Dr Who,
Hamna cha week end au nini , mambo ya michezo iende kwenye sehemu za michezo. Wenzetu wengi wa JF uzalendo uliwashinda na mmeamua kuishi uamishoni (ambako hampigi kura wala hamna fursa hata ya kugombea ubalozo wa nyumba kumi mnasubiri congress iwaokoe) kwa hiyo kwenu kweli kuna week end, sisi tulio amua kufia humu na kuendelea kula sahani moja na mafisadi week end ndiyo siku mbaya kweli maana tunakaa nyumbani nakuona nyumba za mafisadi zikiota kama uyoga wakati wewe uliyeamua kumheshimu mungu na wanadamu wenzio huna hata shilingi mia.
Mpira hata mimi napenda sana lakini haunifanyi niende cafe zaa hizi nianze kujadili kuhusu Arsenal au liverfool. lakini mafisadi wamenifanya nitoe book yangu ingawa nina book mbili tu ili niweze kuwajadili mafisadi ili watuachie na sisi tuanze kuwa na week end
Hoja kama hizi zinanifanye niukubari ushauri wa rafiki yangu anayedai kuwa JF ni ya makuwadi wa mtandao ambao lengo lao kubwa ni kutaka kujua kama wananchi wanaufahamu gani kuhusu madeal yao ili waweze kuyaficha vizuri.
ukiangalia kwenye JF kuna issue nyingi sana ambazo kwa kweli zinatisha lakini watu hawachangii kabisa lakini hii ya Arsenal iliyopostiwa katika sehemu isiyo yake watu wameshaweza kuchangia kibao, sasa sisi tueleweje?
Wana JF tunakuwa kama wabunge wa ccm tunaona issue tunazikimbia na kukimbilia kudai oooh tupewe mafungu ya mjimbo ili na sisi tukawatende wanavijiji wetu
Naomba wanaJF nipate maelezo ya kutosha ya kunifanya niendelee kutoa 0.01% ya mshahara wangu kwenda cafe kujadiliana na wapenda maendeleo wenzangu kwa saa moja na siyo mjadara wa Arsenal Please!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!