FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Cabellos ni Mchezaji gani uyuu😀😀😀😀
 
Rijkaard & Pep hawakuwa na ushawishi ?

Angalia wachezaji waliosajiliwa na Pep & Rijkaard ulinganishe na hawa wanaosajiliwa sasa .

Tito alikuwa assistant wa Pep so ilikuwa rahisi sana yeye kupewa timu baada ya mafanikio ya Pep na alianza vizuri sana

Tata yupo kwenye list ya makocha wabovu kuwahi kufundisha Barca i wonder hata umemtaja

Kwa miaka ya karibuni Ter Stegen na Suarez ndio usajili mzuri uliofanywa na Barca wengine wengi ni magarasa (Song,Vermaelen,Mathieu,Turan,Gomes,Vidal,Paco )

Paulinho sio mchezaji wa kuchezea Barca hata kwa £10m,mchezaji ambaye mpira wa ulaya ulimshinda akakimbilia China kukusanya hela ?
Barca hii ambayo imekuwa ikitoa wachezaji wazuri toka La Masia inataka kusajili mchezaji anayecheza China
 

Rijkaard pindi anachukuliwa awe kocha alikuwa na experience gani ? Alitoka kufundisha timu gani ? Ndio alikuwa anajifunzia ukocha Barca hivyo kwenye tasnia ya ukocha alikuwa hana ushawishi wowote ...



Pep 2008 nani alikuwa anamjua ?alikuwa na experience gani? Aliibuliwa na Laporta hivyo ushawishi hakuwa nayo ila emblem ya Barca ndio iliwavuta wachezaji.

Umesema Tata Alikuwa mbovu haswa hapo ndio point yangu mbona neymar worldclass player alisajiliwa kipindi chake ,nimemtaja Tata sababu hakuwa na ushawishi lakini Neymar alisajiliwa kipindi chake

Mjomba Barca wachezaji hawasajiliwi na rais bali sporting director &Kocha nakupa mfano mmoja 2014 Rais wa Barca alimtaka Pogba na ilikuwa kipindi cha uchaguzi na wagombea 3 walimtaka pogba na tayari alikuwa contacted lakini Enrique alikataa na kusema anamtaka Turan&Vidal mpaka laporta alikasirika lkn aliambiwa mwalimu ameshachagua hivyo signing ifanyike haraka kabla ya uchaguzi


Kuhusu migalasa unayoyasema wewe ni maamuzi ya Luis Enrique

Kuhusu paulinho sporting director amefanya analysis na kufuatilia na ameshauriana na mwl na kapata OK ila fahamu first option ni Verratti paulinho ni alternative wao technical secretary wanajua wanachofanya

Point ya kusema kocha hana ushawishi si kweli sema kila kocha ana mahitaji yake Enrique aliyapenda akina Turan
 
Mkuu kuwa na ushawishi sio lazima upate mafanikio kwenye ukocha ,Pep na Rijkaard ni wachezaji waliopata mafanikio sana wakati wanacheza.Pep ametokea Catalunya na alianza soka La Masia mpaka akaja kuwa Captain wa Dream Team kikosi ambacho kilikuwa cha kwanza kuchukua ubingwa wa Ulaya kwa Barca,Pep ni role model wa wachezaji wengi waliopita La Masia(Fabregas,Busquet,Xavi) na Pep alikuwa anafit sababu anaijua falsafa ya Johan Cruyff na kuwapa nafasi players toka La Masia

Rijkaard pia alipata mafanikio sana kwao Ajax na AC Milan (kote alichukua Champions League kote .Rijkaard alikuwa kocha wa Holland mwaka1998-2000 na aliifikisha Holland nusu fainali Euro 2000 (sijui unazungumzia experience gani)


Falsafa ya Barca inafahamika na wachezaji wanaofaa kwenye hiyo falsafa wanafahamika Paulinho hafit tangu wameingia Rossell na Batromeu ndio wameanza kuachana na falsafa hiyo na kukubali kusajili makocha na wachezaji wasiofit.Arda Turan anafaa kucheza mifumo ya kina Simeone,Mourinho au Conte na sio Barca ilifahamika tu atachemsha

Neymar hakusajiliwa sababu ya ushawishi ni fedha ndio zimemleta ndio maana Sandro Rosell ameenda jela sababu kubwa zilianzia kwenye usajili wa Neymar
Na huu usajili umeharibu sana image ya club
Laporta hakuwepo kwenye usajili wa kina Turan,Vidal hawezi kufanya huo ujinga aliyekuwepo ni Batromeu ndio chanzo cha matatizo mengi ya sasa ya Barca

 
kwa type ya mpira anaocheza Barca,usajili ni trial and error-unaweza kuwa world star na you don't fit in.Hakuna wa kumlaumu cause hakuna binadamu mwenye uwezo wa kujua who will fit in and who will not-hakuna mtu aliejua kwamba hawa recent signings only one or two will fit the bill
 
Kwenye signing usimlaumu Bartomeu unamuonea tu ni kocha na Robert ndio wanaoamua yupi asajiliwe na yupi asisajiliwe kwenye technical issues Bartomeu anakaa mbali sababu kuna technical timu inayoongozwa na Robert na Albert soler na ishu ya Vidal&Turan ni Luis Enrique aliwataka so vipi blames apate Barto na Enrique ndiye aliyeivuruga La masia .

Hivi kuna mchezaji kwasasa hataki kucheza na best players kama MSN.

Paulinho hana calibre ya Barca sijui wamewaza nini hawa ila bado naimani Verratti atatua tu
 
Nimekwambia matatizo mengi yanaanzia kwa Batromeu sababu yeye ndio boss wa Klabu hao kina Robert & Lucho yeye ndio anawaajiri bila Batromeu wasingekuwepo hapo Barca,yeye ndio anatakiwa kuhakikisha falsafa ya Barca " Mes en que " inafuatwa.Umeona jinsi walivyohandle issue ya key players kama Thiago,Alves,Pedro . I hope umeona jinsi Perez alivyoiongoza Real Madrid kwa sasa
 
Hii ni kweli, nani akijua kuwa Gomes aliyekuwa analiliwa na Man U na RM atakuja kuwa flop?
 
Huyu ndio Semedo na hizi ndio baadhi ya particulars za deal yake ya transfer
Kwahiyo habari za Bellerin tena tuzisahau kabisa ,hii ndio RB ,plan B ya Verrati ni nani?
Inasemekana Semedo ana potential zaidi ya Renalto Sanchez
View attachment 541708
Japo highlights za youtube zinadanganya lakini Semedo ni machine kubwa sana. Huwezi mfananisha na Bellerin. Belle anafaa kwenye counter huko.
 
Roberti anarudi kwenye MF. Mwenye kale kavideo anamtoka Modric, anamkimbiza Marcelo, anampa Gomea, Gomes anampa Alba na Alba anampa Messi na inakuwa 3-2 naomba akaweke.
 
Wakuu. Sasa kule right flank tuko covered. Kuna Vidal, na Semedo. Ukipanda zaidi unamkuta Messi. Saa hizi Viungo watafanya kazi ya viungo na si kutawanyika pembeni. Tutakuwa wa moto sana.
 
Sergio Robert arudi mid halafu raktick na turani wauzwe ili anunuliwe Verrati hapo ndio tutapata raha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…