Fastjet hawapo poa

new generation

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
817
Reaction score
1,687
Wadau,

Nimefika Airport hapa Mwalimu Julius, ilikua dakika 40 before boarding.But huwezi amini nimekataliwa kupanda ndege, naambiwa nimechelewa na kufanya re-schedule hawa jamaa wapo very expensive.

Dah sina hamu safari yangu ya Mwanza imebidi ni cancel.
 
Pole saana cheap things do cost....cku hz wako expensive saana
 

Pole sana. ni washenzi sana sijui tuwashitaki wapi vile. Mamlaka gani inahusika na usafiri wa anga. dakika 40 muda ulikuwa bado. nadhani ni dili za wakata tiketi kuweka watu wao.
 
Pole sana. ni washenzi sana sijui tuwashitaki wapi vile. Mamlaka gani inahusika na usafiri wa anga. dakika 40 muda ulikuwa bado. nadhani ni dili za wakata tiketi kuweka watu wao.

Hawa watu wa check-in nimekomaa nao kinoma na nilikua na washikaji wengne, yaan. Du. Ku-reschedule naambiwa laki 2, nimeshangaa sana....
 
Km huna mizigo na ni local hio haihitaj passport/ documentation
dk 40 nyingi sana,hawajawa waungwana

Utakaaje airport masaa 2 kwa local route
 
Hata Precisionair nao walianza hivi hivi na unaweza mambo yao yalivyo kwa sasa! Local flight kumrudisha mtu nyumbani tena kwa gharama ya laki mbili si ni afadhali upande basi tu !
 

aaah nawewe kama ungewai haya yasingekukuta, wewe hili jiji walijua halafu unatoka posta nusu saa kabla ndege kuondoka, dah lzm ile kwako mzee
 
aaah nawewe kama ungewai haya yasingekukuta, wewe hili jiji walijua halafu unatoka posta nusu saa kabla ndege kuondoka, dah lzm ile kwako mzee

Nimekata nyingne ya kesho asubuh but hawa jamaa dah...
 
Pole mkuu lakini wameandika kwenye tiketi yao kwamba 40 min before your flight utakua umechelewa
 

Mkuu kawaida ni 45 minutes before departure... au ndo mara yako kusafiri? ndio maana wanasema 2hr reporting time for domestic flight na 3hrs for international flight angalia kwenye terms and conditions..... ujue pia muda wa kustukiza kiusalama hawaruhusiwi...i guess muda huu hutumia kufanya feting.... next time be ontime... ukienda nje na style kama hii utalia
 
aaah nawewe kama ungewai haya yasingekukuta, wewe hili jiji walijua halafu unatoka posta nusu saa kabla ndege kuondoka, dah lzm ile kwako mzee

Sio suala la kuwahi wala nini hawa fast jet ni wapuuzi tu. Wao wanakwambia ufike 40 minutes kabla ya safari lakini hii kitu hawaifuati. Ukifika kwa muda huo unakuta hata counter wameishafunga. Yalinipata Arusha haya ya fastjet some two years back nikitoka KIA kurudi Dar na tangia siku hiyo sitaki kusikia kitu kinaitwa fast jet, wapuuzi sana.

Tiba
 

Hupaswi kuwalaumu FastJet kama ulisoma ticket yako wamendika kabisa mwisho wa ku-check in ni dakika 40 kabla ya ku-board
 
Pole mkuu lakini wameandika kwenye tiketi yao kwamba 40 min before your flight utakua umechelewa

Nakumbuka hata precision air nao wana huu utaratibu kuwa zikibaki 40 min.kabla ya muda wa kuondoka ndege huruhusiwi kusafiri.
 
Pole sana mkuu.Ni kweli fastjet wako strict kama mashirika yote ya kimataifa katika usafiri wa anga.Hii inatokea sana kama hukuzingatia terms walizokuandikia kwenye ticket yako. Check-in kwenye counter yao pale ndani inaanza masaa mawili kabla ya muda wa kuruka ndege husika.Departure gate inafunguliwa dakika 40 kabla ya kuruka ndege.Cha kuzingatia hapa ni kuwa kwenye departure gate katika muda unaotosha kabisa ie 40min kabla ya take off,Hivyo ndivyo ilivyo kokote duniani,na zaidi sana kwa kufuata masharti waliokuwekea kwenye ticket.Unapochelewa huwa hakuna huruma katika biashara kama tufanyavyo hapa Bongo, Wanakukaribisha kununua ticket nyingine kwa bei mbaya zaidi kwa gharama zako za ziada.
 
Si mara ya kwanza kusafiri... Ingawa kwa precision wana utaratibu poa, maana wao kabla ya ndege kuondoka huwa wanatangaza jina la abiria aliyechelewa, wanatangaza hata mara tatu kwa interval fulan, then ndo wanasepa.. But kwa fast jet du...re-schedule yao tu ndo huwa inachosha.. Bt dah shida sana huu mji. Ukiwa na gari binafsi tabu, daladala ndo usiseme. Bora pikipiki ya boxer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…