Fatilia mwanzo wa ndoto yangu ya kumiliki shule

Eberhard

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
1,153
Reaction score
809
Nilianza ndoto yangu ya kumiliki shule nikiwa nimeuanza mwaka wa tatu wa masomo yangu ya degree. Wakati huo niliapply kazi ya KUFUNDISHA katika shule moja ya English medium. ELIMU ya mkuu wa shule ilikuwa ni certificate level. Kwa kuwa Mimi nilikuwa na diploma ya ualimu nilipewa majukumu ya kumshauri mkuu wa shule pamoja mkurugenzi wa shule na msimamamizi wa usajili wa walimu wapya pamoja na mkakuzi wa kazi zao. Hakuna mwalimu aliyepata ajili bila Mimi kumuandikia taarifa mwajili kuwa mwalimu huyu ameshinda vipimo alivyopewa. Kimsingi kila kitu katika shule ile kilinihitaji na kunitegemea.

Mamlaka niliyopewa ya uamuzi wa mambo mengi na kupitishwa kwa kila kitu nilichosuggest kwa mmiliki wa shule ilinipa moyo wa ujasiri sana. Kutokana na kibarua changu mmiliki wa shule alinipa mshahara mkubwa kushinda mwalimu mwingine yeyote yule. Hata mkuu wa shule nilimshinda kwa mshahara Hapa nikaanza kujiuliza ikiwa mimi ndiyo mshahuri wa karibia kila kitu kihususho utaalamu wa uendeshaji wa shule , Je siwezi na Mimi nikafikiria kuanzisha shule yangu?

Baada ya kufikiria sana nikaona ni lazima Mimi niwe mmiliki wa shule. So kuanzia hapo Mimi nikaanza kujiona kuwa ni mmiliki wa shule kubwa isiyoonekana kwa macho. Kimsingi mimi huwa sianzi kwa kutafutapesa kisha wazo bali naanza na wao kisha nafikiria pesa. Hivyo nikaanza kutafuta jina la shule nikaona iitwe EXODUS. Neno langu la kusimamia katika kitabu hicho ni KUTOKA 3.8 ambacho kinasema "nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi". Hapo nilikuwa nafikilria kuwa shule nitakayoijenga iwe miongoni mwa shule bora katika jamii nitokayo ambayo itakuwa kimbilio la watoto wa masikini ambao wamekuwa wakidanganywa siku zote na walala Hai walioko serikalini kuwa Kiswahil ni lugha ya taifa lakini walala hai wenyewe hawawapeleki watoto wao kwenye shule zinazofundisha ELIMU ya msingi kwa lugha ya Kiswahili hivyo kuwanyima watoto wa masikini fursa lukuki, Katika ulimwengu huu ambaodunia yote tunaishi kama tupo kwenye kijiji kimoja. Kimbilio la watoto walao mlo mmoja. Kimbilio la watu wasiowaza maisha bora na wakitoka wawe kama wametoka kwenye nchi ijaayo maziwa na asali. So ni kuiondoa jamii masikini kwenye nchi ya ya utume anti misri na kipeleka kwenye nchi ijaayo maziwa na asari. ELIMU na mazingira watakayoyakuta shuleni yatawafanya wakitoka hapa wawe na mwendelezo wa kuyatafuta maisha bora kama vile kuishi kwenye nchi ijaayo maziwa na asari. Hivyo ninalenga kuibadili jamii yangu kifikra, kijamii na kiuchumi kuelekea standard life. Naam maisha ya kumjua Mungu pia.

simulizi yangu ya safari yangu ya kumiliki shule itaendelea kesho. Nahaidi kuwawekea picha za jengo langu la shule. Safari ni hatua wakuu.
 
".... And, as we let our own light shine, we consciously give other people permission to do the same.
As we are liberated from our fear, our presence automatically liberates others."
~ M. Williason.
 
Nilianza ndoto yangu ya kumiliki shule nikiwa nimeuanza mwaka wa tatu wa masomo yangu ya degree. Wakati huo niliapply kazi ya KUFUNDISHA katika shule moja ya English medium. ELIMU ya mkuu wa shule ilikuwa ni certificate level. Kwa kuwa Mimi nilikuwa na diploma ya ualimu nilipewa majukumu ya kumshauri mkuu wa shule pamoja mkurugenzi wa shule na msimamamizi wa usajili wa walimu wapya pamoja na mkakuzi wa kazi zao. Hakuna mwalimu aliyepata ajili bila Mimi kumuandikia taarifa mwajili kuwa mwalimu huyu ameshinda vipimo alivyopewa. Kimsingi kila kitu katika shule ile kilinihitaji na kunitegemea.

Mamlaka niliyopewa ya uamuzi wa mambo mengi na kupitishwa kwa kila kitu nilichosuggest kwa mmiliki wa shule ilinipa moyo wa ujasiri sana. Kutokana na kibarua changu mmiliki wa shule alinipa mshahara mkubwa kushinda mwalimu mwingine yeyote yule. Hata mkuu wa shule nilimshinda kwa mshahara Hapa nikaanza kujiuliza ikiwa mimi ndiyo mshahuri wa karibia kila kitu kihususho utaalamu wa uendeshaji wa shule , Je siwezi na Mimi nikafikiria kuanzisha shule yangu?

Baada ya kufikiria sana nikaona ni lazima Mimi niwe mmiliki wa shule. So kuanzia hapo Mimi nikaanza kujiona kuwa ni mmiliki wa shule kubwa isiyoonekana kwa macho. Kimsingi mimi huwa sianzi kwa kutafutapesa kisha wazo bali naanza na wao kisha nafikiria pesa. Hivyo nikaanza kutafuta jina la shule nikaona iitwe EXODUS. Jina EXODUS nililipata kwenye biblia kitika kitabu cha KUTOKA 3.8 ambacho kinasema "nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi". Hapo nilikuwa nafikilria kuwa shule nitakayoijenga iwe miongoni mwa shule bora katika jamii nitokayo ambayo itakuwa kimbilio la watoto wa masikini ambao wamekuwa wakidanganywa siku zote na walala Hai walioko serikalini kuwa Kiswahil ni lugha ya taifa lakini walala hai wenyewe hawawapeleki watoto wao kwenye shule zinazofundisha ELIMU ya msingi kwa lugha ya Kiswahili hivyo kuwanyima watoto wa masikini fursa lukuki, Katika ulimwengu huu ambaodunia yote tunaishi kama tupo kwenye kijiji kimoja. Kimbilio la watoto walao mlo mmoja. Kimbilio la watu wasiowaza maisha bora na wakitoka wawe kama wametoka kwenye nchi ijaayo maziwa na asali.

simulizi yangu ya safari yangu ya kumiliki shule itaendelea kesho. Nahaidi kuwawekea picha za jengo langu la shule. Safari ni hatua wakuu.

speechless!
 
Nilianza safari kwa kufanya study ya sehemu ambayo naweza kununua ardhi kwa bei nafuuana iliyo na population yenye income nzuri kidogo . Nilifanikiwa kupata hekali 10 ndani ya wilaya mojawapo katika mkoa wa Morogoro. Kijiji ndicho kilichonipatia eno. Hekali 10 kwa shilingi laki tatu(300,000/-) tena Ardhi oevu ambayo licha ya ujenzi wa shule tunaweza tukapanda migomba na miti ya matunda kwa ajili ya wanafunzi.
 
Baada ya hapo nikaanza safari ya kutafuta kibari cha ujenzi wa shule. Kusema ukweli hapo nilikutana na vigingi vikubwa sana. Wahusika waliniwekea mizengwe lukuki lakini nilipambana na mwisho wa yote nilifanikiwa kukiweka kiganjani kibari changu ujenzi wa shule.
 
Nilianza ujenzi taratibu. Kila nilipopata pesa nilitenga kiasi furani kwa ajili ya mwendelezo wa ujenzi wa shule yyangu. Kwa sasa namalizia kukamilisha ujenzi wa madarasa mawili na ofisi. Ni matarajio yangu kuwa mwakani nikaanza kuandikisha wanafunzi wa kwanza katika shule yangu. Taratibu sasa nimeanza kuona ile ndoto nilikuwa nikiiota ambayo watu wengine hawaifahamu inaanza kuonekana live. Je ndoto yako ni ipi? Karibu kwa picha na maoni.
 
Hapa ni jengo la shule ambalo nimekuwa nikipambana kwa miaka mitatu kulikamilisha.
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    103.9 KB · Views: 320
  • image.jpg
    image.jpg
    106.4 KB · Views: 300
  • image.jpg
    image.jpg
    122.8 KB · Views: 285
Nilianza ndoto yangu ya kumiliki shule nikiwa nimeuanza mwaka wa tatu wa masomo yangu ya degree. Wakati huo niliapply kazi ya KUFUNDISHA katika shule moja ya English medium. ELIMU ya mkuu wa shule ilikuwa ni certificate level. Kwa kuwa Mimi nilikuwa na diploma ya ualimu nilipewa majukumu ya kumshauri mkuu wa shule pamoja mkurugenzi wa shule na msimamamizi wa usajili wa walimu wapya pamoja na mkakuzi wa kazi zao. Hakuna mwalimu aliyepata ajili bila Mimi kumuandikia taarifa mwajili kuwa mwalimu huyu ameshinda vipimo alivyopewa. Kimsingi kila kitu katika shule ile kilinihitaji na kunitegemea.

Mamlaka niliyopewa ya uamuzi wa mambo mengi na kupitishwa kwa kila kitu nilichosuggest kwa mmiliki wa shule ilinipa moyo wa ujasiri sana. Kutokana na kibarua changu mmiliki wa shule alinipa mshahara mkubwa kushinda mwalimu mwingine yeyote yule. Hata mkuu wa shule nilimshinda kwa mshahara Hapa nikaanza kujiuliza ikiwa mimi ndiyo mshahuri wa karibia kila kitu kihususho utaalamu wa uendeshaji wa shule , Je siwezi na Mimi nikafikiria kuanzisha shule yangu?

Baada ya kufikiria sana nikaona ni lazima Mimi niwe mmiliki wa shule. So kuanzia hapo Mimi nikaanza kujiona kuwa ni mmiliki wa shule kubwa isiyoonekana kwa macho. Kimsingi mimi huwa sianzi kwa kutafutapesa kisha wazo bali naanza na wao kisha nafikiria pesa. Hivyo nikaanza kutafuta jina la shule nikaona iitwe EXODUS. Jina EXODUS nililipata kwenye biblia kitika kitabu cha KUTOKA 3.8 ambacho kinasema "nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi". Hapo nilikuwa nafikilria kuwa shule nitakayoijenga iwe miongoni mwa shule bora katika jamii nitokayo ambayo itakuwa kimbilio la watoto wa masikini ambao wamekuwa wakidanganywa siku zote na walala Hai walioko serikalini kuwa Kiswahil ni lugha ya taifa lakini walala hai wenyewe hawawapeleki watoto wao kwenye shule zinazofundisha ELIMU ya msingi kwa lugha ya Kiswahili hivyo kuwanyima watoto wa masikini fursa lukuki, Katika ulimwengu huu ambaodunia yote tunaishi kama tupo kwenye kijiji kimoja. Kimbilio la watoto walao mlo mmoja. Kimbilio la watu wasiowaza maisha bora na wakitoka wawe kama wametoka kwenye nchi ijaayo maziwa na asali.

simulizi yangu ya safari yangu ya kumiliki shule itaendelea kesho. Nahaidi kuwawekea picha za jengo langu la shule. Safari ni hatua wakuu.

safi sana Eberhard, wewe ni mtu wa kutoa results enh? huna maswali wala hutaki maoni! some character!
barikiwa sana mkuu.
 
Nilianza ndoto yangu ya kumiliki shule nikiwa nimeuanza mwaka wa tatu wa masomo yangu ya degree. ......
simulizi yangu ya safari yangu ya kumiliki shule itaendelea kesho. Nahaidi kuwawekea picha za jengo langu la shule. Safari ni hatua wakuu.
Hongera sana kwa kweli hii ndio mtu kuwa na vision na kuisimamia hadi iwe kweli, wengi wetu tunakutana na vikwazo vidogovidogo tunaachilia ndoto zetu kirahisi, Mungu akutie nguvu usimamie wazo lako.
 
Tuko pamoja mama Joe. Ninazo ndoto nyingi ambazo naamini zitatimia kwa wakati wa Mungu. Kutimia kwa ndoto zangu hakutegemei fedha bali umtegemea Mungu anipaye pumzi.
 
Ukiwa na Mungu siku zote utasema " Nayaweza yote katika YEYE anitiaye nguvu".
Ndoto kwanza, pesa baadaye! Hongera bro!
 
Hasa! Mimi ninafukuzia ndoto yangu, kupitia hapa tayari nimeweza kuandika business plan, nimesimamia hapa: Yeremia 32: 26-27 mambo yakiwa tayari nitakuja waonyesha.

Ngoja nichukue biblia nitazame hiyo. Ndoto ni muhimu kwa ajili ya kutengeneza ulimwengu mpya kwa vijana usiokuwa tegemezi.Nina ndoto na Mungu anatuwaziamema hivyo ndoto itatimia.

Nb. Hakika ni kweli hakuna JAMBO la kumshinda Bwana.
 
Ni kweli ukiamini na kukaza roho, hakuna lisilowezekana ni sisi wenyewe au hatujui nini tunataka au tunakata tama mapema.
 
Kwa sasa nipo katika hatua ya kuvuta maji. Nimeshalipia gharama zote za uvutaji maji. Pia nimeshaamilisha mpango wa kupata walimu wawili wazuri ambao watafungua shule yangu. Hawa nitawatoa Kenya kwani wakenya ni wazuri sana kwenye kufundisha watoto.

Mwendelezo wa ndoto yangu ni pamoja na kupanda hekali 5 za migomba ndani ya eneo langu ili watoto waweze kupata ndizi pia nitapanda matunda hekali mbili watoto waweze kufaidika na matunda. Nitafanya kila liwezekanalo kwa uweza wake aliye juu kuhakikisha vyakula vinakuwa vingi ili kukamilisha ndoto ya nchi ijaayo maziwa na asari pale shule Kwangu.

Yeyote mwenye ndoto ya kumiliki shule kama mimi anaweza kuwasiliana na Mimi kama anao huitaki wa write up ya proposal ya ujenzi wa shule. Proposal ikiwa nzuri ni rahisi kupata financial support. Ya kwangu nimeshapata rafiki mmoja ambaye amehaidi kunisaidia kukusanya funds kwa ajili ya ujenzi wa Bweni naununuzi wa gari la kubeba wanafunzi.
MTU WA DINI YEYOTE ANAWEZA KUPATA MSTALI WA KUSIMAMIA NDOTO YAKE KUTOKA KITABU CHA DINI YAKE.
MUNGU NI MWEMA SIKU ZOTE.

Ninawatakia asubuhi njema.
Bwana wa ndoto.
 
Eberhard hongera kwa kufanikisha ndoto yako, lkn naona unatarget kuchukua walimu wawili kenya kwa sababu umesema wanafundisha watoto vizuri! Ina maana hakuna kabisa watanzania wenye uwezo huo?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom