Fanya biashara ndani ya biashara yako, uokoe pesa unazopoteza na ujiongezee faida

Hivi kuna mtu anabisha kabisa kwamba kilichoandikwa hapa hakiwezekani?

Mfano halisi huu hapa, kuna boss aliniajiri soon after mimi kumaliza chuo ana hotel kubwa na kampuni ya catering , ana duka la vyakula la jumla anasafirisha mizigo so ana magari mengi sana. Sasa basi ana Mashamba makubwa ya mpunga, mhindi maharage nk,

Ambayo akivuna hupeleka mavuno kwenye duka lake la nafaka ambapo huchangnya na bidhaa zingine na kuiuzia hotel, wafanya Kazi wa makao makuu wanalishwa na hotel na ni lazima ofisi iwalipie, mpaka naacha Kazi alikuwa ana sheli 3 ambazo gari zake za usafirishaji zilikuwa zinakunywa mafuta hapo na hizo gari ndo zinasafirisha mazao yake na mradi wa kilimo unatakiwa ulipe gharama.

Kila project inajitegemea na ina wafanyakzi tofauti kabisa. Wenzake wanaishia kumuita mchawi. Hili linawezekana kabisa sio kila kitu cha kubisha jamani.
 
Hata wewe Hawatakuamini
 
Nimekubali

Biashara inahitaji mahesabu,kujiamini na kuthubutu.

Huu ushauri unapaswa kufuatwa.
 
Hivi mkuu una muda wakujibizana na watu ambao hawafanyi biashara?

na kama anafanya biashara mpaka Leo kashafanya biashara zaidi ya 20 na zote hazifanyi tena saivi zimeshamshinda..

ukimuuliza kwann hazifanyi atakupa sababu essay nzima..

unamuona n mtu wa kubishana nae huyo,kuna comment nyingine unazisoma halafu unapita kama hujaziona.

Muhimu Tusiache Ambiana ukweli (tupeane elimu) atae ona tunaongea theory unamuacha kama alivyo hao ndio waita wenzao wachawi....
 
Matajiri wote wangekuwa na mawazo kama yako nadhani hakuna mtu mwingine atakaekuwa na hela zaidi yao.
Hata sasa hivi kuna mwenye hela zaidi yao?! Wote tunapambana tuwe kama wao..

ingekua rahisi hata wewe ungekua na hela ila huna na hata kama unazo si kama za hao unaowaita Matajiri..

unajua ni kwanini? kwasababu wana njia nyingi za utafutaji na za kuingiza kipato,endelea kuwa underrate wanaoitwa "matajiri" usiwachukulie poa Asee.

Hiyo kauli yako ya "Matajiri wote wangekua na mawazo kama yangu" ifikirie mara mbili halafu ukae chini ujiulize Je hao matajiri wana mawazo kama Yako?
 
Mkuu CONTROLA Ebu Andaa somo kwa mtu anaetamani kuja DAR kuanza maisha bila kutegemea ndugu

Gusa kuanzia Maeneo ya kuishi Aanze na budget gani, akimbize biashara gani nk
Nitaifanya kwa Ajili yako Mwisho nitaku TAG...
 
Nitaifanya kwa Ajili yako Mwisho nitaku TAG...
Naisubiri kwa hamu maana Nataka nije mjini

Niliwahi kumsikiliza Masanja mkandamizaji namnukuu Ukiona unafilisika kimbilia mjini maana mjini kuna fursa nyingi hata watu tu ni fursa
 
M/Mungu akubariki kama unamuamini maana kuna mijitu humu mibishi hawataki hata kusikia uwepo wa M/Mungu
 
We jamaa umemaliza ubishi....thread closed
 
Asante kwa SoMo je na sisi tusiokuwa na biashara na wazo tumelielewa tufanyanyaje mkuu au tuanze vip kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…