Faraja: Matokeo Ya Ufugaji Wa Kuku


Duh jamaa we mkali sana mwee
 
Duh jamaa we mkali sana mwee

Ni kweli unajua mkuu nimekuja gundua siri ya mafanikio ni juhudi maarifa na nidhamu katika biashara. Wenzetu weupe wananidhamu sana ndo maana wanafanikiwa.

Muda mfupi hapa nimetoka bandani kuwapa dagaa na nimeona kabisa jike ametaga yai nne wakati hesabu yangu ni mayai matano hadi Leo. Unaweza kuona kwamba nahujumiwa maana nimewauliza wote hapa hom wanadai hawajui. Nimetoa onyo kali sana na hivi naenda kununua kufuli jipya.
 
mapolomoko..hata mie nilikua naomba..unitumie hiko kitabu...plz..
 
Eti ni sahihi kuwachanganya kuku wa umri tofauti,mfano wiki 3 na wa miezi mitatu kwenye banda moja?kama ni sahihi,wakati wa kuwapa chanjo ni lazima kuwatenganisha?
 

Mkuu Hiikitu ilinitokea na mimi, Siku mbili sijaokota yai nahesabu yangu ni yai sita kwa siku hizo mbili. ila niligundua I sababu ya kuleta kuku wengine, maana muda wote walikua ni kufukuzana na kupigana.

Siku ya tatu niasema nitumie njia yako ikwasindsha njaa mpka saa tatu na nusu. nilivyo wapa msosi jioni narudi kutoka kazin nakutana na mayai manne kumbe na jike moja nililo leta likataga.
 

mkuu ulipowachanganya hao kuku walikua wa umri tofauti?
 
Eti ni sahihi kuwachanganya kuku wa umri tofauti,mfano wiki 3 na wa miezi mitatu kwenye banda moja?kama ni sahihi,wakati wa kuwapa chanjo ni lazima kuwatenganisha?

sijaelewa banda moja unamaana hakuna partition? Nafikiri sio sawa, ukiweza watenge hata na wavu au ubao kwani hawa wakubwa wanakula tofauti pia wana kinga tayari.
 
Wakuu,mmoja Kati ya vifaranga vyangu ameumia bawa,kwa sasa limelegea,anaweza kupona?dawa gani nimpe?au nisubiri akikua nimfanye kitoweo?
 
Wakuu,mmoja Kati ya vifaranga vyangu ameumia bawa,kwa sasa limelegea,anaweza kupona?dawa gani nimpe?au nisubiri akikua nimfanye kitoweo?

Mkuu, Una uhakika kaumia au ni dalili za magonjwa (kushusha mabawa)?
Fafanua kidogo ili wadau wapate kukusaidia mkuu.
 
Nmeona jeraha kwenye bawa,nadhani ameumia wakati mtoto anamkimbiza kumwingiza bandani.
 
Nmeona jeraha kwenye bawa,nadhani ameumia wakati mtoto anamkimbiza kumwingiza bandani.

Sina ujuzi mkubwa na hilo tatizo mkuu, ngoja tusubir wadau kwa msaada zaidi. Ila itakuwa bora zaidi ukimtenga ili asisumbuliwe na wenzie. Maana wanatabia ya kudonoana wakiona damu.
 
Hongera sana Kuku wa Kabanga, Nakutakia kila la Kheri Ndugu. Sijui kwanini imekuwa ngumu kupata ramani ya mabanda ya kuku. Ila nitajitahidi nitafute wahusika ili wanielekeze.

Nimepata baadhi sijui kama yatakua msaada, ila kwa kuanzia unaweza pata picha general
 
Msaada wakuu, naweza kupata wapi vifaranga vya kuku wa kisasa (broilers & layers)? Bei yao ikoje/ni kiasi gani? Naishi Dar ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…