Features za kuvutia kwenye simu za Xiaomi

Reuben Challe

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
2,940
Reaction score
5,511
View attachment 2526578
Simu za Xiaomi zina features nyingi za kuvutia bila kupoteza muda naanza direct kuonesha features hizo

1. Hypercharging Ability
Xiaomi anatumia technology yake ya Xiaomi Hypercharging technology inayokuwezesha kuchaji simu yako kutoka asilimia 0 Hadi 100 kwa dakika 15 hadi 20 tu.
ili kufanya hypercharging isiharibu betri Xiaomi ameinclude features 34 kwenye battery, circuit na charger ili kuendelea kuwekea betri katika hali ya usalamaView attachment 2526550

2. App Lock
Simu za Xiaomi zinakuja na feature ya App Lock inayokuwezesha kulock apps unazozitaka kwa kutumia fingerprint scanner au face unlock.
View attachment 2526552

3. Horizontal/ Vertical Recent Apps
Tofauti na ilivyo kwa simu nyingi ambazo Recent apps zimekuwa arranged horizontally simu za Xiaomi zinakiwezesha kuarrange apps zako kwa njia zote mbili vertically au horizontally View attachment 2526555View attachment 2526556

4. Back tap
Feature hii inakuwezesha kuaccess tools kama Camera, torch, calculator, Google Assistant na Silent Mode kwa kubonyeza nyuma ya simu yako mara mbili au mara tatu.View attachment 2526558

5. App Volume control
Hii feature inakuwezesha kuwa na volume tofauti kwenye application tofauti tofauti. Kwa mfano unaweza kuset sauti kubwa YouTube, sauti ndogo Instagram na sauti ya wastani TikTok badala ya kuwa na sauti standard kwa apps zote.

6. Super Macro shots
Feature hii inasaidia kuboost uwezo wa kamera kupiga Macro shots na kufanya macro shots ziwe na ubora wa hali ya juu.

7. Clone Mode on Camera
Hii ni mode inayokuwezesha kuongeza clones za object unazozipiga picha. Kwa mfano ukimpiga picha mtu mmoja unaweza ku-multiply wakatokea wawili au zaidi.

8. Three-finger slide screenshots
Hii ni feature inayokuwezesha kupiga screenshots kwa kuslide down vidole vyako vitatu kutoka juu ya display hadi chini. Hii ni rahisi zaidi kuliko kutumia volume down and power button kupiga screenshots.

9. Second Space
Hii ni feature inayokuongezea phone layout nyingine kwenye simu yako. Feature hii ni nzuri sana, ni kama unatumia simu mbili tofauti ndani ya simu moja. Unaweza kuitumia kutenganisha apps zako za ofisini, au za entertainment na kuzitumia kupitia Second Space ambayo itahitaji password [emoji360] yako ili kuingia Second space.


10. Tones of Animated Wallpapers
Simu za Xiaomi zinakuja na live wallpapers nyingi tena ni za bure. Zipo nyingi yaani kuchagua ushindwe wewe tu

Hapa nimeanza na features kumi tu lakini features zipo nyingi sana. Nitaendelea nazo hapo chini kwenye hiihii thread.
 

Attachments

  • Screenshot_20230222-170252.jpg
    24.9 KB · Views: 35
1. Hypercharging Ability


2. App Lock

3. Horizontal/ Vertical Recent Apps

4. Back tap

8. Three-finger slide screenshots ...
 

Attachments

  • 1622639329748Cargador-Xiaomi-768x417.jpg
    15.5 KB · Views: 35
  • Screenshot_20230222-170224.jpg
    35.7 KB · Views: 43
  • Screenshot_20230222-170234.jpg
    31.8 KB · Views: 40
Hizi ni features nyingine nzuri zinazopatikana kwenye simu za Xiaomi
11. Wild Notification Alerts
Simu za Xiaomi zinakuja na Notification sounds za kutosha ikiwemo zile sauti zinazopatikana msituni au mbugani. Hivyo hii ni part ya software na inakuwezesha kutumia hizo sounds kwa Notification Alerts


12. Sound Assistant
Hii ni feature inayokuwezesha kusikiliza sauti mbili kwa wakati mmoja lakini katika frequency tofauti. Mitandao kama Instagram inaonesha picha na video. Ukifika kwenye video ukiiplay kama ulikuwa unasikiliza mziki basi mziki wako unakata hapohapo ili kuruhusu video ya Instagram iplay. Kwenye simu za Xiaomi unaweza kupunguza sauti ya Instagram na kuongeza sauti ya mziki wako hadi mwisho bila ku-interfere sauti ya Instagram

13. Reading Mode
Feature hii inasaidia kulinda macho yako ikiwa unasoma vitu kwenye simu yako. Kazi ya Reading mode ni ku-reduce blue light, using warmer colors na ku-add paper-like texture kwenye simu yako. Unaweza kuset Reading Mode iwe inaswitch on automatically


14. Dual Apps
Hii ni feature inayokuwezesha kutengeneza copy ya application za simu yako na kutumia app hizo kivyake. Kwa mfano unaweza kutengeneza copy ya app kama Facebook, WhatsApp, Instagram na Jamii Forums na kuzitumia apps hizo kivyake tena kwa kutumia account tofauti tofauti.
NB: Clone ya application haiwezi ku-interfere original applications

15. Video Tool box
Ukiwa unatumia YouTube au application nyingine za kustream video, ukitoa tu kurudi homescreen na video playback inastop. Video tool box inakuwezesha hata kuzima simu yako wakati video inaplay YouTube,. na bado ukawa unasikia sauti bila video. Kwa hiyo unaweza kuendelea kusikiliza kinachoongelewa YouTube bila hata kuwa active ndani ya YouTube. Unaweza hata kuingia Jamii Forums huku sauti ya video ya YouTube inaendelea kupiga.

16. Floating Windows
Software ya MIUI inakuruhusu kufungua apps kwenye floating Windows. Hii ni moja ya feature nzuri sana. Hizo floating windows unaweza kuzi-minimize, kuzi-expand au hata kuzidisable kwa kutumia simple gestures

17. Split Notification Shade
Ukiswipe down kutoka juu kona ya kushoto kushuka chini simu inakuletea Notification bar na ukiswipe down kutoka juu kulia kushuka chini simu inakuletea Mi Control Centre.
Hii ni feature ya kipekee sana na iko tofauti na simu nyingine za Android. Pia unaweza kuiondoa na kuwekea ya kawaida tu kama simu nyingine za Android.

18. Game Turbo
Hii ni feature ambayo kazi yake ni kuboost performance wakati wa kucheza magemu. Inalazimisha simu kutumia kiasi kikubwa zaidi cha RAM kadri inavyowezekana na kukupa smooth gaming experience katika graphics nzuri.

19. Memory Extension
Hii ni feature ya MIUI 13 and above ambayo inakuruhusu kuexpand RAM ya simu yako. Kama simu yako ina storage ya 64GB unaweza kuexpand 1GB RAM tu na kama simu yako ina storage ya 128GB and above unaweza kuexpand 2GB hadi 3GB RAM

20. Themes and Always on display


21. Side Bar
Feature hii inakuwezesha kuaccess your favorite apps kwa kuhold au kutap mara mbili kwenye edge ya simu yako.

22. Security App
Simu za Xiaomi pia zina security app ambayo kazi yake kubwa ni ku-scan simu yako na kila app utakayodownload kama ina virus au malware. Pia inaweza kufanya vitu vingi kama ku-clear RAM, kumanage Blacklist yako, na mambo kibao

Kwenye simu za Xiaomi bado kuna features nyingi sana, na siku nyingine nitakuja kuendelea kuzitaja kwenye hiihii thread. Siku nyingine pia nitataja features za kwenye simu za Samsung.
Ikiwa unatumia simu ya Xiaomi halafu huzijui features zake basi hizo nimekutajia anza kujaribu kutumia ulizozipenda
NB: Features zinategemea na MIUI version unayotumia na simu unayotumia. Features nyingi zinapatikana kwenye more recent MIUI versions na kwenye simu za chini kama Redmi 9A kuna features nyingi unaweza usizipate.
Nitaongezea features nyingine soon.
 
Features mzuri ila design ya simu zao ni mbaya.
Simu za Xiaomi zipo nyingi sana na zina design tofauti tofauti, ni ngumu sana design zote zikuvutie. Mfano kwa hapa Bongo watu wengi hawapendi big circular camera module kama ya Xiaomi 12S Ultra, lakini Xiaomi ana design nyinginyingi. Mfano angalia hizi
Xiaomi 12 Pro
Xiaomi Redmi Note 10 Pro
Xiaomi 12T Pro
Mbona sioni ubaya wake[emoji849][emoji849]
 
Naendelea kuongeza features za kuvutia kwenye simu za Xiaomi na niliishia feature namba 22. Leo naongeza hizi hapa[emoji116][emoji116]

23. "Disable Ads" Feature
Xiaomi amekuja na njia ya kublock ads kwenye simu zake. Unaweza kublock ads za software ya MIUI kwa kupitia hatua rahisi za Settings app. Pia unaweza kublock ads za mitandaoni pia lakini inahitaji kupitia hatua nyingi kuliko kublock ads za MIUI. Lakini hizi hatua sio shida, hata kama ni nyingi kumbuka unablock mara moja tu basi.

24. Faster update feature
Xiaomi ni simu za China kwa hiyo wanapotoa new software na security updates za MIUI software huwa wanaanza kutoa China kwanza halafu za Global huchelewa kidogo. Siku hizi kuna feature ya Faster updates ambayo unaweza kuenable kupitia settings na inakuruhusu kupata updates ambazo hazijaachiliwa katika eneo unaloishi. Kwa hiyo MIUI update ikiachiwa China na wewe wa Nachingwea pia unapata.

25. Quick Ball
Hii ni feature inayokusogezea favorite apps zako zote kwa ukaribu zaidi kupitia kiduara kidogo ambacho kinakaa pembeni kabisa kwenye display yako. Quick Ball inakuwezesha kuaccess your favorite apps kwa haraka zaidi

26. Xiaomi MiraCast
Xiaomi MiraCast inakuruhusu kucast content yoyote kutoka kwenye simu yako kupitia TV yoyote yenye casting feature au aina yoyote ya monitor au hata laptop.

27. Clean Speaker
Speaker zimekuwa zikiingia vumbi au mchanga na kufanya zisitoe sauti nzuri ipasavyo. Kama maajabu vile, feature ya Clean Speaker (au Clear Speaker) kwenye simu za Xiaomi inakusaidia kusafisha speaker hizo bila wewe kuhangaika kwa sekunde 30 tu. Xiaomi inadai unapaswa kurudia kutumia feature hii mara 2 hadi 5 kulingana na kiasi cha vumbi kwenye speaker yako. Xiaomi wenyewe ndio wanajua feature hii inafanyaje kazi kwenye speaker yako, kweli teknolojia imekua.

28. Optical Character Recognition
Hii ni feature inayokuruhusu kusoma maandishi yaliyopo kwenye picha yoyote ile, au hata documents. Kwa mfano ukipiga picha bango lenye maandishi ya Kifaransa au Kichina simu yako inaweza kusoma maandishi hayo na feature hii haiishii hapo, inaweza hadi kutafsiri maandishi hayo kutoka lugha moja hadi nyingine na kukufanya uelewe.

29. Snap Mode & Camera enhancement
Hii ni feature inayokuwezesha kupiga picha huku kioo cha simu kikiwa kimezima ili kutunza chaji. Kupiga picha, unapress na kuhold volume down button na picha zitapigwa wakati screen ipo off. Unaweza hata kutoa sauti ya kupiga picha ikiwa unataka kupiga picha za siri.

30. Personalized Health App
Simu za Xiaomi zinakuja na application ya afya inayoitwa Mi Health ambayo ni next level kuliko health apps nyingi. Mi Health inaweza kufanya vitu vingi mfano kurekodi idadi ya hatua unazopiga kwa siku, na activities nyingine unazofanya kama kuogelea, kulala, kutembea, kukimbia na hata kuhesabu mapigo ya moyo. Pia inaweza kutrack tabia zako wakati wa kulala mfano kukoroma, n.k.

31. Calamity warning
Simu za Xiaomi zinakuja na AI feature inayoweza kukupa tahadhari juu ya majanga mbalimbali yanayoweza kutokea mfano matetemeko ya ardhi, tsunami au kimbunga kikali, milipuko ya mabomu na kadhalika. Vyote hivi vinawezeshwa na Artificial Intelligence.

Nimeshataja features 31 tofauti tofauti za simu za Xiaomi. Lakini bado kuna features nyingi sana. Nitakuja kuziongeza siku nyingine kwenye hiihii thread.
 
Ni toleo gani hilo lona specification hizi mkuu! Na bei yake!!?
Features nyingi hapa zipo MIUI 12 na kuendelea. Kwa hiyo ukinunua simu kama Redmi Note 10 kwenda juu, Xiaomi Mi 11 kwenda juu, au simu nyingi tu za Xiaomi zenye hiyo MIUI 12 kupanda utakuta hizo features.
Redmi Note 10 ni around 450000/=, Simu za mamilioni zina features nyingi zaidi.
Pia unapaswa kujua features nyingi zipo kwenye software kwa hiyo Xiaomi nyingi sana katika bei tofauti tofauti zina hizi features.
 
Ahaa! Ok
 
Umesahau features ya ukiwasha tochi kuzima una bonyeza power button Tu pia, pia data sio lazima uzime ikiwa unatumia itajiwasha na usipotumia itazijima, vile vile Sim nyingi za xiaomi zina infrared kukuwezesha kutumia kama remote. Second space Ndio mzigo mtamu hasa km simu yako hushikwa shikwa ukiwa kwenye xiaomi hilo wamezingatia unaweka vitu vyako tofauti na first second unatumia application tofaut Na second space yaan haziingiliani Hata msg iingie first second wakati huo wewe upo second itakujulisha tu ujumbe umeingia na huwezi kuingia mpaka uweke password yake
 
Dah, natumia Redmi 11 zaidi ya miezi 7 lkn sikuwahi kujua ina mambo mazuri hivi.

Pia kama kuna anayefahamu namna ya kupata camera nzuri kwa hizi simu atuelimishe tafadhali.

Thanks for sharing.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…