Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu nashukuru nimefanya hivyo nimefanikiwa kwa kiasi japo bado sound sio quality Kama mwanzoChukua waya nene mfano wa 4mm
Unga kwenye ground ya power supply na pale kwenye ki bati cha frash(ground!)
Sio quality kama mwanzo kwa maana gani?Mkuu nashukuru nimefanya hivyo nimefanikiwa kwa kiasi japo bado sound sio quality Kama mwanzo
Kama Kuna mbinu zaidi naomba tafadhali
Pia nifunge kifaa gani ili kupunguza kidogo bass
Kabla ya kuweka mp3 module mkuuSio quality kama mwanzo kwa maana gani?
Yaan baada au kabla ya kuweka hiyo mp3
Iko vizuri ina ina features za 3DSeapiano wameleta sp 993 ni noma inagonga balaa na ina umbo la kibaba zaidi
Ni hatari sn nadhan huyu ndiye mpinzani halisi wa seapiano sp 1002 iliyokuwa inasifiwa kuliko seapiano zote mzki mzto na umetulia sn.....Iko vizuri ina ina features za 3D
Unapoongeza spika ni lazima pia uongeze amplifier kwa sababu ya hizo spika za ziada.Habari ya wakati
Natumaini tuko salama
Fanya haya ili subwoofer yako na sound system yako idumu kwa muda mrefu
[emoji1314] usichajie simu sehemu ya kuchomeka frash disk
Sababu hi imekua ndio sababu kuu ya kuuwa system ya frash ya watu wengi zaidi Ile haikutengenzwa kwajiri ya kuchajia bali kuchomeka frash peke. Na hi sio kwenye subwoofer pekee bali hata DVD players
[emoji1314] usiongeze speaker nyingine zaidi ya zile zilizokuja na system yako
Mara zote redio inapotengenezwa hua inatengenezwa kusukuma speaker za kiwango husika
Unapoongeza za kwako bila ya kua na kipimo maalumu au kiwango cha ukinzani wa coil ya speaker yako (ohms) KUNAUWEZEKANO wa kusababisha uharibifu wa system yako.
Sikukatazi kufanya hivyo ila kwanza elewa kiwango cha ohms kinachotakiwa na system yako kisha elewa kiwango cha ohms cha speaker zako zote kabla ya kuziunganisha na sound system yako
[emoji1314] usipende kuweka sauti kubwa sana kwa muda mrefu na mara kwa mara.
Hii inawahusu zaidi wenye subwoofer za mchina.
Hii itakusaidia kuifanya subwoofer yako iishi kwa muda mrefu zaidi.
Hii inawahusu wenzangu na mimi wa birthday na vipaimala[emoji16].
Kwa faida yako tu ni kuwa.
Unapoongeza sauti kwenye redio yako tafsiri yake ni kua unaruhusu umeme mwingi kutoka kwenye amplify yako na kwenda kwenye speaker.
Hivyo ongezeko la joto hupanda zaidi kwenye baadhi ya components zinazounda circuit za subwoofer yako (components zinazounda circuit ni vitu vote kiujumla vinavyounda ramani, kadi, mashine ya system yako).
Hivyo unapoifungua kwa sauti kubwa kwa muda mrefu zaidi ni kua ile joto inakuwepo humo kwa muda mrefu.
Kumbuka kua subwoofer nyingi kama sio zote hazina mfumo mzuri wa kupooza (feni)
[emoji1314] Kwa namna yoyote jitahidi mende, panya wasiingie ndani ya system yako
Sababu mkojo wao huweza kutengeneza short ya components.
Hii ni kwa wale wanaotumia home theater na subwoofer hizi za kisasa
Pia panya hula waya na speaker.
Hivyo unatakiwa kuzilinda kwa namna yoyote utakayoiweza
[emoji1314]tumia voltages stabilizer kulinda vifaa vyako vya kielecronic.
Hii sio kwenye sound system pekee.
Bali vifaa vyako vyote vinatakiwa kulindwa na stabilizer.
Stabilizer za kisasa huweza kujizima zenyewe pindi umeme unapokua juu au chini ya kiwango.
Na zipo nyingine zinabalance bila ya kuleta hitilafu ya vifaa vyako
Kwa leo ni hayo tu
For additional
Ili kupata sound safi (bass nzuri) usiweke subwoofer yako juu ya meza au stool au sehemu itakayoitenga mbali na floor
Itakupa good sound ikiwa on floor
View attachment 2368030
K’phin.