FAO: Tusipowadhibiti nzige wanaoikabili Ethiopia, Kenya na Somalia watasambaa

FAO: Tusipowadhibiti nzige wanaoikabili Ethiopia, Kenya na Somalia watasambaa

Hao wadudu waskie hivyo hivyo ni noma,Siku kadhaa tu wanaleta baa la njaa.
FAO waache unoko wawaache huko somalia waendelee kupambana na ALSHABABU
Alshabab si wanajifanya wajanja wawapige risasi hao nzige tuone.Nawaunga mkono nzige kuendelea kuwepo somalia kushambulia mashamba ya ALSHABAB
 
ningependa kufahamishwa nini kina sababisha Population Ya hao viumbe kuwa wengi kiasi hicho, Wanatokea wapi, Wanazaliana vipi mpaka wanakuwa wengi hivyo, Chanzo Chao ni wapi na ni nini ?
au ni lab 🧪 made/modified boosted

Naombeni msaada wajuvi
 
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limeonya kwamba nzige walioivamia Ethiopia, Kenya na Somalia sasa ni wimbi kubwa kuwahi kushuhudiwa hivi karibuni na lisipodhibitiwa kuna uwezekano wa kusambaa katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Wimbi kubwa la nzige walionekana kutamalaki angani na kughubika mashamba pembe ya Afrika, kwa mujibu wa FAO tayari limeshasababisha uharibifu mkubwa kwa kusambaratisha maelfu ya ekari za mazao hali ambayo inaathiri uhakika wa chakula katika nchi hizo ambazo zinakabiliwa na changamoto nyingine nyingi ikiwemo kutokuwa na uhakika wa chakula katika baadhi ya maeneo.

Rosanne Marchesich kiongozi wa timu ya dharura na mnepo ya FAO anasema mlipuko wa safari hii wa nzige ni mkubwa sana, “Tunachojua kuhusu uvamizi huu wa nzige wa jangwani ni kwamba ni mbaya zaidi kuwahi kushuhudia Ethiopia na Somalia katika kipindi cha miaka 25 na ni mbaya zaidi kushudiwa Kenya kwa zaidi ya miaka 70."

Hata hivyo amesema kiwango cha nzige hao kinatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine lakini kwa sasa nchi zilizoathirika zaidi ni Ethiopia , Kenya na Somalia na nzige wameshasababisha athari kubwa , na hofu ni kwamba wanavyoendelea kuvamia sehemu zingine za nchi hizo athari hasa katika uhakika wa chakula zitakuwa kubwa zaidi, lakini pia katika kilimo, na maisha kwa wakulima na wafugaji.

FAO imetoa wito wa kuwa na kampeni ya pamoja kukabiliana na janga hilo la nzige ikihofia kwamba janga linaweza kusambaa kwa nchi zingine za Afrika Mashariki.“Kuna hatari ya kusambaa, nchi muhimu zaidi zinazoangaliwa hivi sasa ni Uganda na Sudan Kusini. Uganda haijawahi kukabiliana na wimbi la nzige tangu miaka ya 60, hivyo kuna wasiwasi kuhusu uwezo wa wataalam mashinani kuweza kukabiliana na janga hilo bila msaada toka nje. Na katika nchi kama Sudan Kusini tayari kuna asilimia 47 ya watu wasio na uhakika wa chakula.”

Ameongeza kuwa mbali ya zahma zingine zinazowakabili mabadiliko ya tabianchi yamekuwa kichocheo kikubwa cha nzige kuzaliana.

Pamoja na kufuatilia janga hili kwa karibu FAO inatoa msaada wa hatua za kuwadhibiti nzige hao kwa njia ya anga na ardhini lakini pia mbinu za kuweza kuwasaidia wakulima na wafugaji kuendesha maisha yao.

Pia imeonya kwamba mazingira ya kuruhusu kuzaliana bado yapo na ongezeko la nzige linaweza kuendelea hadi Juni mwaka huu 2020.

Umoja wa Mataifa waingilia kati

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura OCHA imesema imetoa dola milioni 10 kutoka katika mfuko wake mkuu wa dharura CERF ili kuongeza nguvu katika kupambana na mlipuko wa nzige wa Jangwani ambao wamevamia maeneo kadhaa ya Afrika Mashariki. Akizungumza leo na vyombo vya habari mjini Geneva Uswisi, Msemaji wa OCHA Jens Laerk amesema,“Ni mlipuko ambao uko Afrika Mashariki na pembe ya Afrika. Pia umebainika kusini magharibi mwa Asia na Bahari ya shamu, ni mlipuko mbaya wa aina yake katika miaka 25 kwa Ethiopia na Somalia na ni mbaya zaidi kwa Kenya kuwahi kuuona katika miaka 70. Madhara katika nchi hizo ni mabaya kwa kuwa malisho na mazao yanatoweka katika jamii ambazo tayari zilikuwa zinakabiliwa na upungufu wa chakula.”

View attachment 1336053
View attachment 1336081

















































Inaelekea hawa wadudu wanazaliana sana.

Hivi lifesapan yao ni muda gani?

NB:
Tanzania inabidi tujipange maana hili ni janga kama majanga mengine hivyo ni vizuri serikali ikaweka fungu na ikachukua hatua za tahadhari kupambana na hili janga.

Ni vizuri pia kuwasaidia wakenya kwa hali na mali, kwani wahanga walisema "Mwenzako akinjolewa, nawe tia maji"

Hatuwezi kuwa salama kama nyumba ya jirani inateketea kwa moto.
 
ningependa kufahamishwa nini kina sababisha Population Ya hao viumbe kuwa wengi kiasi hicho, Wanatokea wapi, Wanazaliana vipi mpaka wanakuwa wengi hivyo, Chanzo Chao ni wapi na ni nini ?
au ni lab 🧪 made/modified boosted

Naombeni msaada wajuvi
hawa wadudu huwa wapo,na katika hali ya kawaida huwa hawajikusanyi kwa makundi wala hawali sana
Ila inatokea hali fulani wanaanza kubadilika na kujikusanya kwenye kundi kubwa, na kula kwa fujo

Kinachochea mabadiliko haya kwa kifupi ni jinsi misimu ya mvua na ukame inavyopishana, hili lina maelezo mengi kidogo,
Hawa wadudu wapo tangia hata Yesu kristu hajazaliwa, nafikiri kwenye Biblia pia wameelezewa, kipindi hicho kulikuwa hakuna maabara za kutengeneza wadudu
 
Hivi hakuna dawa ya kupulizia hewani kuwaua hao wadudu kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mpaka saa Kenya ndege 9 ziko kazini kila siku zInanyunyizia dawa wanakufa lakini kila siku wanaingia wengine kwa mabilioni. Na eneo wanaloharibu linazidi kuongezeka shida ndio ipo hapo mkuu. Vita ya nzige sio ya kitoto.
 
Back
Top Bottom