Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Faris Buruhani, amewataka watu wanaowapa wananchi taarifa zinazoweza kuwachochea kumchukia Rais Samia Suluhu Hassan kuacha kufanya hivyo, akisema juhudi zilizofanywa na Serikali katika sekta mbalimbali zinapaswa kutambuliwa.
Akizungumza Oktoba 31, 2026, wakati wa mapokezi yake mkoani Kagera, Buruhani amesema Serikali imefanya kazi kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kijamii, ikiwemo madarasa, zahanati na vituo vya afya, lakini badala ya wananchi kutambua mafanikio hayo, kuna watu wanaodaiwa kumchonganisha Rais na wananchi.
Amesema viongozi waliopewa dhamana katika taasisi za umma wanapaswa kutambua kuwa nafasi hizo ni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi, na si kutumia madaraka yao kuzuia utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
Katika kauli yake, Buruhani alitoa onyo kwa watu anaodai wanajaribu kudhoofisha uungwaji mkono wa Rais Samia na CCM, akisema chama hicho hakitakubali juhudi za Serikali na maslahi yake kuathiriwa na vitendo vya mtu mmoja.
Soma Pia: Buruani: CHADEMA kila wakizunguka wanataka Katiba Mpya, Kuna mwananchi anakula Katiba hapa?
“Kwa kazi hii aliyofanya Rais Samia, unayejiandaa kumzamisha Rais Samia tutakuzamisha wewe kabla Rais Samia hajazama. Tutakuchukua kama samaki anavyochukuliwa na ndoano baharini. Hatuwezi kukubali Rais wetu na chama chetu kizamishwe kisa mtu mmoja,” amesema Buruhani.