'Farouk Tech' inawafaa wengi hapa nchini kukomesha wizi: Mwizi akutwa amelala ndani ya gari

'Farouk Tech' inawafaa wengi hapa nchini kukomesha wizi: Mwizi akutwa amelala ndani ya gari

Tungepata na namba za aliyenusurika kuibiwa ingependeza sana.

Tujue alifanyeje, huku tunaibiwa adi tumechakaa
 
NI kutokea visiwani Zanzibar ambapo kumetokea kisa cha Mwizi kusinzia eneo la tukio baada ya kufika nyumbani kufanya uhalifu, itazame hii video hapa ujionee nilichokuandalia ufahamu zaidi mkasa huo.
Kwa heshima na taadhima naomba mamba ya alieibiwa.
 
Sasa hiyo ni kwa gari tu,jaribu kwa mkewe uone cha moto...
 
Jeshi la polisi lifikirie namna ya kumtumia huyu mwandishi na benchi lake lote la ufundi kwa kile kilichotokea nyumbani kwake Juzi tena Ikibidi lianzishe jukwaa ama kitengo mbadala cha kupambana na uhalifu kwa kutumia mbinu za kienyeji ikiwezekana kila mkoa kuwe na vikosi hivi tunaweza jikuta kama nchi tumepunguza sana tatizo la wizi na ujambazi hivyo kupelekea kuokoa mali na roho za watu wengi mno.

Na hili likifanikiwa huenda hata mataifa mengine watakuja kuomba huduma hizo ambapo taifa litaingiza fedha za kigeni kupitia tozo mbali mbali.

Jeshi la polisi hii ni fursa kubwa kwenu muitumie ni kama tiba mbadala ya nyungu katika mapambano ya Covid 19 kwani lengo au kusudio ni lile lile la usalama wa raia na mali zetu hakika itawarahisishia sana kazi zenu maana wahalifu wengi mtawatia mikononi bila hata jasho mithili ya samaki nyavuni.
 
Inaweza ikawa ni Mbinu ya kujizolea Umaarufu kipindi hiki cha Uchaguzi.Tulioyaona wa Mlandizi aliyejifanya hawezi kutua mahindi, pia tukaona Iringa aliyejifanya kaanguka na Ungo
 
Usingizi wa pono.. Manyoya ya fisi yamehusika hapo

Jr[emoji769]


We ni mtu wa pili kuhusisha fisi katika suala hili. Umetofautiana kidogo na jamaa wa kwanza....yeye ali-suggest kuwa ni mavi ya fisi yaliyochanganywa na shahawa yake pamoja na dawa za kienyeji.
 
Back
Top Bottom