FBI walivyobaini utapeli na ugaidi wa Nabii Rashnishi toka India

FBI walivyobaini utapeli na ugaidi wa Nabii Rashnishi toka India

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
43,321
Reaction score
109,608
Hiki Ni kisa Cha kweli kabisa , kilichotokea nchini marekani kati ya mwaka 1981 Hadi 2009, ambapo Nabii MILLIONEA aliekua akifanya miujiza ya ajabu na mikubwa Sana kimataifa na Kujaza majukwaa mbalimbali ya mahubiri , alistukiwa na FBI Kua ni tapeli, Hasa pale alipojikuta anavuka mipaka na kuanza kufanya vitendo vya kigaidi kwenye ardhi ya marekani.

Tafadhali mods na msije peleka Uzi huu jukwaa la historia Wala jukwaa la simulizi, kisa hiki kibaki hapa hapa jukwaa la Intelijensia. Pia ntaiweka ktk mfumo Wa comment moja ili isiwachoshe wasomaji Hadi mwishoni. Natanguliza Shukran🙏

Ni hivi,
Mwaka 1981, Nabii MILLIONEA na maarufu duniani kutoka nchini India Dokta BAGWAN RAjNeeSh (inatamkwa "RAjNISHI) alifunga ndoa na mmarekani mwenye asili ya India anayeitwa Madam Anand Sheera(inatamkwa SHILA), mkazi WA Oregon,PORTLAND nchini marekani.

Baada ya wawili hao kufunga ndoa, Nabii Dr. RASHNISHI alijipata uraia WA kimarekani, uliomuwezesha kua na uhalali wa kununua na kumiliki ardhi, hivyo kushawishika kufungua tawi jingine la kanisa lake nchini marekani.

Nabii Dr. RASHNISHI alinunua zaidi ya hekali 64,400 za ardhi mjini oregon kusini , na kuanzisha kilimo Cha kisasa Cha umwagiliaji matunda na mbogamboga, ndani ya Hilo Hilo eneo, akajenga KANISA lake KUBWA, shule yake,hospitali yake, shopping mall zake, barabara za lami, pamoja na apartment za kisasa zaid ya 1,000 Kwa ajili ya waumini wake, wagonjwa wake,familia yake pamoja na wafanyakazi wake.

****************
 
2.
Sasa Kwa jinsi kanisa lake lilivokua linazidi kukua Kwa kasi, wenyeji WA Oregon hawakupenda mtindo wake WA kuabudu WA kanisa lake (makelele yalikua mengi). Hivyo walipeleka malalamiko serikalini kua analeta usumbufu Kwa jamii ya wenyeji.

Na kwasababu baadhi ya viongozi WA kisiasa eneo lile hawakua na shida nae, kesi nyingi dhidi yake hazikuchukuliwa uzito Sana. Zaid zaid utaulizwa "Unahitaji sh ngapi ulipwe ili uhamie sehemu nyingine unakohisi utapata utulivu".

Wengi wa walilipwa walihamia kaskazini mwa oregon na maeneo mengineyo kuepuka adha za makelele ya kanisa la nabii RASHNISHI.

Nabii RASHNISHI aliendelea kujitwalia maeneo Hadi akafikia kumiliki hekali 76,000 kusini mwa oregon kihalali kabisa.

Suala la kuhamisha Watu ovyo, ujaaji wa wageni wa kihindi ndani ya oregon (wengi wakiwa waumini na wafanyakazi wake) na ukuaji WA kanisa lake Kwa Kasi sn, na malalamiko juu ya namna yake ya kuabudu kwake, vilizua minong'ono mingi sana serikalini Hadi kufika bungeni akajadiliwe, either aendelee na kanisa lake au afurushwe tu arudi kwao India.

**************
 
3.
Mjadala ulikua mkali sn Ila mwisho wa siku bunge liliazimia aachwe tu maana Imani sio kitu Cha kupangiana, Kama ni ishu ni wageni kujazana Oregon mbona "marekani yote imejengwa na wageni, Hadi wabunge wengi ni wageni" .

Hivyo bunge la seneti hawakuona hatia yoyote kwake, ukzingatia eneo lote la Oregon alilohamisha Watu limeendelezwa kiuchumi na linakua kimaendeleo Kwa Kasi sana.

Pia MIONGONI mwa wabunge waliokua wanamjadili , walikuepo baaadhi wabunge waliokua waumini WA kanisa lake. Na wengi wao walitoa shuhuda mbalimbali jinsi Nabii Dr. RASHNISHI mbali na kutibu matatzo mbalimbali ya watu kiroho, pia aliwawezesha wananchi maskini kiuchumi.

Watu maarufu (wanasiasa Hadi waigizaji maarufu wa Hollywood )waliokua wakimtembelea kanisa kwake walipewa zawadi mbali mbali, ikiwemo fedha, Vito na magari ya kifahari.

Kiufupi televisheni zote nna vyombo vyote vya habari Kwa wakati huo vilikua vikimzungumzia Sana Nabii Dr. RASHNISHI, miujiza yake,waumini wake, maisha yake,utajiri wake pamoja na project zake zote Kila KUKICHA.

Mivutano na wenyeji iliendelea Hadi kipindi cha kukaribia uchaguzi mdogo wa oregon, Supporters WA RASHNISHI nao wakataka wawe na uwakilishi wao kwenye serikali inayowaongoza wakidai kua wananyanyapaliwa Sana na wenyeji.

Mivutano ya kisiasa ilkua mikali sn Hadi kufikia kutishiana maisha pande zote mbili. Ila serikali ilijitahidi sn kuzituliza pande zote mbili kuelekea uchaguzi mdg ili yasije kutokea maafa, maana Oregon siku zote inafahamika jinsi ilivyokua kitovu cha amani.

***********************
 
4.
Siku Moja, kaskazini mwa oregon, hospitali ya serikali, madaktari wakapokea wagonjwa wengi sn Wenye dalili za kufanana (tumbo kunyonga sana,kuharisha na kutapika mfulurizo) na wote wakiwa ktk Hali mbaya sana kiafya.

Vipimo vilipochukuliwa, majibu ya maabara yalivorudi, ikaonekana wote wanasumbiliwa na mdudu mwenye asili ya kufanana na salmonella. Kikawaida, salmonella ndie mdudu anaesababisha taifodi. Hivyo wagonjwa wote walioletwa hospital wakaanzishiwa matibabu ya taifodi haraka Sana.

Ikabidi sasa taarifa zaidi zifike wizarani kua Oregon kaskazini wamepatwa na mlipuko WA ugonjwa WA taifodi, Ni siku ya 3 mpaka Sasa, Ila wagonjwa WA taifodi wanazidi 100 na wengine wakizidi kuletwa.

Hivyo taarifa zile wizara ikazipeleka CDC (center for disease control) ili waanze Mara Moja ufuatiliaji na upambanaji WA ugonjwa huo WA mlipuko.

****************
 
5.
CDC walivofika Oregon ikabidi wawapitie wagonjwa mawodini, mmoja mmoja, kuwahoji, imekuaje kuaje wameambukizwa, makazi na shughuli zao, wamekula Nini, wapi na walichokula kimetoka wapi.

Kwenye interview, Asilimia kubwa ikabainika walikula kachumbali na mboga za majani, na wengi wao walipata chakula migahawa miwili maarufu, na wafanyakazi wao wengi walilazwa pale. Basi ikabidi migahawa Ile ipigwe LOCKDOWN (isitishe huduma haraka sana) ili kupisha uchunguzi.

Sasa uchunguzi ulivozidi kuendelea na wagonjwa wakizidi kumiminika hospitali, CDC wakabaini, sio TU wahusika WA migahawa Ile, Bali Hadi Watu waliokula vyakula vYao majumbani mwao, nao walipatwa na ule mlipuko.

Uchunguzi WA CDC ukaendelea, wakahisi labda maji ya manispaa wanayotumia pale North Oregon huenda ndo yamesababisha ule mlipuko, vipimo vya maji vikachukuliwa, na majibu yakaja ni NEGATIVE. CDC wakazidi kuchanganyikiwa.

********************
 
6.
Basi ikabidi wapitie masokoni na supermarkets mbalimbali kubaini huu mlipuko either umetokana na nyanya, vitunguu, hoho au spinachi (chainizi) maana wagonjwa wengi wanaosumbuliwa wanaonekana wametumia vyakula hivyo.

Majibu Sampuli zilizochukuliwa yakaonyesha mlipuko huu umetokana na SPINACH maana Sampuli za nyanya, vitunguu na hoho yalikuja NEGATIVE (hazikua na salmonella). Hivyo CDC Wakahitimisha kua huu mlipuko umesababishwa na ulaji wa spinachi.

Sasa swali likaja, Ni spinach ya wapi hii imeleta huu mlipuko. Ikabidi ifanyike tena interview ya kuwauliza wote (masokoni na supermarkets ) waliokutwa na spinach zenye positive salmonella, waeleze wamezinunua kutoka wapi.

Majibu Ya wengi wao yakawa ni kua wamezinunua kwa wafanyabiashara wanaojumua mboga mboga za jumla toka kwenye mashamba ya kanisa la kiorthodox lililoko kaskazini mwa oregon.

CDC wakajiuliza swali, Je Hawa salmonella humu mashambani kwenye mboga mboga wametokea TU wenyewe au Kuna mtu kawapandikiza? . Wote Majibu wakakosa, Basi ikabidi mashamba Yale yote ya kanisa yapigwe lockdown, kusubiri uchunguzi zaidi huku matibabu ya wahanga yakiendelea.

*******************
 
7.
Siku zimeenda na wagonjwa wanazidi kuzidiwa, vijana ndo angalau walipata nafuu wakitibiwa, ila wazee na watoto wachanga wengi wao walifariki Kwa tumbo kuuma, kuharisha na kutapika bila kikomo.

Matibabu ya taifodi waliyokua wanapewa,wengi wao yalikua yanadunda. CDC wakapewa taarifa kua matibabu ya taifodi wengi wao hayawasaidii.

Wananchi nao walivoona wagonjwa wanaopelekwa hospital kutibiwa wanafariki Sana, baadhi Yao wakaacha kwenda hospitali kabisa.

Wengine walienda kwa waganga kupiga ramli, wengine tiba asilia, wengine wakaenda makanisani, Kwa wachungaji, na manabii. Ila wengine walipakimbia kabisa pale North Oregon na kuhamia maeneo mengine.

Cha kushangaza Sasa,
Wagonjwa WA taifodi waliopelekwa kuombewa kanisani kwa Nabii RASHNISHI, wengi wao walipona kabisa.Na shuhuda zilikua nyingi. Media zote zilimtangaza Nabii RASHNISHI Kama mkombozi Kwa kutibu wagonjwa WA mlipuko kwa maombi na kuwanywesha maji ya upako.

Serikali ilifurahi sn na Kumpa Kila sapoti aliyohitaji maana wagonjwa waliofika kanisani kwake kutibiwa walikua wengi Sana na usalama wao ilishakua mdg sn sababu ya msongamano kua mkubwa sn.

Ila Sasa Kwa upande wa wanausalama (FBI) wakaanza kutilia mashaka hii move ya Nabii RASHNISHI, wakahisi huenda kuna foul play, maana ugonjwa ulikoanzia ni kwenye mashamba ya kanisa pinzani na hili linalowatibu Wagonjwa Hawa Hawa wa taifodi.

*************
 
8.
Mashaka ya FBI yakawapeleka Hadi Kwa mtafiti mkuu wa CDC kwenye lile janga (DR. MICHAEL SKEEL), wakakuta nae ana mawazo Kama Yale Yale ya Huenda kuna foul play. Basi ikabidi washirikiane kufanya uchunguzi kimya kimya bila kuzua panic kwenye jamii.

Fbi wakamtuma mtu wao kwenye kanisa la NABII RASHNISHI nae ajifanye mgonjwa WA mlipuko,nae anahitaji maombi pamoja na maji ya upako.

Mgojwa WA fbi alipofika madhabauni, akaombewa vizuri na nabii, Ila ilipofika wakati WA kunyweshwa maji ya upako, mgonjwa yule akawa Kila akinyweshwa maji anayatapika.

Ndugu WA mgonjwa yule (nao ni fbi) wakaomba wafungiwemaji ya upako ili akanywee nyumbani. Nabii akaikataa kata-kata kua maji Yale huwa hayaondoki madhabauni. Wagonjwa wote wanaywea pale na kuondoka zao.

Basi ikabidi mgonjwa yule awekwe pembeni na chupa yake ya Dawa, ili anyweshwe polepole mpaka amalize.Huku Nabii akiendelea kuhudumia wagonjwa wengine waliofika pale madhabauni.

Sasa kwasababu ya ubize WA Nabii pamoja na wasaidizi wake, mmoja wa ndugu WA mgonjwa akachomoka Kama anaenda chooni, na kule akaswap maji ya upako (akaweka mfukoni) na maji ya kawaida (akayaweka kwenye chupa ya upako) na kurejea madhabauni Kama kawaida.

Baada ya kufanikisha mchakato huo, mgonjwa feki akapewa signal kua anywe ili waondoke zao (mission tayari). Na kweli mgonjwa kanywa na wameondoka zao pale madhabauni.

Maji Yale ya upako yamepelekwa CDC kwenda kufanyiwa utafiti zaid, Nini kinapelekea yanatibu ugonjwa ule.

**********************
 
9.
Dr. SKEEL akachukua Sampuli ya maji Yale ya upako na kuyapeleka kwenye mashine za CDC (electronic spectrophotometer) kujua Kama either Kuna kemikali za aina yoyote mle ndani au ni maji TU ya kawaida.

Alichobaini, ni kwamba ndani ya yale maji kuna mchanganyiko wa kemikali za ceftazidime pamoja na meropenem.

Wakarud kwny vitabu vyao, hizo Dawa ziliundwa kwa ajili gani na umekuaje zikaweza kutibu taifodi na wkt hazijawai kua Dawa ya taifodi. Wote wakakosa majibu.

Ila wakaamini huenda Kuna Siri imejificha ndani ya yale maji ya upako, na sio suala la kiroho TU yanatibu watu, maana nabii RASHNISHI kitaaluma ni daktari na Huenda Kuna vitu anaficha.

CDC na fbi hawakuishia hapo, ikabidi watafte wataalamu zaid WA microbiology, huenda wakapata majibu zaidi khs aina Ile ya wale wadudu WA taifodi.

Wakaambiwa Kuna Dokta mmoja anaitwa Tom Crook yupo Columbia university, ni mtaalamu zaidi WA diagnosis ya bacteria na muda mwingi amekua akifanya research khs aina tofauti tofauti za strain adimu za bacteria duniani. Ikabidi wakamuone.

Dr. Tom alivopewa zile Sampuli za wale bacteria, akaombwa awachunguze zaidi Kama kweli WAle ni salmonella au ni aina nyingine ya bacteria. Dokta akaanza kuwatizama Kwa umakini kwenye microscope yake, jinsi wanavyobehave kwenye mazingira tofauti tofauti.

Baada hapo akatoka na hitimisho kua wale ni SALMONELLA kweli, Ila sio salmonella Hawa tuliowazoea siku zote. Hawa ni aina adimu sana ya salmonella, wanaitwa Salmonella Typhimurium pig, Almaarufu kama Salmonella strain No 389.

**********
 
10.
Dr. Tom Akaongezea kua, Hawa ni salmonella wanaoambukiza zaid taifodi Kwa nguruwe. Na sio nguruwe TU, ni aina flani ya nguruwe weusi (adimu sana) wanaopatikana zaidi nchini india. Kesi za binadamu kuambikizwa aina hii ya taifodi ni adimu sana. Maana kutokea endapo umekula kinyesi chake au nyama isiyoiva vizuri ya nguruwe yule.

Mara ya mwisho mlipuko huu umetokea, ilkua ni mwaka 1914, nchini India, ambapo Watu zaid ya milion 4.5 waliambukizwa, na zaid ya watu 8,930 walifariki dunia kutokana na ugonjwa huu.

Sasa Wapelelezi Waliposikia kua Hawa wadudu asili Yao ni India, afu Nabii mwenyewe anatokea India, Kuna dot dot zikawa kama zinaungana kichwani.

Basi wakamuuliza, je Hawa salmonella strain no 389, wanabehave vipi Kwa dawa mbalimbali, na Kwanini hawawezi kutibiwa na Dawa za kawaida za taifodi.

Dr. Tom akawaambia kua Hawa salmonella Wana membrane ngumu sana, bila kuvunja membrane yao ya juu, huwezi kuwatibu kabisa, na wakishavunjwa membrane Yao, Wanakua dhaifu sana, wanaweza kuuwawa Hata na kinga TU ya kawaida ya mwili wa binadamu.

Akaulizwa "ni aina gani sasa za Dawa zinaweza kuvunja membrane Yao ili kutibu hili janga" . Dokta Tom akawaandikia list ya Dawa 3 zilizotumika mwaka 1914 kutokomeza janga lile nchini India.

Sasa MIONGONI mwa Dawa 3 alizotaja Dr.Tom, zilikuemo dawa mbili za ceftazidime pamoja na meropenem. Duh! Wataalam wakabaki na mshangao.

Wakakumbika kua ndo Dawa zile zile kule CDC walisema wamezibaini kwenye mchanganyiko wa maji Yale ya upako Toka Kwa Nabii RASHNISHI akiwanywesha wagonjwa.

Basi wote Fbi, CDC naColumbia university wakaamini ugonjwa ule haikua bahati mbaya, Nabii RASHNISHI aliupandikiza kusudi, maana utaalamu anao (ni daktari WA binadamu mzoeafu), Sababu anayo (lile kanisa mboga zilipolimwa, salmonella walikopandikizwa, walikua maadui) , na nyenzo anazo (ana miliki hospitali kubwa na yenye maabara ya kisasa).

Basi FBI wakaamua kwenda mahakamani na vielelezo vyao ili wapewe "search warrant" kwenda kukagua mazingira yote ya NABII RASHNISHI yanayomhusianisha na mlipuko ule WA ugonjwa. Kweli wakafanikiwa kupewa search warrant na kwenda kukagua Nabii RASHNISHI.

***************
 
11.
Wataalamu WA CDC, maafisa usalama WA fbi pamoja na maafisa uchunguzi (forensic team) kutoka vyomba mbalimbali wakatinga kwenye viwanja vya Nabii RASHNISHI kumkagua.

Nabii RASHNISHI mwenyewe hakuepo, alikuepo mkewe Madam Anand Shila na wanawe , pamoja na wafanyakazi wake mbalimbali

Breki ya kwanza ikawa ni hospitali, wakakagua hospitali nzima hakuna Cha maana wakapata. Ikabidi waelekeze Nguvu zao eneo la maabara. Pale maabara wakabaini kua Kuna handaki Kwa chini.

Yaani maabara ya juu ndio ilkua ikuhusika na matibabu ya kawaida pale oregon, Ila chini ya handaki, kuna maabara nyingine ya Siri na kubwa zaidi,ikiwa na Kila kitu kinachohusisiana na mlipuko ule.

Kwenye handaki walikuta:-
1. Mapipa 22 yenye kemikali mbalimbali, zikiwemo za ceftazidime pamoja na meropenem.
2. petri dish zaid ya 2,00 zenye wadudu Wale wa salmonella strain 389 waliorutubishwa pamoja na petri dish nyingine zaid ya 400 zenye wadudu wasioweza kutambuliwa wakiendelea kurutubishwa.

3. makopo ya Dawa mbalimbali za kurutubishia wadudu WA magonjwa.

4. vitabu na manual mbalimbali za jinsi kurutubisha wadudu WA magonjwa, kuwasambaza na kuwatibu.

5. CENTRIFUGE mashine kubwa ikiwa na mabaki ya mengi ya mbegu na maganda ya mimea ambayo baadae yalitambulika kua ni yakutengeneza sumu Kali Sana toka kwnye mimea mbalimbali.

Wakasema, "hakika mlipuko ule umeanzia humuhumu, hii maabara ndio imerutubisha wadudu wale, na Kila kitu kuwaeutubisha Kiko humu".

Basi wakakubaliana wafanyakazi wote WA Ile maabara wakamatwe na wakahojiwe ipasavyo. Kuna mengi Sana tusiyoyajua humu maabara.

Kweli wafanyakazi wote WA hospital wakawekwa chini ya ulinzi

*******************
 
12.
Uchunguzi ukaendelea Hadi kwenye makazi yake mwenyewe RASHNISHI, kule walibaini ndani ya Chumba anacholala, kwenye kabati analoweka Nguo, Kuna mlango WA Siri unaofungua Chumba kingine kilichokua kimesheheni silaha mbalimbali za kivita kama assault rifles, Ak47, grenades, rocket launch, landmines, pipe bombs, n.k.

Uchunguzi ulivoendelea ndani ya Chumba kile, wakabaini chini yake Kuna handaki, kufungua mlango wa handaki, wakakutana Chumba kikubwa chenye kufanana na maabara ya kijeshi.

Yaani walikutana na material mbalimbali za kutengeneza silaha za kivita.
1. Computer na server mbalimbali za kisasa,
2. 3D rifle moulding mashine-hii ni mashine ya kutengeneza bunduki
3. 3D silicon face printing mashine-hii ni mashine ya kutengeneza sura feki na vinyago mbalimbali.
4. Mapipa kadhaa yenye gun powder- unga wa kutengeneza baruti.
5. Masanduku kadhaa yenye dynamite, maligafi za kutengenezea mabomu na milipuko mbalimbali.
6.manual na vitabu mbali mbali vyenye maelekezo ya kuunda silaha mbalimbali.
7. Bunduki zaid ya 15

Sasa walipoanza kutoa zile bunduki ili kuzikagua zaidi, NDIPO walipobaini mlango mwingine Tena wenye handaki la Siri lenye urefu WA kilometa 2 linalotokea kwenye Banda la mifugo nje kabisa

Na walipofuatilia lile handaki Hadi mwisho, wakakutana nyayo mbichi za bidadamu kwenye vinyeshi vya mifugo (ishara ya kwamba, handaki hili Kuna watu wametokea hapa muda sio marefu).

FBI wakaamua kufuatilia zile nyayo
********************
 
13.
Basi wakaambiwa maaskali wafuatilie zaidi nyayo zile zinaelekea wapi. Kufuatilia wakagundua zinaelekea mashambani, Hadi kwenye uwanja WA ndege binafsi.

Vile FBI wanafika TU uwanjani, Ndege binafsi ya Nabii RASHNISHI ndo inang'oa nanga INASEPA. Ikabidi FBI wapige simu jeshi la anga (us air force) waone Kama wanaweza kuintercept ndege ile, Nabii RASHNISHI asije akakimbia nchi.

USA air force nao wakatuma ndege zao mbili juu kufuatilia ndege ya Nabii RASHNISHI. Sasa Nabii akiwa juu ya ndege akiamini Sasa anaenda kutorokea mexico, pembeni akaona fighter jet za kimarekani mbili zinaamuamrisha rubani WA ndege ageuze njia kwenda kutua ndege, vinginevyo watatunguliwa.

Ikalazimika ndege ya Nabii ikatue airport ya air force iliyokua karibu na mpakani. Nabii RASHNISHI na walizi wake, pamoja na rubani wakewakawekwa chini ya ulinzi.

Kule nyumbani, vitu vyote vikataifishwa na MKE WA Nabii RASHNISHI nae akakamatwa Kwa mahojiano zaidi.

***************
 
14.
Baada ya mahojiano makali na wafanyakazi mbalimbali ikiwemo wa hospitali khs kilichosababisha ule mlipuko WA janga lile,wakabaini kua master plan MKUU alikua Ni MKE WA Nabii RASHNISHI (yaani madam SHILA), na mtekelezaji. Mkuu alkua meneja WA hospitali. Dr. Gathi.

Dr. Gathi, Meneja WA hospital alikua (microbiologist kitaaluma) akafinywa na akafunguka kua ktk kikao chao kilichoongozwa na madam SHILA ktk vuguvugu la usumbufu WA wenyeji WA pale oregon (wakitakiwa wahame), waliazimia kupunguza idadi yao Katika namna ambayo haitazua shida Kwa serikali.

Plan ikawa ni litengenezwe tukio ambalo litasababisha siku ya kupiga kura, wenyeji WA North Oregon wote waumwe, lengo siku ya kura Wenyeji wa south oregon wawe ndio wengi, ili mtu wao aweze kushinda uchaguzi kirahisi. Ndipo madam akawaletea zile strain za salmonella na kuanza kuzirutubisha kisirisiri kwa kasi Sana.

Akaulizwa, "Sasa Kama lengo lenu lilikua ni waumwe siku ya uchaguzi, Kwanini mfanye shambulio lenu mwezi huu September wakati mnajua siku ya uchaguzi itakua ni mwezi November?"

Akafunguka kua, hili lilikua ni shambulizi la majaribio tu kutest Kama project yetu iko sawa au lah. Na Hilo sio shambulio la Kwanza , hili ni la shambulio lao la 5.

Tushafanya mashambulio mengi Ila mengine ni ya kawaida na hayana madhara Sana, ,lengo ni kuvuta waumini kanisani kwetu. Akaambiwa afafanue.

Dr. Ghati akasema kua Mara kwa mara wamekua wana project ya kuprocess mimea ili kutengeneza sumu ya ricin, sumu hii utengenezwa katika ile pure form Ila ktk concentration ya 50% (usiwe na madhara sana) ikiwa ktk Hali ya vumbi vumbi laini sn ambalo ni ngumu sn kuonekana Kwa macho ya kawaida.

Sumu hii ikishakamilika, kuwekwa ktk chupa ya kuspray na ushonewa ktk koti la nabii, Kisha Nabii anaweza kuibonyesha anapoamua na kuruhusu imuingie puani muumini wake anaemtaka MDA ule anapokua anamuombea jukwaani uku kamshika kichwani kwenye paji la uso.

Mtu yoyote akishaivuta hii sumu,ni lazima atapata kizunguzingu na kisha atapoteza fahamu ghafla na kuanguka. Ila kwasababu makali yake (concentration) sio Kali Sana,Hadi ila baada ya muda mfupi atazinduka.

Akasema pia IPO siku, Nabii aliwahi kutwambia tuiweke katka kiyoyozi Cha kanisa akiwa hayumo ndani yake, almost kanisa zima walipoteza fahamu, baada ya MDA dawa kupungua makali, akaingia na kujifanya kawaombea, wamepona na kawaokoa.

Ila kiuhalisia hakuwaokoa, alikua ndo muda anajua dawa ishatoka mwilini, kutokana na kujua imetengenezwa ikiwa ina makali kiasi gani.

Baada ya hapo, wapelelezi wakamwambia aendelee kuwaelezea mashambulizi mengine waliyoyafanya.

***************
 
15.
Jamaa kazidi kufunguka kua,
SHAMBULIO LA PILI,
Akasema mwezi march ktk kipindi ambacho sukari ilipanda Bei, walishawai kuagiza sukari na wakaifungua na kuichanganyia na kemikali hatari ya LEAD, iliyochanganywa na ACETATE, na Kisha kuifanyia repacking na kuirudisha sokoni ili kwenda kuuzwa north oregon tu ili watakaoinywa, wapatwe na utasa, wasiweze kuzaliana Sana (Huku wao south wakizaliana Sana). Hili lilifanikiwa maana sukari Ile ilishambuliwa Sana kwasababu iliuzwa Bei rahisi sana.

SHAMBULO LA TATU
Hili lilikua la kwenda kuspray vitasa vya milango ya wenyeji na ofsi za umma upande wa North oregon. Shambulio hili halikufanikiwa sana. Watu hawakuumwa Sana.

Shambulio la NNE,
Hili lilikua dhidi ya Wadhamini wawili WA kampeni za uchaguzi wa mgombea Toka north, waliokua na biashara za bar& restaurant eneo la North Oregon ndio walikua target ili kuwayumbisha kiuchumi na kuwatoa kabisa ktk biashara, Kwa kwenda kupandikiza wale bacteria Kwa kuwaspray maeneo ya mabenchi ya jikoni, vitasa vya milango na vyombo visafi vitakavyotumika kuhudumia wateja WA vyakula kesho yake. Shambulio hili lilifanikiwa maana tutakumbuka ndo migahawa Ile miwili ilipigwa lockdown mwanzoni TU mwa mlipuko na serikali kua sio salama Kwa afya za binadamu.

Shambulio la TANO:
Ndo lilikua la kwenda kuspray shamba kubwa Sana la mboga mboga la kule north oregon lililokua linamikikiwa na kanisa pinzani. Na Hali lilifanikiwa maana Watu zaidi ya 700 tayar walishakua wameumwa.

Jamaa akasema kua tathmini Yao, walishabaini kua ktk wiki hiyo ya uchaguzi, ndio wiki ambayo wataspray kila Kona ya North Oregon ili idadi ya wahanga angalau iweze kuanzia 5,000+ ili kuweza kuziba pengo la idadi ya watu 3000+ wanaopatikana south Oregon ili waweze kushinda uchaguzi kirahisi.
Duh! Wapelelezi wakabaki na mshangao.

Ikabidi wakamuhoji pia na madam SHILA nae wajue atafunguka yapi.

************
 
16.
Madam SHILA akawaambia hawezi kuongea chochote kile bila mawakili wake. Wapelelezi wakaendelea kumshikilia bila kumpeleka mahakamani, Ila wapi madam hakufunguka chochote kile. Mawakili nao wakawa wanazuiwa kuonana nae.

Basi Mawakili WA madam walivoona mteja wao anashikiliwa TU na hapelekwi mahakamani, na hawaelewi Nini kinaendelea , ikabidi waende mahakamani Kuomba mahakama iingikie kati.

Kule mahakamani jaji akatoa amri kua madam afunguliwe mashtaka mahakamani haraka iwezekanavyo, Kama hawawezi, Basi FBI wamuachie huru, Wanachofanya kukifanya ni kuvunja Sheria.

Basi ikatoka court order,
ikalazimika Madam afikishwe mahakamani. Hawakukawia Sana, NABII RASHNISHI nae akafikishwa mahakamani, pamoja na wafanyakazi waliotuhumiwa kuhusika WA hospitali ile. Wote wakashtakiwa Kwa makosa yanayohusiana na ugaidi. Shauri lao likaanza kusikilizwa rasmi.

***********
 
17.
Shauri lao lilivoanza kusikilizwa mahakamani,
MAHAKAMA ikasema NABII RASHNISHI mashtaka dhidi yake khs ugaidi hayana mashiko, maana hakuna kokote alikoonekana akuhusika Moja kwa Moja na kurutubisha au kusambaza wale salmonella WA mlipuko.

Pia mashahidi wote walioletwa na upande wa mashtaka, hakuna aliesema aliwai kuongea au kupanga chochote kile na nabii RASHNISHI khs Yale mashambulizi. Na pia chumbani kwake hakuna chochote kilichokutwa kinachohusiana na shambulizi lile la salmonella.

Nabii RASHNISHI akabadilishiwa mashtaka na kushtakiwa Kwa kumiliki silaha za kivita na vilipuzi kinyume na Sheria. Pia akashtakiwa Kwa kuingiza wageni nchini kinyume Cha sheria (baadhi ya madaktari kwny hospital yake walibainika wanaishi nchini kinyume na Sheria na walikiri wenyewe kuletwa marekani na nabii RASHNISHI).

Kwenye mashtaka hayo, shtaka la Kwanza khs silaha, Nabii RASHNISHI aliehukumiwa miaka 15 jela au faini ya Dolla LAKI 5 . Shtaka la pili khs uhamiaji, alihukumiwa miaka 5 jela au faini dolla Elfu 20. Mashtaka yote mawili Nabii RASHNISHI alilipa faini na kuachiliwa huru.

Nabii RASHNISHI punde TU baada ya kuachiliwa huru, alipanda ndege yake (private jet) na kwenda kutua jf Kennedy international airport, ambako alipanda ndege (Indian airways) na kwenda zake India. Hajawai kurudi Tena marekani, na ndege yake binfsi aliyoitelekeza pale jf Kennedy airport . Ilivokosa mwenyewe WA kulipia deni la parking and maintaince fees, serikali ikaitaifisha.

*************
 
18.
Kuhusu upande wa shaur la madam Sila,
Madam aliyakana mashtaka yote ya ugaidi aliyoshtakiwa nayo, akidai mashtaka yake yameegemea kwenye "hear says" na "someone said".

Mawakili WA utetezi (madam) wakasema kua upande wa mashtaka (serikali) hauna hoja na ushahidi za Moja Kwa Moja kumhusisha madam na ugaidi zaidi ya maneno ya kuambiwa na mashahidi wao (madaktari).

Ambao huenda wameyatamka under duress (kuteswa Sana) maana baadhi Yao wanaonekana waliingizwa mahakamani wakiwa wanachechemea.

Hivyo Basi upande wa mashtaka wakaamriwa na mahakama kua waende wakafanye uchunguzi Tena na wake na na ushahidi WA kueleweka ili kusapoti mashtaka Yao ya ugaidi. Hivyo dhamana ya madam ya madam SHILA IKO WAZI.

Sasa baada TU ya madam kupata dhamana, alitoroka nchini marekani na kukimbilia India. Siku ya kesi ilivotajwa tena.madam ikatafutwa na hakuonekana. Hivyo wadhamini wake wakakatwa na kuwekwa ndani.

Wadhamini wake walikaa ndani miez 9 jela mpk pale televisheni Moja iliyomuonesha Nabii RASHNISHI nchini Colombia kwenye mkutano WA injili akiwa na mkewe Madam SHILA.

Serikali ya marekani wakawasiliana na CIA kwenye ubalozi wao wa colombia ili ikiwezekana madam SHILA aweze kutekwa na kuwekwa kizuizin arudishwe marekani.

Sababu ya kutowahusisha serikali ya Colombia ilkua ni mivutano Yao kuhusiana na suala la kukamatwa Kwa Pablo Escobar na Genge lake la Medellin cartel (muuza madawa ya kulevya maarufu enzi hizo)

Ni kwamba Marekani waliilaumu Sana serikali ya Colombia ni CORRUPT SANA, wanakula na wahalifu, Kila wakiwahusisha kwny mission ya kumkamata Pablo Escobar,mission inafeli. Hivyo Hata hii ya kumdaka madam, wakahofia itafeli.

**********"
 
19.
Sasa msafara WA Nabii RASHNISHI na mkewe ukitoka kwny mkutano WA injili, ulivohisi unafuatiliwa na magari yasiyojulikana, na wanaowafuatilia Wana silaha, ukaamua kukimbilia kwenye majengo ya ubalozi WA India. Hivyo CIA WA pale Colombia wakashindwa kuwashikilia.

Ubalozi WA USA Colombia ukawasiliana na ubalozi WA India pale Colombia ukiwashinikiza wahalifu wale wakabidhiwe mikoni mwao. Ubalozi ukakataa, wakasema Kama wanataka kuwakamata raia wao, Basi wakawakamatie kwenye ardhi ya India au USA huko, wao hawahusiki. Ikabidi cia waachane na mpango huo.

Ubalozi WAo uliwasindikiza Hadi airport na wakahakikisha panda ndege salama na kuelekea India. Walipofika India, wakawa huru kuendelea na maisha Yao, huku serikali ya marekani ikiwasiliana na serikali ya India kuona namna gani madam anaweza kukamatwa na kurudishwa marekani kujibu mashtaka yanayomkabili.

Baadae serikali ya India ilikubaliana na marekani kumkamata madam na kumrudisha marekani akajibu mashtaka, Ila mpaka wanakubaliana, wakawa tyr washachelewa, madam keshakimbia,madaam alitafutwa Sana bila matokeo, Hadi akawekwa kwenye jarida la FBI MOST WANTED.

*******************
 
20.
Ilipofika mwaka 1990,
NABII RASHNISHI Akafariki dunia kwa kuugua maradhi ya moyo. Ilipofika mwaka 2010 FBI wakafunga rasmi faili la kumtafuta madam SHILA wakiamini Kwa miaka zaid ya 100 waliyokkua wakimtafuta, hawezi kua Bado Yuko hai, tayar atakua keshafariki dunia.

Sasa siku ya kufunga faili la kesi ya madam SHILA, kuliibika mabishano makali kati ya maafisa WA fbi kua either Ile kesi iwekewe hadharani au waache tu, maana kuweka wazi kesi Kama Ile kunaweza kuzalisha magaidi wengine ndani ya ardhi ya marekani Kwa mfumo Wa "COPY CAT" .

Yaani GAIDI anaweza kutokana na. Kile anachokiona kwenye tv, mabishano haya yalipofika ikulu, ikaamuliwa faili Hilo liwekewe wazi TU Kwa ummma, Haina haja ya kuficha ficcha, teknolojia ya Sasa imekua Sana sio Kama zamani, ukifanya ugaidi, tukiamua kukutafuta, tutakupata TU.

Basi habari ikawa imeishia hapo, waandishi wa habari wakaruhusiwa kuandika kisa hiki kwenye magazetinna majarida.Kampuni ya MEDICAL DETECTIVES chini ya filmrise, wakawatafuta wahusika waliokuepo enzi hizo, wakatoa shuhuda zao,Kiha documentary inayohusu kisa hicho inaitwa "BIO -ATTACK" ikazinduliwa,

FBI nao kwenye website Yao, upande wa "unsolved mysteries" ukiitafuta hii kesi utanikuta (japo Kwa Sasa sio unsolved Tena). Walishafunga faili la uchunguzi tayari.

*****THE END

NAWASILISHA🙏
 
Back
Top Bottom