Kibunango nasubiria hiyo mifano mingine. . . .
Nilibahatika kupata udhamini wa kusoma nje ya TZ kwa miaka miwili. Sikuwa peke yangu, tulikuwa ni wengi na ni wengi sana. Tofauti miongoni mwetu ilikuwa ni muda wa masomo. Wapo waliopata udhamini wa miaka mitatu, miwili na miezi tisa.
Kundi la miezi tisa wengi wao walikuwa tayali wana mahusiano ya kindoa, uchumba na uhusiano wa kawaida wa kimapenzi. Wengi tuliona kwa miaka miwili/mmoja ama miezi tisa ni muda mfupi sana. Zaidi waliokuwa kwenye mahusiano walipenda kusisitiza kuwa huo ni muda mfupi sana na utakwenda haraka pasipo kujua. Mie niliyekuwa single sikuwa na chochote cha kujadili katika hilo, kwani ndoto zangu zilijiweka zaidi katika kukutana na marafiki wapya wa kike.
Baada ya miezi mitatu ugenini mambo yalianza kubadilika. Hapa napenda kuweka wazi kuwa mwezi wa kwanza huko ugenini, ulikuwa ni mwezi Mtukufu, Jiji lilikuwa limepoa na utulivu usio kifani. Mwezi uliofuata ulikuwa wa kuzoea shule mpya na kujaribu kupata hili na lile katika mazingira ya ugenini.
Vituko vilianza mapema baada ya kumalizika kwa miezi mitatu, ingawa dalili za kupotoka zilianza mapema kidogo ya hapo. Ni siku ambayo kijana mmoja aliposhauri kufanyike party nyumbani kwake, akinadada wakiandaa vyakula mbalimbali na akina kaka wakiingia madukani kutafuta kila aina ya vinywaji kwa party hiyo. Huu ulikuwa ni mwanzo wa kuona ni jinsi gani long relationship inavyoweza kutofanikiwa kwa sababu mbalimbali ... Hapa chini naweka mifano kadhaa kwa yale niliyoweza kuyaona baada ya watu kufunguka baada ya party hiyo.
Ashura
Ni mke wa mtu wa kawaida hapo nyumbani (TZ). Mumewe ni fundi mkubwa wa magari na wamejariwa watoto wawili katika ndoa yao ya miaka sita. Ashura ni mfanyakazi serikalini na ni msichana mwenye kujipenda sana. Sio mimi ama mumewe ambaye alikuwa anajua nini Ashura anapenda siku zote. Kumbe binti huyu anapenda sana watu maarufu.
Kupitia party hiyo na baadae baada ya party hiyo alianzisha uhusiano wa kudumu na kijana moja ambaye alikuwa ni maarufu sana huko nyumbani (TZ). Hakuona aibu yoyote ya kumsaliti mume wake. Alifanya kila alichoweza kumweka karibu kijana huyo kwa muda wote wa miezi tisa aliyokaa hapo.
Fatuma
Hakuwahi hata siku moja kuamwamini mume wake. Mume wake ndie aliyemchongea mchongo wa kwenda kusoma nje ya Tanzania. Siku zote alikuwa kwenye simu akiongea na mume wake, hatukujua ni mapenzi ama ni wivu tu. Wiki moja kabla ya party hiyo alionekana kuwa ni mnyonge sana. Shoga zake walisema kuwa mume wake ameondoka TZ na kwenda nje ya nchi kikazi.
Fatuma kwa upande wake aliona kuwa mume wake atakuwa ameenda kufanya ufuska kwa kimada mmoja ambae alikuwa nje ya TZ lkn nchi tofauti na yetu. Tokea siku hiyo nae akaona isiwe shida, wenye bahati wakabahatika
Mwaka mmoja baada ya kurudi Tanzania ndoa yao iklivunjika.
Grace
Baada ya kudumu katika ndoa kwa miaka zaidi ya sita, alijikuta hana hamu tena na mume wake. Na zilipotekea nafasi za kusoma nje aliona ndio wakati pekee ambao ataweza kurejesha upendo kwenye ndoa yake iliyoweza kutoa watoto wazuri wawili. Akiwa ni afisa mkubwa serikalini na mume akiwa ni afisa katika idara ya nje ya serikali maisha yao yalikuwa ni mazuri sana.
Aliwabeza sana wale wote ambao wameshindwa kuvumilia katika kipindi hicho kifupi cha kwa na wapenzi hao. Alijiangalia matatizo yake kwenye ndoa yake na nafasi yake aliyokwa nayo, na akaona bado anaweza kuhimili mahusiano ya mbali.
Miezi sita baada ya ile party, alionekana kapendeza sana, kulikoni? Kumbe nae tayali kesha ingia kundini! Uzalendo ulimshinda na kuamua kutafuta kijana... Baada ya kurudi nyumbani aliamua kujitenga na mume wake.. dhamiri imemponza?
Juma
Huyu ndie aliyekuwa kinara wa kuchambua wale wote walioshindwa kuwa wahaminifu kwenye mahusiano yao ya mbali. Zaidi umaarufu wake ulizidi kwa kuwa ndie Mtz pekee aliyekuwa analeta mawasiliano ya simu kwa watz.(Mobile phone in early 90's ilikuwa issue)
Akiwa ameacha watoto watatu na mke nyumbani, alijikuta akiingilia ndoa ya mtu kwa kujihushisha na mke wa mtu. Uhusiano wao ulidumu kwa muda mrefu sana, kabla ya mwanamke huyo kujua kuwa hakuwa peke yake.
Mwanamke amepoteza ndoa yake na Jamaa sasa ana wake watau.
Zuhura
Hakuwahi kuwa kwenye serious relationship, Hata hivyo kabla ya kuondoka TZ alikuwa engaged! Na siku zote mdomo wake ulijaa jina la kijana mtarajiwa. Mwaka mmoja baadae kaishia kwa mnajeria
Sasa anaishi Marekani na ana watoto watatu.