Farewell RO....

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anatakiwa awe anastaafu leo kwa mujibu wa sheria. Ametumikia chini ya Kikwete tangu miezi michache tu baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Chini ya uongozi wake wa idara hii nyeti kabisa nchini ambayo haiko chini ya Katibu Mkuu Kiongozi mengi yametokea na kwa kiasi kikubwa mengi ya kufanya watu wakumbuke idara wakiwa na maswali mengi kichwani.

Tunaweza kuanza kuorodhesa mambo ambayo yameonesa ulegevu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika ulinzi wa taifa chini ya uongozi wa Rashid Othman na Zoka (ambaye naye legally amestaafu lakini "bado yupo"). Kuna viongozi kadhaa wa Idara wanaotakiwa kustaafu hivi sasa lakini wote bado "wapo" na kuna dalili kuwa RO anataka Rais amuongezee muda ili wamalize wote 2015.
 
Mhhhh! Haya hutokea bongo tu! Kwani wakati wanampa hiyo post hawakujua tastafu muda si muda? Haya bana gharama kwa walipa kodi hiyo...
 
Habari Mzee Mwanakijiji,kabla ya kuanza kujadili madudu yaliyojiri chini ya uongozi wa RO.tafadhali tuangalie hili swala la kuongezea muda wa staafu au wanaostahili kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Naamini chini yao huwa na watu wengi tu wenye uwezo kuendesha taasisi hizo au ofisi za umma,ila toka ndugu yetu ameukwaa uraisi hii ndio imekuwa style ya watu kung'ang'ania maofisini.Tatizo liko wapi au ni nini?
 
Zaidi ya nusu ya wafanyakazi walio kwenye serikali ya JK umri wa kustaafu umepita kitambo",
na mheshimiwa RO sidhani kama anaweza kuondoka kwani kwa aliyoyaongoza kufanyika kwenye
awamu hii,lazima mkuu atamuongezea muda wamalize pamoja"

Kuna issue kama za akina Mulungi bado ziko pending"
 
Mzee Mwanakijiji,
Humo serikalini na taasisi zake za umma watu wenye nyadhifa kubwa hawataki kustaafu kabisa kama Robert Mugabe! Umezuka mtindo wa kupeana mikataba hadi inakera na kukatisha tamaa vijana wasomi tulionao kwa sasa.
 
Utaratibu wa uongozi kwa nchi yetu ni tatizo,viongozi hawasukumwi na dhamira za kutumikia umma na baada ya muda kuisha wangekuwa wanaona ufahari kustaafu.Kwetu kutumikia umma ni starehe ni kuwa peponi hivyo inakuwa ngumu viongozi kuliacha pepo walilonalo la uongozi wa umma.MENTALLY BADO TUKO NYUMA SANAAA.
 
Udhaifu wa serikali ya msafiri pamoja na yeye,hao wote ni fadhira ya mtandao ndo sababu anaogopa kuwawajibisha,aibu!idara ya usalama wa taifa imechezewa kama genge la vibaka,ro apishe wengine
 
Sijui kama KATIBA MPYA itatuokoa katika hili. Kenya wameweza. Kila nafasi inatangazwa na watu wanadahiliwa kwa uwazi kabisa.
 
kwanza niulize imekuaje amekaa muda wote bila kufukuzwa...that organisation is the most corrupt kuliko wakati mwingine wowote, watu wengi wamekufa au kupoteza mali zao bila hatia watu kutoka nchi zingine wanapitishwa kwenye hii nchi na wao wamekaa kimya..wanyama wanapitishwa airport (KIA) wanapelekwa uarabuni yeye kafumba macho...how did he manage to last this long?
 
La kwanza na kubwa kuliko yote kwangu ni ndege ya kijeshi kutoka falme za kiarabu, kuja na kupita kwenye raddar iliyonunuliwa kwa fedha za kufuru kwa kisingizio cha ulinzi na usalama, kisha dege hilo likatua pale KIA (UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA KILIMANJARO) , kisha dege hlo likabeba mamia ya wanyama pori wetu ambao ni alama ya utajiri wa taifa na urithi wa dunia.
Kisha dege hlo likaondoka na mpaka sasa haieleweki ni kipi kilifanywa au kimefanywa na hyo idara ya Bw RO, katika kurejesha hazina yetu iliyoibiwa na kuwawajibisha wote waliohusika.
Kwenye tukio hili ndio nilikubali kuwa TANZANIA NI TAIFA LA MAJUHA......
 
Kwa mawazo yangu mambo mawili yanatishia uhai wa taifa letu

(1) muungano, kuna matukio/matendo ya watu ambayo yalipaswa kuonekana mapema na chombo hiki na hatua stahiki kuvhukuliwa;
(2) udini: matendo ya uchochezi ya waziwazi ambayo yalitedeka au yanaendelea kutendeka na inaonekana 'hayaonwi' na chombo hiki muhimu ambayo yanachochea mgawanyiko wa kidini.
 
CHUNGA SANA HAWA WATU.... Hawajamalizia kazi waliyopangiwa kuifanya... mulizeni Mwakyembe anajua kazi waliyopangiwa hawajakamilisha.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…