Jeshi la polisi lifikirie namna ya kumtumia huyu mwandishi na benchi lake lote la ufundi kwa kile kilichotokea nyumbani kwake Juzi tena Ikibidi lianzishe jukwaa ama kitengo mbadala cha kupambana na uhalifu kwa kutumia mbinu za kienyeji ikiwezekana kila mkoa kuwe na vikosi hivi tunaweza jikuta kama nchi tumepunguza sana tatizo la wizi na ujambazi hivyo kupelekea kuokoa mali na roho za watu wengi mno.
Na hili likifanikiwa huenda hata mataifa mengine watakuja kuomba huduma hizo ambapo taifa litaingiza fedha za kigeni kupitia tozo mbali mbali.
Jeshi la polisi hii ni fursa kubwa kwenu muitumie ni kama tiba mbadala ya nyungu katika mapambano ya Covid 19 kwani lengo au kusudio ni lile lile la usalama wa raia na mali zetu hakika itawarahisishia sana kazi zenu maana wahalifu wengi mtawatia mikononi bila hata jasho mithili ya samaki nyavuni.