, Hata hivyo kabla ya kuondoka TZ alikuwa engaged! Na siku zote mdomo wake ulijaa jina la kijana mtarajiwa. Mwaka mmoja baadae kaishia kwa mnajeria

Sasa anaishi Marekani na ana watoto watatu.
 
Back
Top Bottom