Pole sana kwa kushindwa kunielewa na nitarudia kusema kile niaminicho....sijakusoma hapa,hiyo tiki taka ni phylosophy,na kila kocha ana phylosophy yake na ndio Guardiola ameamua kuifata.
...kuhusu kushinda makombe nayo ni bahati tu,unaweza kuwa na Messi kwenye timu na bado usishinde kila mashindano utakayoingia.
.....habari ya Mourinho anajua eti angeanza kumfunga Guardiola,nayo ni sababu fake..coz Mourinho ndio kaharibu mara mia zaidi ya Guardiola mpk kufikia stage ya kufukuzwa!!
..mwisho; unatakiwa ufahamu,kila kocha ana level yake na Guardiola sasa ni miongoni mwa makocha wachache wa daraja la kwanza.Hivyo kukaa unasubiri eti siku moja aende kufundisha stoke city,then washinde CL final ndio uamini anajua,is simply insane!
1. Unaposema Pep filosofi yake ni tiki taka naweza nikakubalia ila tambua mimi nimesema pep ameonesha udhaifu mkubwa kuipeleka tiki taka Bayern. Bayern ndo timu ya taifa ya German, ni sawa na Barca pale Spain. Amepeleka Tiki Taka Bayern, amevuna nini UEFA!!?? Unaweza ukaiweka level moja Bayern Pep na ya Heynkess!!??
Kama unatazama kwa makini utaona hata Style wanayocheza ni tofauti, Bayern ilikuw nzuri ktk nafasi ya Kiungo, Winga, Beki mpaka Mshambuliaji. Miaka ya hivi karibuni Pep kapeleka Tiki Taka, angalia Game zote alizotolewa UEFA amefungwa kwa style ipi. Anza na Game za Real Madrid alizomchapa nje ndani, angalia hata ile aliyompiga 4 kwake. Bayern ilikuwa ni weak ktk kukaba, na ndo hata Barca yake ilikuwa ni hivyo. Barca na Madrid wameifunga Bayern kwa pasi zisizozidi hata 8.
----Ukweli ni kwamba mashabiki wengi wa German hawakupendezwa na Tiki Taka, wajerumani hawataki soka la pasi nyingi, yaani mchezaji akipata nafasi ya kupiga mbali hawezi kupiga mpaka aingie ndani ya 18.
-----Wajerumani wamezoea kuona soka la kupiga pasi kadhaa kisha mpira unapelekwa golini, hawataki kuona timu inamiliki mpira mda mwingi bila kushambulia.
2. Huwezi kusema kushinda makombe ni bahati wakati una timu nzuri na kila kitu, bahati hii ilidondoka kwa Chelsea tuu na ndo maana mpaka leo hawajafika tena final. Mpira ni kujipanga, andaa wachezaji wazuri na mbinu nzuri makombe yatafata. Kama mpira ni bahati mbona Tanzania haijawahi hata kushirik World Cup au Arsenal kubeba UEFA. Pep alikuwa ana wachezaji wazuri sana pale Barca akiwemo Messi, Xavi na Iniesta ambalo walikuwa moto kipindi kile huku mfumo wa tiki taka uliosisiwa na Johan Cruyff ulikuwa ukisumbua sana timu pinzani.
-Zamani Barca magoli yake mengi alipenda afunge kwa move nzuri, yaani pasi zinaanzia kwa mabeki mpaka viungo, na viungo mpaka kwa Washambuliaji. Leo hii Soka linachezwa kwa viungo na mabeki na ikifika kwa washambuliaji basi mpira kwa viungo, kazi ya viungo wa sasa ni kudondosha mpira kwa MSN popote ilipo hata kama wamecheza pasi 3 ilimradi tu MSN imekaa sehemu nzuri basi pasi inadondoshwa, hii ni tofauti na zamani ambapo ni lazima wafate miiko ya tiki taka.
3. Ninasema na ninarudia kusema, Pep ni kocha wa kawaida tuu, sitashangaa kama Man City nao wakafundishwa tiki taka. Na endapo ikakutana na timu yenye wachezaji wenye kasi basi tutegemee mengine kwa Man City, mbali na hapo wachezaji waokoe jahazi maana Man City wana wachezaji wazuri wenye vipaji.