Father Dkt. Kitima: Tunakubaliana na Rais Magufuli kwamba tumuombe Mungu na tuchukue tahadhari za kisayansi dhidi ya Covid 19

Father Dkt. Kitima: Tunakubaliana na Rais Magufuli kwamba tumuombe Mungu na tuchukue tahadhari za kisayansi dhidi ya Covid 19

Yaani Padre anaongea kama ndiye Mwenye Nchi vile! Halafu huyo Mwenye nchi mwenyewe ndiyo kwanza anaongea kama Padre!! Kazi kweli kweli.
Hii ndo hali halisi mkuu.
IMG-20210220-WA0014.jpg
 
Nani ambae haamini km huo ugonjwa upo?, huyo asie amini ameshikilia afya yako?!, wewe huyo asie amini ni mmeo kwamba mko nae kitanda kimoja,.?.ukijikinga wewe atapona yeye?, AU asipojikinga yeye utakufa wewe,usiwe mjinga na mpumbavu,fanya kile unachoona kinakufaa
Acha mawazo mfu, ugonjwa huu anaweza kukuletea mtoto wako kutoka huko shuleni alipochangamana na watoto wenzie kutoka familia zisizojilinda.

Vita ya Taifa zima haiwezi kupiganwa kwa mafanikio kama hakuna jitihada ya pamoja. Sasa uadhani nani ana power na resources za kucoordinate jitihada hizo zaidi ya serikali?
 
Akizungumza katika misa ya mazishi ya Balozi Kijazi Katibu wa TEC father Kitima amesema wanakubaliana na tamko la Rais Magufuli kwamba wananchi wamwombe Mungu bila kuacha kuchukua tahadhari za kisayansi dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Father Kitima amesema ni vema wananchi wakachukua tahadhari zote za kisayansi dhidi ya ugonjwa wa Corona huku wakimtanguliza Mungu mbele.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!

Dk. Charles Kitima ni padre na mwalimu wa sheria na Katiba aliye na elimu ya uzamivu.

Akisema kuwa "ni vema wananchi wakachukua tahadhari zote za kisayansi dhidi ya ugonjwa wa Corona huku wakimtanguliza Mungu mbele" ni sawa. Anacho kibali cha kikatiba cha kuyasema hayo.

Lakini kauli yake kwamba wao "wanakubaliana na tamko la Rais Magufuli kwamba wananchi wamwombe Mungu bila kuacha kuchukua tahadhari za kisayansi dhidi ya ugonjwa wa Corona" inayo dosari kubwa kisheria.

Rais wa nchi ambayo inaongozwa na Katibu isiyofungamana na dini yoyote hana kibali cha kikatiba cha kumruhusu kutoa tamko kwamba "wananchi wamwombe Mungu."

Kwa kauli hii Rais anakuwa anavunja Katiba ya nchi. Na kina Kitima wakisema kuwa "wanakubaliana na tamko la Rais" wanakuwa wanakubaliana na uvunjaji wa Katiba ya nchi.

Kwa hiyo, Dk. Charles Kitima anataka tuamini kuwa sasa Kanisa Katoliki limeachana na tabia yake ya kuheshimu Katiba ya nchi?

Ni swali la udadisi tu.
 
Dk. Charles Kitima ni padre na mwalimu wa sheria na Katiba aliye elimu ya uzamivu.

Akisema kuwa "ni vema wananchi wakachukua tahadhari zote za kisayansi dhidi ya ugonjwa wa Corona huku wakimtanguliza Mungu mbele" ni sawa. Anacho kibali cha kuyasema hayo.

Lakini kauli yake kwamba "wanakubaliana na tamko la Rais Magufuli kwamba wananchi wamwombe Mungu bila kuacha kuchukua tahadhari za kisayansi dhidi ya ugonjwa wa Corona" inayo dosari kubwa.

Rais wa nchi ambayo inaongozwa na Katibu isiyofungamana na dini yoyote hana kibali cha kikatiba cha kumruhusu kutoa tamko kwamba "wananchi wamwombe Mungu."

Kwa kauli hii Rais anakuwa anavunja Katiba ya nchi. Na kina Kitima wakisema kuwa "wanakubaliana na tamko la Rais" wanakuwa wanakubaliana na uvunjaji wa Katiba ya nchi.

Kwa hiyo, Dk. Charles Kitima anataka tuamini kuwa sasa Kanisa Katoliki limeachana na tabia yake ya kuheshimu Katiba ya nchi?

Ni swali la udadisi tu.

Kama kina
Mungu hana dini binadamu ndio wenye dini.

Tunaimba katika wimbo wa taifa " Mungu ibariki Tanzania "

" Mungu wabariki viongozi wetu"
 
Mungu hana dini binadamu ndio wenye dini.

Tunaimba katika wimbo wa taifa " Mungu ibariki Tanzania "

" Mungu wabariki viongozi wetu"

Maswali matatu:

1. Mungu yupi asiye na dini? Yehova? Allah? Luhanga? Ng'ombe wa Wahindi?

2. Wimbo wa Taifa ni sehemu ya Katiba na sheria za nchi?

3. Maneno MUNGU, SALA, MAOMBI, MAOMBEZI, MISA na IBADA ni misamiati ya kiserikali hapa Tanzania?
 
Huu ugonjwa ni communicable desease, maana yake ni ugonjwa unaoambukizwa kwa haraka kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Wewe mwenyewe ukijikinga halafu watu wengine hawajajikinga haikusaidiii maana hili gonjwa kupamabana nalo inahitaji ushirikiano kwa jamii nzima.

Sasa ikiwa kwenye jamii kuna wengine hawaamini kama huo ugonjwa upo na mbaya zaidi wameaminishwa na kiongozi wa nchi unategemea hata wewe ukichukua hatua mwenyewe itasaidia nini?
Kosa kubwa lililofanywa na utawala ni kushindwa kutoa tamko kitaifa la kurudi kwa corona wakiamini watu wata hofu. Watu wengi wanajua, lakini pia kuna kundi la watu wengi zaidi (mbumbumbu) ambao bila kusikia kiongozi katamka, hawaamini. Nao ndio wapokea na wasambazaji wakubwa. Ndio wanao sombwa kwenye malori kufikisha nyomi ya mikutano ya waheshimiwa.
 
Kama TAG wameshatupa tuzo ya kuishinda corona kupitia maombi matamko ya nini tena
Uelewa wetu ndio kikomo hapo. Watashindwaje kutoa tuzo ilhali juzi ndugu zao wametoka kwa sangoma na maiti ya mwenzao aliekufa kwa kushindwa 'kupumua' na sangoma akawambia alikabwa na jini?
 
Back
Top Bottom