Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kuku wa kienyeji pure wanapatikana mahala pengi ila kwa msaada mzuri Cheki uzi Mbalimbali hapa jukwaani.
nashukuru Jana nimefanikiwa kuanza ufugaji,nimeanza na vifaranga 10 vya wiki 3.
kulea vifaranga wala si tatizo. kwahao kuku wako banda la bati 3 za mita 3 au 2.5 litakutosha. PM namba yako nikuelekeze cha kufanya dhidi ya vifaranga na kama utakuwa karibu na nilipo naweza kukutumia kitabu (bule) bila malipo nilicho toa SUA
Hongera sana Kuku wa Kabanga, Nakutakia kila la Kheri Ndugu. Sijui kwanini imekuwa ngumu kupata ramani ya mabanda ya kuku. Ila nitajitahidi nitafute wahusika ili wanielekeze.
sielewi mnaposema mnataka ramani mbona sample zipo umu nyingi tu. Mfano unaweza google chicken huts/house pia kwa kiswahili utapata local. Kuna uzi uliwekwa na picha hadi cost, ni wewe kuwa mbunifu ukitumia nafasi, vifaa ulivyonavyo na idadi na aina ya kuku. Hakuna formula maana kila mtu ni unique ingawa kuna vitu muhimu kama hewa, sakafu na paa lisilovuja vingine unajazia vyako
dah ulipotelea wapi best? Bunge la katiba? Maana naona ufugaji ulitupa kule hahaa. Sisi tupo bado tunapambana sasaivi nina Kenbro wa Reti wanakaribia kutaga. Karibu tena kundini. Kubota anazama na kuibuka mara chache sana sijui yuko wapi.
Nakumbuka uzi wa Kubota ni moa wapo ya nyuzi zilizo nivutia kanza ufugaji wa kuku.
Habari Mkuu!
Yaan leo hawa kuku nimeshindwa cha kuwafanya. Niliamka asubuhi sana kuenda kusafisha banda ile naingia Paaa... Hamad!! nakuta ndio wanaalizia yai nimeangalia banda Zima sijakuta hata masalia ya ute wa yai. Hapa ndipo nilipo pata jibu la Kwanini wiki hii sijapata mayai ya kutosha japokuwa kuna kuku wengine wawili wenye dalili kuwa wameanza kutaga.
Hapa najipanga kutengeneza chakula chenye choka ya kutosha tu, sijui kama itasaidia!
Kama kuna mbinu nyingine naombeni jamani maana wameniweza hawa viumbe wiki hii.Yaani mayai 8 kwa wiki!
Pole sana ni chokaa itakuwa pia madini ya chuma hivi, mi wangu huwa nawapa masaa kama matatu tu kila wiki wale nyasi. Nimepanda nyasi kibao kwa kweli sina mgogoro kabisa na ulaji wa mayai.
Sikia, inaonekana wakati unampa awalee alikuwa anakuona. Majuzi mie kuku wangu alitotoa vifaranga sita akaacha mayai nane. Mie nikamchekiii nikaona sio kesi. Nikamuweka kwenye kachumba kadogo nikaweka msosi na maji.
Yale mayai nane nikamuwekea mwingine alikuwa na mayai 16 na ambaye alikuwa analalia karibu muda sawa na huyu wa kwanza. Mungu akajaalia juzi huyu wa pili ambaye alikuwa na mayai 24 sasa akatotoa vifaranga sita. Nikavibeba vyote nikamfata yule wa kwanza nikamchapa na ufagio akakimbia nje nikaweka vifaranga sita puu. Nikamfata nje namtolea macho kwa hasira nikamkimbiza atokomee mbali ili vifaranga wamlilie apate mzuka na kweli nikawasha fegi navuta pafu moja ya pili mara na yeye kacharuka kaja mbio balaa nikawa nacheka tu. Karuka hadi kwenye kakibanda kake akawakumbatia vifaranga wake mie kikuu na njia nawahi bar.
Jana tena nikaenda kwa yule aliyebakiza mayai 18 sasa nikakuta katotoa vifaranga 7 nikabeba kama kawaida, mie siwabembelezi na wao washajua wakiniona na mfagio wanakuwa wapole sana. Nikamfata yule wa kwanza tena kama kawaida kala wa mgongo paa kaona atakufa kakimbia nje, nikaweka tena vifaranga halafu nikamsikilizia nikaona anakuja spidi mie nikaenda zangu kuvuta fegi. Sasa hivi nina vifaranga hao 19 na huyu wa pili ana mayai 11. Asubuhi wakati nawapa matikiti na dagaa nimeona yule wa kwanza anaishi kwa amani kabisa na wanae.
Kamwe usimpe kuku vifaranga akiwa anakuona ataua wote. Na pia kaza sura wajue muda wa kazi ni kazi.
Pangu Pakavu.
Mama Joe, Usiniambie umeachana na kuku wa kisasa! Nini tatizo/changamoto au faida ya chotara inazidi wale wa kisasa?
changamoto ya kuku ni chakula na soko. Wale kisasa wanakula sana na hivyo faida yao wawe wengi, sasa tena kuwa wengi kama soko niliko limekuwa sio zuri na hiyo kula yao ni risk. Pili ikitokea umepata hasara waweza anguka mtaji maana unaanza moja na vifaranga wa kununua. Chotara ni dual purpose kama soko sio zuri waweza subiri huku unauza mayai pia hawali sana kama broiler. Pia waweza totolesha mayai yako kupata batch mpya. Broiler ukikosa soko unahesabu hasara kwa siku
Shukran Mama Joe,
Nimekupata vizuri, Ngoja nikomae kidogo nikikaa sawa nitainvest kikamilifu tu.
mi nilianza kufuga mwezi wa tano mwaka huu nikiwa na majike 8 na jogoo 1. Kwa sasa nina kuku 63 na majike matatu wanalalia jumla ya mayai 38 natarajia kupata vifaranga vipya mwezi ujao mapema. Nina plan ya kufikisha kuku 200 by december. Eneo no dogo so nina plan ya kununua ekari 2 nipanue business. Siri ya kuwa na kuku wengi ni kuwanyang'anya vifaranga majike wanaototoa kwa pamoja na kuwatia jela siku mbili wakitoka huko ni msosi tu. Baada ya wiki 2 anaanza kazi tena.