Fastjet PLC inatarajia kuuza hisa zake katika shirika la Fastjet Tanzania

Fastjet PLC inatarajia kuuza hisa zake katika shirika la Fastjet Tanzania

ukiona mwenzio tena mkwengwe kwenye soko anakimbia unapaswa uwe makini maradufu, nadhani n fursa kwa ATCL ila nawa wawe makini sokoni kugumu kwelikweli
 
Shirika la Ndege la Fastjet linatarajia kuondoka katika soko la Tanzania, baada ya kujiendesha kwa hasara kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo ushindani kutoka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), changamoto za kisheria, na uwezo wake wa kukusanya fedha.

Kampuni ya Fastjet Plc iliyoorodheshwa katika soko la hisa la London, nchini Uingereza inatarajia kuuza hisa zake asilimia 49 katika Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania kutokana na changamoto kubwa za kibiashara.

Kuondoka kwa Fastjet Plc ndani ya Fastjet Tanzania kutaliacha shirika hilo (Fastjet Tanzania) na uwezo mdogo wa kushindana na ATCL, ambayo imeanza kwa kasi kufufua upya shirika hilo.

Fastjet imeeleza kuwa, changamoto za mazingira ya kufanyia biashara na ushindani wa ATCL ndio changamoto kubwa ambazo mmiliki mpya atakabiliana nazo katika kuhakikisha shirika hilo linatengeneza faida. Baada ya serikali kununua ndege nne mpya, imeongeza ushindani mkubwa kwa Fastjet kwani imekuwa ikifanya safari katika maeneo Fastjet ilikuwa ikifanya, na hivyo kupunguza wateja.

Fastjet imeeleza kuwa imekuwa ikipata changamoto kubwa katika safari za Dar es Salaam-Mwanza na Dar es Salam-Kilimanjaro baada ya ATCL kuanza kutumia ndege yake mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo ina uwezo wa kubeba abiria 262.

Changamoto za kisheria ambazo shirika hilo limeeleza kukumbana nazo ni pamoja na kuchukua muda mrefu kwa ndege zake mpya tatu aina ya ATR72-600 kuruhusiwa kuanza kufanya kazi. Hatua hiyo inafanya wazidi kuingia gharama za kutunza ndege hizo wakati hazifanyi kazi.

“Hakuna dalili changamoto hizi zitamalizika lini. Kulikuwa na changamoto za uingizwaji wa ndege mpya za ATR72-600, pamoja na kibali cha safari za ndani kwa ajili ya ATR72-600 na ERJ190 ambacho kwa miezi kadhaa sasa bado hakijapatikana, na hii imeathiri kwa kiasi kikubwa ukuaji wa kampuni.”

Aidha, Fastjet imesema kuwa itakodisha ndege hizo, kuliko kufanyia biashara katika anga la Tanzania.
Kuanzia Januari hadi Juni 2018, Fastjet ilisafirisha abiria 201,000 ambapo safari kati ya Dar es Salaam na Mwanza, ndizo zilikuwa na abiria wengine zaidi.

Lakini idadi hiyo ya abiria ilipungua kwa asilimia 9, kutokana na kubadilishwa ndege ya safari kutoka Airbus A319 yenye uwezo wa kubeba abiria 144 na kutumia Embraer190s yenye uwezo wa kubeba abiria 104.

Swahili Times
Urasimu usio na maana ndiyo unaodhoofisha uwekezaji Tanzania. Kuna Wenye mamlaka katika Kutoa vibali and so forth ambao very possible wanafanya haya kwa makusudi Au kwa maelekezo ili kudhoofisha hili shirika.
 
Huyu fastjet bhana anachekesha kweli kwan lazima awekeze tz duh aende hata huko Ben congo DRC
 
Habari wadau!

Katika hali ya kuhuzunisha na kuondoa hali ya ushindani nchini wa usafiri wa anga. Shirika la ndege la fast jet limeanza kufunga virago Tanzania kwa mazingira magumu ya uwekezaji na serikali kuwanyima vibali vya baadhi ya rout na kuwanyima kibali cha kuingiza ndege mpya nchini.

Mkurugenzi wa shirika hilo kathibitisha kufunga virago kwa kushindwa kuwa na mazingira rafiki ya uwekezaji na kutotoa uwanja mpana wa ushindani
 
mkomoe mtoto wa jirani na mpendelee mtoto wako.

hii nchi imekuwa ngumu sana kwa wafanyabiashara.
Hawa hata wakibaki wenyewe wataishia kushindwa tu.

Sasa tunakwenda kukosa hata hiyo kodi waliokuwa wanalipa serikalini, hela (charges) walizokuwa wanalipa TAA na TCAA,n.k na pia watu wanakwenda kupoteza ajira na hivyo PAYE ya staff wao nayo tunaikosa pia.
 
Habari wadau!

Katika hali ya kuhuzunisha na kuondoa hali ya ushindani nchini wa usafiri wa anga. Shirika la ndege la fast jet limeanza kufunga virago Tanzania kwa mazingira magumu ya uwekezaji na serikali kuwanyima vibali vya baadhi ya rout na kuwanyima kibali cha kuingiza ndege mpya nchini.

Mkurugenzi wa shirika hilo kathibitisha kufunga virago kwa kushindwa kuwa na mazingira rafiki ya uwekezaji na kutotoa uwanja mpana wa ushindani
Kwa taarifa yako Fastjet walikuwa wababaishaji ila basi tu tulikuwa hatunajinsi ya kufanya kwa kuwa walikuwa hawana mshindani na nilishawaambie likija shirika la ndege jingine wajitayarishe kwa maumivu. Angalia Server zao ziko UK na hakuna admin TZ baada ya kuona sasa wanabanwa na sheria ya .co.tz wamekimbilia Msumbiji lakini wanajifanya wako TZ ofisi zao za TZ hazina maamuzi kabisa just operators.
 
It is not science rocket to know that 'CHARITY BEGINS AT HOME" JAPOKUWA UNATIMIZA WAJIBU WA CONTRACT YAKO, LAKINI KUNA KAZI NYINGI NI AIBU KUFANYA, HASA ZA KUWADI
Ni ukuwadi au maneno ya kweli..
 
It is not science rocket to know that 'CHARITY BEGINS AT HOME" JAPOKUWA UNATIMIZA WAJIBU WA CONTRACT YAKO, LAKINI KUNA KAZI NYINGI NI AIBU KUFANYA, HASA ZA KUWADI
Kweli kabisa aisee kazi ya kusifia jiwe kila uchao huku wengi wetu tukishindwa kumkosoa tunapokuwa na uhakika kuwa anastahili kukosolewa ni unafiki kama si ulimbukeni uliokithiri. Hakuna mbeleko ya kuibeba ATCL kimataifa!
 
Back
Top Bottom