FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

UEFA Champions League Final: Barcelona vs. Manchester United Updates

The two best teams in the two best leagues in the world clashing in arguably the world’s most famous football stage—is there really anything not to love about Saturday’s UEFA Champions League final between Barcelona and Manchester United?

Saturday’s highly-anticipated final at Wembley in London should look somewhat familiar to most football observers, considering the match features the same sides that battled for Champions League glory two years ago in Rome, with Barcelona emerging victorious 2-0.

But plenty has changed since then.

Manchester United have transformed from a side that so heavily relied on the talents of Cristiano Ronaldo to a stout, resilient bunch that brushed aside English Premier League challenges from the likes of Arsenal and Chelsea en route to a domestic triumph.

Barcelona have a similar side to the 2009 group that triumphed in Europe, but replaced aging stars Thierry Henry and Samuel Eto with younger stars Pedro and David Villa to compliment the always-spectacular Lionel Messi up top. Pedro was on Barcelona’s 2009 side, but was rarely featured.

Some consider this to be an even stronger Barcelona side than 2009′s edition, but Manchester United have shown repeatedly that they are more than capable of comprehensively disposing any of Europe’s top competition in their run to the final.

Nikiwa kama mchambuzi wa soka nisiye shabiki wa timu yoyote duniani (ukiondoa Tanzania), hizi hapa nazitoa ni sababu 5 kati ya nyingine kadhaa zitakazoifanya FC Barcelona kuifunga Man U tarehe 28/05/2011. Ukiweza soma taratibu mstari kwa mstari, nimejaribu kufupisha sana angalau nisiweze kukuchosha.
  1. Ubora wa Kikosi
Hakuna ubishi kuwa hii ni fainali inayokutanisha timu mbili bora zaidi duniani kwa sasa. Wachambuzi wa soka tunaamini Barcelona ndio timu bora kuliko zote duniani kwa sasa na Man U ni timu ya pili kwa ubora kwa sasa. Ukiangalia kwa udani, utagundua kikosi cha Man U kimekosa ubora wa kiwango cha juu katika msimu huu ukilinganisha na misimu ambayo Man U ilitwaa ubingwa wa UCL (2008,1999). Ukiangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa FC Barcelona na Man U utaona fika kwamba kikosi cha Barca ni bora zaidi. Man U ina wachezaji wenye ubora, lakini wachezaji wenye ubora wa juu kabisa binafsi nawaona ni Edwin Van Der Sar, na beki nguli, kisiki cha mpingo Nemanja Vidic. Ili Man U iweze kuwa bingwa basi hawa wachezaji wawili ndio watakuwa nyota wa mchezo. Kuna makosa mengi ambayo Sir AF huwa anakubali kuwa aliyafanya na yaliicost Man U, kati ya yote ukimuuliza ni kosa lipi kubwa sana alilifanya atakuambia, pamoja na kumuuza beki nguli Jaap Stam bila kuwa na replacement, kosa kubwa zaidi alilolifanya ni kutomnunua Edwin Van Der Sar baada ya Peter Schmeichel kustaafu mwaka 1999.
Kwa tathmini ya one to one, FC Barcelona ni bora zaidi ya Man U.

  1. Kutokuwa na Consistence
Kikosi cha Man U msimu huu kimekosa consistence, ukiangalia tathmini ya msimu huu utagundua wachezaji wa Man U wamekuwa na ups na downs nyingi. Kuna mechi wanaweza cheza vizuri mno, lakini kuna mechi wanacheza hovyo kabisa, hii sasa inawaweka njia panda, kama siku ya fainali watakuwa down basi dhahama itawakumba. FC Barcelona wamekuwa katika kiwango cha juu msimu mzima. Hata game wanayofungwa unaona kabisa timu pinzani lazima ifanye kazi ya ziada sana sana sana. Japokuwa wachambuzi wa soka tunaamini FC Barca bado haijaweza kuwa katika kiwango chao walichofikia mwezi wa December, 2010 ila bado wanacheza katika consistence ya hali ya juu mno.

  1. Ukosefu wa Mchezaji Kiongozi
Baada ya Man U kupata tabu sana katika mechi ya kwanza iliyochezwa Old Trafford kwenye nusu fainali ya UCL 1999 na Juventus, goli la Ryan Giggs la dakika ya 90 likiwa la kusawazisha baada ya Antonio Conte kuwapa goli la kuongoza Juventus, kila mmoja alijua mechi ya marudiano jijini Turin, Man U angeangamizwa vibaya. Kumbuka Juventus ilikuwa inaongozwa na viungo bora kabisa Zinedine Zidane na Edgar Davids. Kweli, kwenye mechi ya marudiano baada ya magoli mawili ndani ya dk 11 za kwanza ya Fillipo Inzaghi kila mtu alijua Man U washatolewa. Inapofika sasa katika hali kama hii ndio hapo timu inahitaji mchezaji kiongozi. Kwa sasa Man U haina mchezaji wa kuinyanyua timu inapokuwa imelowa. Enzi zile walikuwa na kiungo, mwongoza timu Roy Keane. Yaliyotokea baada ya Roy Keane kufunga goli la kwanza la kurudisha matumaini dk ya 34 ya mchezo naamini wote mnayakumbuka.

  1. Nje ya Uwanja
Nje ya uwanja Man U ipo katika wakati mgumu sana. Ni ukweli usiopingika kuwa Man U wanaingia katika hili game la tarehe 28 wakiwa hawana uhakika mkubwa wa ushindi kama FC Barcelona. Kuingia kwenye game kama underdogs kawaida huwa kunakuwa na madhara sana especially pale mambo yanapoenda kinyume na matarajio dakika za mapema. Endapo Man U itaanza kufungwa uwezekano mkubwa mpira ukaisha mapema hata kabla ya dk 90, kwa wanaojua soka nadhani mmenielewa ninaposema mpira utaisha mapema. Kiujumla nje ya uwanja Barcelona wapo katika saikolojia nzuri zaidi kuliko Man U.

  1. Trio
Ofcoz, Trio ni sababu kubwa ya 5 ya Man U kufungwa tarehe 28. Hawa watu watatu wataigharimu sana Man U kuweza kuwadhibiti dakika zote 90 za mchezo. Nionavyo ni kwamba kwa sababu Pep anajua Man U ina ukuta mgumu sana katikati, atakachofanya ataanza kwa kushambulia tokea pembeni huku akiwa hana namba 9. Lionel Messi atacheza deep kama kiungo akiwa anatumika kama virtual centre forward hii itamfanya asiweze kukabwa na Vidic au Ferdinand. Wakati Messi atacheza kama kiungo, David Villa atakuwa anashambulia zaidi kwa kutokea kulia huku Pedro Rodriguez na Andres Iniesta watakuwa wanashambulia tokea kushoto. Hii itawalazimisha Nemanja Vidic na Rio Ferdinand kutanuka pembeni ili kuwasaidia mafullback Patrice Evra na kulia sina akika ataanza Fabio au Raphael, ila binafsi ninaamini akianza John Oshea itakuwa advantage kwa Man U maana yupo physic kuliko mapacha na pia anauwezo mkubwa wa kukaba na kuoverlap. Kutanuka kwa hawa centre defenders kutatoa mwanya kwa Xavi Hernandez na Andres Iniesta kusupply mipira kwa Lionel Messi. Mbinu pekee ambayo itawasaidia Man U kuweza kuwadhibiti hawa Trio ni kuanza kwa kutumia double holding midfielders, Darren Fletcher na Michael Carrick. Sina hakika sana na fitness ya Fletcher kwa ajili ya huo mpambano, maana japokuwa amecheza mechi ya mwishoni mwa msimu lakini bado fitness yake ina mashaka kidogo especially kwa sababu ya ugumu wa mechi yenyewe.
Ni jinsi gani Sir AF ataweza kuwadhibiti hawa vijana wa Barca, lets wait and see.

Cheers.
 
Naona auto numbering imegoma kwenye JF. Ila sio ishu sana japokuwa imereflect kama namba 1 kwenye points zote.
 
Mi roho inanidunda, ila kinachonipa matumaini ni kuwa siku zote Man Utd wakiwa Underestimated ndo huwa wanafanya kweli, yule mzee SAF anajua kuzichanga hamtaamini! Naamini safari hii Barca watalazimika kurudi Spain bila kombe!
Lets wait and see! Cheers kwa thread yako mkuu!
 
safi umejitahidi sana kuchambua lakini kikubwa tusubiri siku ya tukio.......
 
Mimi naamini siku hiyo mambo yatakuwa tofauti na wengi wanavyotarajia
 
Timu kama Chelsea, Arsernal au Real Madrid ndio unaweza kuwafanyia uchambuzi wa aina yako............Huyu Babu SAF ni kitu ingine aisee.....sijui huwa anawapa nini wale vijana wake.........Good try though
 
Kweli huyu mzee hatabiriki kabisa
 
Code:
1.Trio
Ofcoz, Trio ni sababu kubwa ya 5 ya Man U kufungwa tarehe 28. Hawa watu watatu wataigharimu sana Man U kuweza kuwadhibiti dakika zote 90 za mchezo. Nionavyo ni kwamba kwa sababu Pep anajua Man U ina ukuta mgumu sana katikati, atakachofanya ataanza kwa kushambulia tokea pembeni huku akiwa hana namba 9. Lionel Messi atacheza deep kama kiungo akiwa anatumika kama virtual centre forward hii itamfanya asiweze kukabwa na Vidic au Ferdinand. Wakati Messi atacheza kama kiungo, David Villa atakuwa anashambulia zaidi kwa kutokea kulia huku Pedro Rodriguez na Andres Iniesta watakuwa wanashambulia tokea kushoto. Hii itawalazimisha Nemanja Vidic na Rio Ferdinand kutanuka pembeni ili kuwasaidia mafullback Patrice Evra na kulia sina akika ataanza Fabio au Raphael, ila binafsi ninaamini akianza John Oshea itakuwa advantage kwa Man U maana yupo physic kuliko mapacha na pia anauwezo mkubwa wa kukaba na kuoverlap. Kutanuka kwa hawa centre defenders kutatoa mwanya kwa Xavi Hernandez na Andres Iniesta kusupply mipira kwa Lionel Messi. Mbinu pekee ambayo itawasaidia Man U kuweza kuwadhibiti hawa Trio ni kuanza kwa kutumia double holding midfielders, Darren Fletcher na Michael Carrick. Sina hakika sana na fitness ya Fletcher kwa ajili ya huo mpambano, maana japokuwa amecheza mechi ya mwishoni mwa msimu lakini bado fitness yake ina mashaka kidogo especially kwa sababu ya ugumu wa mechi yenyewe.

Hapa umezungumza vyema kama mchambuzi..n kweli jmosi fletcher hataanza na huko nyuma babu amejipanga vyema maana anajua madhara ya hiyo trio ..ngoja siku ya leo iende jioni then kesho presha ianze kupanda taratibu..mpaka jmosi itakaposhuka kwa Nderemo na vifijo!
 
Ninavyojua mimi huwezi kuchambua mpira kiasi hicho halafu hukawa huna timu Ulaya, inavyoonyesha wewe kama si ARSENAL basi utakua CHERLSEA subiri uone maajabu ambayo wewe utayaelezea au kuyachambua.
 
Broda hongera kwa uchambuzi

But you know what, this is not a game of Man U talented player against Barcas....it was in 2009 wakati kila mtu alipompa Ronaldo sifa ya kuwa skill na talent yake inaweza kuipa Man U ubingwa lakini haikufua dafu.....

This time it is Fergie against Barca and i tell you Fergie anajua yote haya and United have better chance kwa kuwa wanachukuliwa kama underdogs na unaweza ukachunguza United katika hali kama hii ndio huwa wanafanya mambo

By the way, wait and expect a very good game, a fantastic one
 
Ninavyojua mimi huwezi kuchambua mpira kiasi hicho halafu hukawa huna timu Ulaya, inavyoonyesha wewe kama si ARSENAL basi utakua CHERLSEA subiri uone maajabu ambayo wewe utayaelezea au kuyachambua.

Nilishakuwa mshabiki sana miaka ya 90 ndugu yangu, na mpira wa kimataifa nimeanza kuutazama zamani za kutosha, ila presha ilikuwa inanifanya nisiweze tazama mpira vizuri, nikaamua kujivua gamba la ushabiki. Hakika sina timu kabisa nje ya Tanzania japo mpira upo damuni. Saizi naangalia mpira kwa raha sana na ndio maana naweza kucome up na observation isiiya biased kabisa.
 
Man U ndio nini? Kuhusu Messi kucheza deep solution yake ni Three Lungs Park.
 
Man U ndio nini? Kuhusu Messi kucheza deep solution yake ni Three Lungs Park.

J.S Park hawezi kumzuia Messi kabisa, Messi anataka mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kukaba na kuzunguka uwanja mzima. Kumbuka ishu nyingine inatakiwa supply ya mipira kuelekea kwa Messi ipunguzwe sana au iwe blocked kabisa. Shida ya Messi akishaweka mpira mguuni kuuchukua ni either umfanyie faulo au otherwise anakuacha. Faulo kadhaa kwa Messi lazima zitaelekea kutolewa kwa kadi. Hivyo basi Messi anahitaji timu iliyojipanga vema sana kwenye diffence. Na kwa tactics ya mpira kama ushacheza, sio rahisi kwa mtu anayetumia mguu wa kushoto kukabwa na mtu anayetumia mguu wa kushoto.
 
Reactions: Aza
Observer analysis yako imekaa kitanzania Tanzania sana... Hivi katika Man Utd kuna mchezaji anayezunguka uwanja mzima kuanzia dakika ya mwanzo hadi mwisho zaidi ya Park?
 
Man U ndio nini? Kuhusu Messi kucheza deep solution yake ni Three Lungs Park.

Hapa mkuu umeniwahi., Park ni soln ya Messi., n'wayz let's wait maana babu hatabiriki, kikosi kinaweza kuja tofauti na tunavyotarajia..!!
 
mambo yapo iyo siku,kila kitu kitasimama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…