jana nilikuwa nacheki rekodi za makipa laliga 2015-16 za stegen siyo vutizi kabisa. alicheza mechi 7 na kuruhusu goli 7. Bravo alicheza 32 na kuruhusu 22. kwa uwiano huo Stegen angecheza 32 angeruhusu goli 32. Bravo alipigiwa mashuti 104 na kuokoa 84, ni kama 80% stegen alipigiwa 20 na kusave 13, kama 65%. katika mechi 7 ana cleansheets 2 wakati bravo ana 15 kwa mechi 32. kwa huo owiano stegen angecheza mechi 32 angekuwa na kama cleansheets 9 tu. ukilinganisha Navas, Oblak, Bravo na stegen, Stegen yuko kiwango cha chini sana. kwakweli tuna tatizo la kipa.