Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anatakiwa awe anastaafu leo kwa mujibu wa sheria. Ametumikia chini ya Kikwete tangu miezi michache tu baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Chini ya uongozi wake wa idara hii nyeti kabisa nchini ambayo haiko chini ya Katibu Mkuu Kiongozi mengi yametokea na kwa kiasi kikubwa mengi ya kufanya watu wakumbuke idara wakiwa na maswali mengi kichwani.
Tunaweza kuanza kuorodhesa mambo ambayo yameonesa ulegevu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika ulinzi wa taifa chini ya uongozi wa Rashid Othman na Zoka (ambaye naye legally amestaafu lakini "bado yupo"). Kuna viongozi kadhaa wa Idara wanaotakiwa kustaafu hivi sasa lakini wote bado "wapo" na kuna dalili kuwa RO anataka Rais amuongezee muda ili wamalize wote 2015.