Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Kufuatia tukio la mwanaume mmoja anaesemekana kuwa na mataizo ya akili kukata uume wake, ambapo toka tukio hilo limetokea mpaka baada ya matibabu waandishi wametoa taarifa zote juu ya hali yake, ikiwemo jina, umri, jinsia, makazi na ugonjwa wenyewe.
Wadau mbalimbali wamelalamikia kitendo cha Taarifa Binafsi za mgonjwa huyo kuanikwa mtandaoni kwa kukiuka Sheria na miongozo ya taaluma za afya ambapo Faragha ya mgonjwa inatakiwa kulindwa na kuheshimiwa, lakini pia inaenda kinyume na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo imeanza kutumika tangu Mei 1, 2023
Kwa mujibu wa Kifungu cha 25, Kifungu kidogo cha 2 cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kinaeleza jinsi uchakataji wa Taarifa Binafsi unavyotakiwa kufanywa endapo taarifa hizo zitatumiwa kwa madhumuni mengine tofauti na madhumuni yalilokusudiwa, ambapo kifungu kidogo 2 (d) kinasema mchakataji ataweza kutumia Taarifa Binafsi kwa matumizi mengine kwa namna ambayo muhusika hatambuliki.
Wachakati wa Taarifa Binafsi wanatakiwa kuelewa Sheria vizuri, na ndio maana Serikali inatakiwa kutoa kipindi cha mpito kwa taasisi, makampuni na watu binafsi wanaoathiriwa na Sheria hii kuelewa vizuri kabla ya matumizi rasmi kuanza.
Kutokana na madhara yanayoweza kutokea, Wadau walipendekeza Serikali itoe Kipindi cha Mpito kwa wote wanaoathiriwa na Sheria hii ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ili kuendana na mabadiliko yaliyokuja na sheria hii.