Farhan Jr kauliza kwanini elimu ya sasa imepungua mvuto? Majibu aliyo pewa, wanaosomesha English Mediums hawatayafurahia👇

Hizo shule zako zimekudumaza sana ubongo.....
 
Hivi ukimchukuwa profesa aliyekulia na kusomea Lukuledi huko atamshinda mwingereza aliyesoma elementary education tu kwenye mambo ya kileo kama matumizi ya simu, kudafiri kwa ndege n.k? Exposure inapatika kwa kuwa exposed kwenye ulimwengu tofauti tofauti na ule uliozaliwa na siyo darasa lililo kijiji ulichozaliwa. Exposure is a broader concept encompassing the diverse range of experiences one encounters, while education specifically refers to the intentional and systematic acquisition of knowledge and skills. Upo?
 
Una point ya msingi. Mwenye kusikia na kuelewa akuelewe
 
Mwingine huyu hapa 👇
Hivi huwa mnakosa vitu vya kuanzishia thread!?...

Mwisho wa siku utakuletea Uzi wa huyo mwanaume Wako!... kihamu sijui kifamu... jinsi alivyomshughulikia mke wake usiku!!!!.

Siku hizi Jf....Tuna vijana Wahovyo! Sana humu!
 
Elimu haijapoteza mvuto, mambo yamebadilika na watu wenye elimu wamekuwa wengi sana na hakuna waajiri wa kuweza kuajiri wasomi wote. Hiyo hali imepelekea wasomi wengi kupata msongo wa mawazo na kudharau elimu zao, pia elimu zao kuonekana hazina faida kwao na kwa jamii zao kwakuwa hazijawasaidia kujitoa kwenye umasikini (hii ni kwa wale wanaoitazama elimu kama chanzo cha kipato)

Ni kawaida pale kitu kinapoongezeka kwenye jamii kuzidi uhitaji wake huwa kinaanza kuonekana cha kawaida sana.

Ushauri wangu; kutokana na mazingira ya sasa, mzazi kama una uwezo msomeshe mtoto wako mpaka kidato cha nne na ukiona amepata kijitambua na uwezo wake ni wa kawaida sana kwenye masomo, mpe mtaji au hakikisha anapata ujuzi wowote ambao utamsaidia kuanza kupata kipato kwa kujitegemea. Elimu haina mwisho!
 

Hiyo sio elimu mkuu. Ni vyeti vinavyo thibitisha uwezo wa kukariri wa mtu. Elimu ni ufunguo. Ina mpa mtu uwezo wa kufungua sehemu zilizo fungwa. Ajira ni suala lililo fungwa. Elimu inatakiwa kumpa msomi husika uwezo wa kufungua eneo hilo lililo fungwa kwa kuja na majibu ya swali hilo ambalo dunia ina muuliza. Sasa kama mtu anasoma elimu ambayo haimpi uwezo wa kupata suluhisho la tatizo la ukosefu wa ajira kwanini upoteze mamilioni yako kumlipia mtoto wako kwenye shule ambayo elimu yake haimpi uwezo wa kutatua hili tatizo?

Kwanini usimsomeshe tu kwenye shule za kawaida kwa usimamizi wa karibu halafu hayo mamilioni uka invest kwenye miundombinu ya kumtafutia maarifa yatakayo mpa uwezo wa kufungua sehemu zilizo kufunga?
Joannah
 
Yaani wewe bado mawazo wako yametawaliwa na "ELIIIIIIMUUUUUU NI UFUNGUO WA MAISHA,SHIKAMOOOOOOO MWALIMU"
 
Umeeleza vema Sana mkuu
 
Kwenye hiyo paragraph yako ya mwisho unataka mwanangu akashindwe kufanya presentation huko kwenye ma international exhibition si ndio?ndio lengo lako nakuuliza?
We niambie hivi "J unapomsomesha mtoto wako,viende sambamba na kumuandalia miundombinu atakayo simamia baadae'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…